Wakati akipiga picha za dokumentari nchini Cambodia, mtayarishaji wa filamu Roberto Serrini alipata wasaa wa kutembelea vijiji kadhaa vya mjini na vijijini katika nchi hiyo. Timu yake ilitumia ndege aina ya DJI Phantom na kamera ya GoPro kupata picha za uzuri halisi wa Cambodia. Alielezea zoezi hilo la upigaji picha kama ‘uzoefu wa mzuri ajabu':
Kwenye eneo la Phnom Pehn na kwenye kijiji cha Anluk Leak, niliweza kuchnguza uzuri wa kifilamu wa nchi hii nzuri kutoka angani.
Uzoefu mzuri ajabu sana, kwa sababu wengi wa watoto hawa hawjawahi kuona televisheni, achilia mbali ndege inayopaa angani; mchanganyiko wa mvuto, msisimko na maajabu ya wanachokiona ndilo lilikuwa likionekana kwenye nyuso zao.
Hapa chini ni baadhi ya picha za kwenye mtandao wa Flickr zinazoelezea safari ya Roberto nchini Cambodia:
*Video na picha za Roberto Serrini, zimetumiwa kwa ruhusa yake.
2 maoni
Bahatimganwa@yahoo.com
kiongozi bola niyule anae fuata maadili yanchi nawatalifu watanzania tunapaswa kufanya mabadiliko