Sudani: Maandamano Yachochea Kukamatwa kwa Mwanaharakati wa Twita

#MwanchieUsamah

Maandamano ya jana yalisababisha polisi wakishirikiana na maafisa wa Usalama wa Taifa kuwakamata waandamanaji wengi katika mitaa kadhaa. Miongoni mwao alikuwa mtumiaji wa twita na mwanaharakati ambaye ni raia wa Sudani Usamah Mohammed Ali.
(@simsimt). Katika twiti yake ya mwisho, Usamah alikuwa akifanya utetezi wa maudhui huru kusaidia kusambaza habari za matukio yanayoendelea katika mitaa ya jiji la Khartoum:

Kiukweli, ni kwamba ninajaribu kufanya ujanja. Unaweza kutumia twiti zangu bila hata kunitaja. Utetezi wa maudhui huru!

Twiti chache za mwisho za Usamah zilikuwa pia na taarifa kuhusu mahali alipo na hali ilivyo katika eneo alipo. Alikuwa kwenye eneo la Burri karibu tu na Mtaa wa Nile[ar]:

في بري الشريف. عدد كبير من بكاسي الاحتياط والأمن ودفارات الشرطة والأهالي بأعداد متفرقة واقفين. ‎#جمعة_الكتاحة

Niko Burri al-Sharif. Kuna idadi kubwa ya magari ya Usalama na Polisi na wakazi wa eneo hili wamesimama barabarani kwa wingi.

mahali hapo, alisema walikuwepo wanausalama wengi na watu walikuwa wakikamatwa

الأمنجية أعدادهم كبيرة ومتمركزين في أكتر من بوكسي. في بحري الشفناهم كانو مسلحين. أفتكر كلهم بكونو كدة. ‎#جمعة

Kuna idadi kubwa ya maafisa wa Usalama na wapo katika gari zaidi ya moja. Huko Khartoum Kaskazini, tuliwaona wale wenye silaha. Nadhani ndivyo walivyo wote, wana silaha.

Alitwiti picha ya watu wakimatwa na watu wa usalama, dakika chache kabla na yeye mwenyewe kukamatwa.

بوكسي الأمن دة وقف العربية السيلفر الواقفة وراو وطلعو منها زول وركبو معاهم. العربية فيها أولاد وبنات. ‎#جمعة_الكتاحة

Gari hili la Usalama wa Taifa lilizuia gari lenye rangi ya shaba lililokuwa limeegeshwa na kumtoa mtu humo. Walimchukua wakaondoka naye kwa kutumia gari lao. Gari limejaa watoto wa kiume na kike.

Masaa mawili kabla ya kukamatwa kwake, Usamah alihakikisha anawaarifu watu kuwa alikuwa akifuatana na kaka yake aitwaye Asaad, (@Arch_Asaad), ambaye naye hali kadhalika aliwekwa kizuizini lakini akiachiwa muda mfupi baadae

أنا معاي ‎@Arch_Asaad عشان بس لو حصلت اي حاجة.

Niko na Asaad, ikitokea chochote kimenipata

Asaad alitwiti mara tu baada ya kuachiwa kwamba hakuwa anajua aliko Usamah.

@simsimt hajaachiwa bado! Na sijui aliko!

Kwa mujibu wa Asaad, Usamah alipelekwa kwenye jengo la makao makuu ya Idara ya usalama wa Taifa yaliyopo Khartoum Kaskazini wakati yeye mwenyewe alipelekwa kwenye kituo cha polisi mjini Khartoum.

Rafiki za Usamah walitwiti kuonyesha mashaka na usalama wa Usamah wakitaka aachiwe huru mara moja.
Ayman Elkhidir alionyesha hofu yake kwa usalama wa Usamah,

Mwanaharakati na mtumia twita @simsimt alikamatwa na Usalama wa Taifa jana #FreeUsamah #SudanRevolts #السودان_ينتفض

Montaga Elameen aliwataka watu kusambaza habari juu ya watu wote waliokamatwa katika maandamano hayo:

Endeleeni kutwiti na kupiga simu kuhusu watu waliokamatwa @simsimt & @OmarMahgoub ‪#FreeOmer‪#FreeUsamah ‫#السودان_ينتفض‪#Sudan_Revolts

M-Misri Mohammed Al Dahshan, mwanahabari, mwandishi wa vitabu na rafiki binafsi wa Usamah, naye alikuwa na hofu na usalama wake,
alitwiti :

Habari za usiku. Bila shaka kesho tutapata habari nzuri kutoka
‪#Sudani, na Mungu akijalia
@Simsimt, Ahmed Hussein, na wote wengine watakuwa huru.

Mapema siku hiyo, Usamah alirekodi picha ya video kwa ajili ya kipindi cha Al Jazeera kinachowapa fursa watazamaji kutuma video walizotengeneza wenyewe kiitwacho ‘The Stream’ akionyesha sababu zake za kuingia mtaani tarehe 30 Juni 2012 –siku iliyopangwa kuwa kwa ajili ya maandamano, na ndiyo siku ambayo chama tawala cha nchini hiyo cha NCP kitakuwa kikiadhimisha miaka 23 tangu kushika dola.

Wa-Sudani wengine kadhaa wanaotumia mtandao wa twita wamekamatwa na kuachiwa, kama Omer Mahgoub (@OmarMahgoub), ambaye aliachiwa leo. Alikuwa ameshikiliwa kwenye jengo hilo hilo aliko Usamah, ingawa anasema hakumwona.

Usamah amekuwa kwenye kizuizi cha Idara katili ya Usalama wa Taifa kwa zaidi ya masaa 24, na marafiki wake wa twita wanafanya kampeni ya kuachiwa kwake kwa kutumia alama habari ya #FreeUsamah.

Tangu kuibuka kwa maandamano haya yanayoendelea jijini Khartoum na katika majimbo yote kushinikiza kuanguka kwa utawala wa nchi hiyo, waandamanaji wengine wengi waliokuwa wakiandamana kwa amani wamekuwa wakitekwa na Idara ya Usalama wa Taifa hilo na wengi wao wanateswa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.