Misri: Watu 10 Wenye Ushawishi Zaidi Nchini

Mwanablogu Ahmed Shokeir aliendesha taftishi ya kutafuta watu 10 wenye ushawishi zaidi nchini Misri baada ya kushangazwa na matokeo ya Gamal Mubarak, mtoto wa Rais Hosni Mubarak wa Misri – kama mmoja wa washindi 100 wa mwisho wa mwaka 2009 wa TIME.

Shokeir anaandika:

المفاجأة الحقيقة كانت في إسم الشخصية العربية التالية والتي تظهر في القائمة أيضا للمرة الأولى وتحتل المركز الثامن عشر بفارق بسيط عن الشيخ أحمد وتحصل على ثمانمائة وثلاثون ألف صوت بمتوسط 31 نقطة وهو جمال مبارك متقدماً على أسماء مثل بريتني سبيرز التي حلت في المركز الثلاثون وباراك أوباما في المركز السابع والثلاثون

Jambo la kushangaza sana lilikuwa kwamba Mwarabu wa pili mwenye ushawishi zaidi baada ya Shehe Ahmed bin Zayed Al Nahyan, ambaye ni mkurugenzi wa Abu Dhabi Investment Authority, aliyeshika nafasi ya 13 baada ya kupata kura 839,000. Kwa mara ya kwanza jina la Gamal Mubarak limejitokeza katika nafasi ya 18 ya orodha baada ya kupata kiasi cha kura 832,593. Gamal Mubarak alimshinda Britney Spears (aliyeshika nafasi ya 30) na Barack Obama (nafasi ya 37).

Zeinobia alikuja na orodha ya watu 10 wenye ushawishi zaidi nchini Misri kwa mujibu wa taftishi ya Shokeir:

Kwanza kabisa huwa hatuna aina hii ya ushindanishaji nchini Misri mara kwa mara, pili huna budi kutambua kwamba jambo hili liliendeshwa kwenye blogu ya nchini Misri, washiriki wanaweza kusemwa kwamba ilikuwa ni sampuli ndogo sana katika jamii ya Wa-Misri “Zaidi ya washiriki 120 kwenye blogu yake na zaidi ya washiriki 300 kwenye tukio katika face book” na kwa hiyo baadhi ya watu huenda watasema kwamba sampuli haikuwa wakilishi vya kutosha, hata hivyo, kwa namna ya kushangaza kabisa, baadhi ya majibu yanawakilisha maoni ya Wa-Misri walio wengi.

Akitunza kile kizuri ili kukitoa mwishoni kabisa, Zeinobia alianza na washindi bora 9:

Katika nafasi ya 10 yenye pointi 168 yupo kocha wa timu ya taifa ya soka ya Misri Hassan Shahata.
Katika nafasi ya 9 yenye pointi 181 ni mfanyabiashara Naguib Sawiris.
Katika nafasi ya 8 yenye pointi 200 ni Rais Hosni Mubarak. “kura 26″
Katika nafasi ya 7 yenye pointi 200 ni mwandishi wa habari Ibrahim Eissa. “Kura 46″
Katika nafasi ya 6 yenye pointi 202 ni mfanyabiashara Ahmed Ezz.
Katika nafasi ya 5 yenye pointi 215 ni mwanasayansi Ahmed Zowail.
Katika nafasi ya 4 yenye pointi 262 ni mwendesha kipindi cha TV Mona El-Shazely.
Katika nafasi ya 3 yenye pointi 325 ni mcheza soka Mohamed Abu-Tarika.
Katika nafasi ya 2 yenye pointi 364 ni Gamal Mubarak.

Sasa kuhusu mtu mwenye ushawishi zaidi nchini Misri,

Na kwa mshangao wangu mkubwa:

Katika nafasi ya 1 yenye pointi 496 ni Mhubiri wa dini ya Kiislamu kwenye TV Amr Khalid.
Hakuna shaka kwamba hao wengine tisa ukitoa Ahmed Zoweil wamekuwa na nafasi ya pekee katika maisha yetu katika mwaka 2009,lakini Amr Khalid!!??

Zeinobia anatambua kwamba:

Taftishi hii ilikuja katika kilele cha matukio ya Khalid hasa kwa umaarufu wake kutokana na vipindi vyake vya TV vya wakati wa Ramadhani, hivyo hicho kilichangia sana matokeo hayo na bila shaka nafasi ya dini katika maisha yetu.

Hata hivyo, bado anajiuliza kama kweli alistahili kushika nafsi ya kwanza kwenye orodha hiyo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.