Maandamano ya Kudai Uhuru Yafanyika Kwenye Miji ya Saudi Arabia.

Makundi madogo ya wanawake wa Saudi Arabia, kwa wakati mmoja waliitisha “maandamano ya kudai uhuru” katika maeneo mbalimbali ya majiji ya Saudi Arabia mnamo Juni 10, 2013. Maandamano hayo yaliratibiwa na kikundi kisichofahamika cha mawakili @almonaseron [ Waunga mkono], lengo likiwa ni kushinikiza kuachiwa huru kwa ndugu zao waliofungwa gerezani. Matokeo yake ni kuwa, kwa kipindi cha siku mbili zilizopita, zaidi ya waandamanaji 140, wanawake kwa wanaume walitiwa nguvuni na maofisa wa polisi wa Saudi Arabia.

Vyanzo huru vya utetezi wa haki za binadamu vinasema kuwa, kuna mahabusu wanaokadiriwa kufikia 30,000 [ar], wengi wakiwa ni wale waliotiwa nguvuni wakati wa “vita ya ugaidi ya 9/11 . Wanaoshikiliwa walitiwa nguvuni bila ya hati ya kimahakama ya kuwakamata na hawakuwahi kuwa na mawasiliano yayote na wanasheria na wala kuhojiwa. Maandamano yanapingwa vikali nchini Saudi Arabia kiasi kwamba wanaoshiriki katika maandamano, pindi wanapokamatwa, hukabiliwa na adhabu ya kutumikia jela kwa miezi mingi. Hata hivyo, pamoja na karipio hili, kamwe haikuwazuia ndugu wa wafungwa hao kuitisha maandamano katika makundi madogo madogo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Majira ya saa10:55 jioni, @almonaseron alitangaza kuanza kwa maandamano, na alitwiti [ar]:

بدأ #اعتصام_الحرية نساء في عدة مناطق في آن واحد فعلى أهالي المعتقلين الإنضمام إليهم فوراً

@almonaseron: mikutano kwa ajili ya kudai uhuru imeanza hivi punde: wanawake katika maeneo mbalimbali wanakutana kwa wakati mmoja. Ndugu wa watu wanaoshikiliwa, hawana budi kuungana nao haraka iwezekanavyo.

Huko Riyadh, kikundi cha wanawake, baadhi yao wakiwa ni miongoni mwa ndugu wa Suliman al-Roushodi, ambaye ni kiongozi wa Jumuia ya Haki za Kisiasa na Kiraia ya Saudi Arabia, walikusanyika mbele ya jengo la Utaifa na Haki za Binadamu lenye ufadhili wa serikali, mahalipofanyia maandamano mapema mwezi Februari . Miongoni mwa waandamanaji hao, alikuwapo mtoto wa Bahia al-Roushodi, ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi minne mara baada ya maandamano hayo. Haukupita muda, walizingirwa na zaidi ya magari 30 ya polisi [ar], na na kisha dereva wao kutiwa nguvuni [ar] na wote walizuiwa kuondoka. Moja ya barabara kuu za jiji la Riyadh, Barabara ya Mfalme Fahad, ilifungwa na polisi wakati wa pilika pilika nyingi ili kuweza kukabiliana na mikutano ya waandamanaji. Mnamo saa 12:20 jioni, mmoja wa waandamanaji, ambaye ni mke wa, al-Roushodi, alitwiti:

تم اعتقالنا واعتقال اخي

@omamar1: walitutia nguvuni, na pia walimtia nguvuni kaka yangu.

Relatives of the arrested women protesters gathered in front of the prison where they were reportedly held. Photograph shared by @fatma_mesned on Twitter

ndugu wa waandamanaji wanawake waliokamatwa wakiwa wamekusanyika mbele ya gereza lililotaarifiwa kuwa ndiko walikokuwa wameshikiliwa. Picha imewekwa na @fatma_mesned katika ukurasa wa Twita

Mnamo saa 5:44 usiku, ndugu wa waandamanaji wanawake waliokamatwa wakiwa wamekusanyika mbele ya gereza lililotaarifiwa kuwa ndiko walikokuwa wameshikiliwa, mjukuu wa kike wa al-Roushodi, Fatima al-Mesned alitwiti:

الآن مجتمعون امام سجن الملز قسم النساء لمن اراد المطالبه بمعتصمات #الرياض انصروا من نصر أسرانا

@fatma_mesned: kwa wale wanaoshinikiza kuachiwa huru kwa waandamanaji: kwa sasa tupo mbele ya gereza la al-Malez, upande wa wanawake. Waunge mkono wale waliowaunga mkono wenzetu waliofungwa jela.

Huko Buraydah, wanawake walikusanyika mbele ya mahakama kuu ya Jiji, na kwa muda mfupi wanawake wengi waliungana na wenzao kwenye mkutano huo wa kudai uhuru. Majira ya saa11.52 jioni, wanausalama wa Saudi Arabia waliwazingira waandamanaji [ar]. Pale kijana mdogo alipojaribu kuwapa maji waandamanaji, alikimbizwa na wanausalama na kisha kutiwa nguvuni [ar]. Askari kanzu waliovalia nguo za kiraia waliwaamuru wanawake hao waondoke na kisha kuwatishia, lakini walikataa kuondoka hadi pale ndugu zao watakapoachiliwa huru (video [ar]). Idiadi ya wanawake waliokuwa wakiandamana iliongezeka hadi pale polisi walipotumia nguvu kuwatia nguvuni waandamanaji. Mapema saa 2.24 usiku, @almonaseron alitwiti:

الآن تم أركاب المعتصمات للباصات في بريدة بالقوة

@almonaseron: wanawake walilazimishwa kuendesha mabasi ya polisi.

Siku iliyofuata, Juni 11, saa 11 jioni, kundi lililokuwa na wanaume na wanawake lilikusanyika kupinga kukamatwa kwa waandamanaji kulikotokea siku iliyotangulia. Ndani ya dakika kadhaa, walizingirwa na maafisa usalama wa dharura [ar], beaten [ar] na kisha kukamatwa.

Mikusanyiko mingine midogo ilifanyika huko Mecca, Aljouf na Hial.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.