Habari kuhusu Sri Lanka

Mapigano Dhidi ya Waislamu Yaendelea Nchini Sri Lanka

  30 Juni 2014

Yametimu majuma mawili tangu ghasia dhidi ya Waislamu kwenye majiji ya pwani nchini Sri Lank- Aluthgama na Beruwala. Ingawa hali imetulia baada ya kulaaniwa sana kila sehemu, bado ghasia hizo dhidi ya Waislamu zinaendelea katika maeneo tofauti ya Sri Lanka. Mwanablogu Abdul Khaleq anatwiti kuhusu tukio moja huko Ratmalana sehemu...

Wanawake wa Sri Lanka na Mbinu za Kuzuia Mimba

  26 Machi 2014

Mwandishi, Mpiga picha na mwanablogu Meg at Life in Lanka anaripoti kuwa kwenye sehemu za vijini nchini Sri Lanka baadhi ya wanawake hawana kauli kuhusu aina ya mpango wa uzazi wanaoutaka. Waume zao hawatumii kondomu na wanapenda wake zao watumie mbinu nyingine za kupanga uzazi; kwa hiyo njia rahisi inayopatikana...

Vyombo Vikuu vya Habari Vyaihujumu Facebook

  24 Februari 2014

Mwanablogu wa Teknolojia Amitha Amarasinghe anadai kwamba mtandao wa Facebook unapewa taswira hasi na vyombo vikuu vya habari nchini Sri Lanka kwa vichwa vya habari kama “Mwanafunzi ajiua shauri ya picha iliyowekwa Facebook”, “Mapenzi ya Facebook yaishia na kifo” na kadhalika. Ghafla tu, kuna mwongezeko mkubwa wa maudhui yanayotoa taswira...

Sri Lanka: Wanablogu Watathmini Kifo cha Kiongozi wa LTTE

  19 Mei 2009

Serikali ya Sri Lanka imetangaza kwa kupitia vyombo vya habari vya taifa pamoja na ujumbe wa simu za mkononi mchana leo (Jumatatu, 18 Mei, 2009) kwamba kiongozi wa Kundi linalotaka kujitenga la Wa-Tamil, the Liberation Tigers of Tamil Eelam (LTTE), Vellupillai Prabhakaran, amefariki. Salamu za rambirambi zinaashiria kwamba alikuwa shujaa kwa baadhi ya watu kadhalika wengine walimchukulia kama muuaji katili. Wanablogu wa Ki-Sri Lanka wanatathmini urithi wa kiongozi huyu wa vita na maana ya kifo chake kwa mustakabali wa Watamil na watu wa Sri Lanka.