GlobalVoices katika

Irani: Vuguvugu la Kijani Laupinga Utawala Tena

TafsiriMakala hii inapatikana pia katika:

Malagasy · Iran: Nihaika ny fitondrana indray ny Hetsika Maitso
Deutsch · Iran: Die Grünen Bewegung trotzt wieder dem Regime
Français · Iran : Images de la "révolution verte" défiant le gouvernement
Italiano · Iran: video delle nuove proteste del Movimento Verde
polski · Iran: Zielony Ruch znów sprzeciwia się rządowi
简体中文 · 伊朗:在野阵营再度上街
繁體中文 · 伊朗:在野陣營再度上街
বাংলা · ইরান: সবুজ আন্দোলন আবারো বিরোধিতা করলো শাসকদের
English · Iran: Green Movement defies regime again


Upande wa upinzani wa Vuguvugu la Kijani nchini Irani mnamo tarehe 4 Novemba mwaka huu (13 ya Abani) uliendesha maandamano makubwa ya mitaani, baada ya kutumia fursa ya maandamano rasmi yaliyoendeshwa siku hiyo ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 30 ya ukaliaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Teherani. Maandamano hayo ya upinzani yalikabiliwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi ya kuyavunja yaliyofanywa na vikosi vya usalama.

Kama ambavyo sasa imekuwa jambo la kutarajiwa, vyombo vya habari vya kiraia vya Irani vilirekodi ‘historia' hiyo kupitia simu zao za mkononi.

Waandamanaji jijini Teherani walikanyagakanyaga picha ya Kiongozi Mkuu wa Kidini nchini humo, Ayatollah Ali Khamenei, kitendo ambacho wala kisingefikiriwa miezi michache tu iliyopita.

Ujumbe kwa Obama: Ama uko upande wetu au uko upande wao.

Kiongozi wa upinzani, Mehdi Karoubi, akiwa katikati ya watu.

Vikosi vya Usalama vikishambulia waandamanaji.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Taratibu

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.


Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha