Habari kuhusu Naija

Baada ya Maandamano Burkina Faso na Burundi, Naija na Togo Zinafuata?

  8 Juni 2015

Wanaija 20,000 wameingia mitaani mjini Niamey, Naija mnamo Juni, 6. Kuna ababu nyingi za maandamano hayo: umaskini uliokithiri, utawala mbovu na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza yakiwa ni moja wapo ya malalamiko ya asasi za kiraia nchini humo. Maandamano kama haya yalitokea katika nchi za Burkina Faso, Burundi na Togo....

Vijana wa Naija Wacharuka Kufuatia Shambulizi la Boko Haram huko Bosso na Diffa

  8 Februari 2015

Kwa mara ya kwanza, Boko Haram kimetekeleza shambulio kwenye mpaka na Naija na vijana wa ki-Naija hakuweza kuvumilia. Boko Haram walishambulia Bosso na Diffa, miji miwili iliyo kusini mashariki mwa Naija kwenye mpaka wa nchi hiyo na Naijeria lakini walirudishwa nyuma na majeshi ya Chad na Naija. Boko Haram imepoteza...

Niger Yapata Kituo Chake cha Kwanza cha Reli Baada ya Kusubiri kwa Miaka 80

  11 Aprili 2014

Aprili 7, Niger ilizindua katika mji mkuu wa Niamey kituo chake cha kwanza cha treni kuwahi  [fr]. Mamlaka tayari ilikuwa na makadirio ya ujenzi wa kituo cha treni miaka 80 iliyopita lakini mradi kamwe haukuanzishwa. Tukio hilo litaanzisha ujenzi wa reli kati ya Niger, Benin, Burkina Faso na Côte d'Ivoire....

Mradi Mkubwa wa Reli Kati ya Mji wa Niamey na Cotonou Kuanza

  4 Novemba 2013

Mradi wa reli wa urefu wa kilometa 1,500 kati ya Niamey, mji mkuu wa Niger na Cotonou, mji mkuu wa Benin umepitishwa na mamlaka ya nchi hizo mbili na ujenzi utaanza Machi 2014 [fr].  Francois Ndiaye katika Niamey anaelezea kuhusu makubaliano ya fedha [fr] inayojumuisha wadau mbalimbali na itasimamiwa na kundi la uwekezaji...

Wahamiaji 87 Wafariki kwa Kukosa Maji Kaskazini mwa Niger

  4 Novemba 2013

Mnamo tarehe 30 0ctoba, watu 87 waliokuwa wakijaribu kuifikia bahari ya Mediterania walifariki mara baada ya madereva waliokuwa wakiendesha magari waliyoyatumia kusafiria kuwatelekeza wahamiaji hao katika Jangwa la Sahara. Wahamiaji hawa walihangaika kutafuta msaada bila ya mafanikio. Simulizi ya kuhuzunisha kutoka kwa mmoja wa watu walionusurika aliyejulikana kwa jina la...

Shambulio la Mabomu Mawili ya Kujitoa Muhanga Nchini Niger Yaua Watu 23

  24 Mei 2013

Benjamin Roger wa Jeune Afrique anaripoti [fr] kuwa wanajeshi 18, raia mmoja na magaidi wanne waliuawa mapema subuhi ya leo katika shambulio la mabomu ya kujitoa Muhanga kwenye gari mjini Agadez, Niger tarehe 23 Mei. Anaongeza kuwa wanafunzi wa chuo cha kijeshi wametekwa na gaidi mwingine kufuatia mabomu hayo. Wakati...