Habari kuhusu Benin

Jinsi Mabadiliko ya Hali ya Hewa Yanavyowaathiri Wakaazi wa Vijiji Nchini Benin

  20 Juni 2014

Mbenin, Alain TOSSOUNON, alipachika muhtasari wa ripoti kwenye blogu ya Mtandao wa Afrika Magharibi wa Waandishi wa Habari Unaohusu Maji na Usafi wa Mazingira (WASH). Ripoti yenyewe ilishughulikia tathmini ya mahitaji ya baada ya maafa nchini Benin kufuatia mafuriko makubwa ya hivi karibuni. Maafa hayo yalisababisha vifo vya karibu watu...

Mradi Mkubwa wa Reli Kati ya Mji wa Niamey na Cotonou Kuanza

  4 Novemba 2013

Mradi wa reli wa urefu wa kilometa 1,500 kati ya Niamey, mji mkuu wa Niger na Cotonou, mji mkuu wa Benin umepitishwa na mamlaka ya nchi hizo mbili na ujenzi utaanza Machi 2014 [fr].  Francois Ndiaye katika Niamey anaelezea kuhusu makubaliano ya fedha [fr] inayojumuisha wadau mbalimbali na itasimamiwa na kundi la uwekezaji...

Benin: Kampeni ya Kusaka Wahalifu Yawagawa Wananchi

  7 Julai 2013

Ikiwa imezinduliwa na wizara ya Mambo ya Ndani, Ulinzi wa Umma na Dini, kampeni ya Djakpata yenye lengo la kuwasaka wahalifu wote wanaojihusisha na shughuli zisizo halali ambazo zinaweza kuhatarisha hali ya utulivu ya wananchi wa Benin. Hata hivyo, kwa siku chache zilizopita, wananchi wamekuwa na maoni tofauti sana kuhusu jambo hili.

Matatizo Makuu ya Raia wa Benin ni Yapi?

  7 Juni 2013

Tite Yokossi anafunua matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Mfuko wa Zinsou ambao uliwauliza wananchi wa Benin ni yapi ndiyo matatizo yao makuu leo [fr]. Tatizo la kwanza lililoorodheshwa lilikuwa uwezo mdogo wa kufanya manunuzi miongoni mwa watumishi wa umma. Mengineyo ni uwezekano wa kupata fursa ya elimu, huduma ya maji safi, huduma...