Habari kuhusu Peru

Mwizi Akamatwa, Aomba Msamaha na Kusamehewa

  19 Aprili 2015

Labda alidhani ingekuwa vyepesi kuiba shampoo mali ya mmiliki wa duka nchini Peru, lakini mambo yalimwendea mrama mwizi huyu. Mtu mmoja akiwa ameongozana na mwenzake waliingia kwenye duka lililoko kwenye jiji la Huancayo nchini Peru, wakisema walikuwa wanataka kununua pombe, na mmiliki alipokuwa amepumbazwa kidogo, jamaa walibeba boksi la shampoo....

Jumuiya ya Kimataifa na Mgogoro wa Ukraine

  24 Mei 2014

guest blogs [es] ya Angie Ramos [es] katika Tintero kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine na baada ya kuchambua mambo mbalimbali muhimu husika anahitimisha kwa majibu ya Jumuiya ya Kimataifa: Jambo ni, jumuiya ya kimataifa, inayokabiliwa na kesi kama hii, hufanya vitendo watakavyo kwa kuwa inategemea ukubwa wa maslahi yanayoshiriki...

Peru: Wafanyabiashara Wachoma Nguo Kupinga Bidhaa za Kichina

  2 Septemba 2013

Wafanyabiashara kutoka eneo la Gamarra [es], kituo maarufu cha viwanda vya nguo na ambako ndiko lilipo eneo la kibiashara jijini Lima, walichoma nguo zilizoingizwa kutoka China [es] katika mitaa kupinga biashara hiyo ya nguo zinazouzwa bei ndogo ambazo, kwa mujibu wao, hufanya biashara zao kufilisika. Kwenye mtandao wa Twita, Alfredo “Alial” (@ Alfredo_jch) [es] alipendekeza...

Peru: Mchezaji wa Kandanda Afariki Dunia Uwanjani

  22 Julai 2013

Dakika tano kabla ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu zaReal Garcilaso na Sporting Cristal, mchezaji nyota wa timu ya Sporting Cristal mwenye miaka 18 Yair José Clavijo alipata mshituko wa moyo na akapoteza maisha. Madaktari wa timu hiyo walijaribu bila mafanikio kunusuru hali yake akiwa kwenye sehemu ya kuchezea...

Peru: Kampeni ya Kuzuia Kufungwa kwa Maktaba ya Amazon

  11 Novemba 2010

Juan Arellano wa Globalizado [es] anaripoti juu ya kampeni ya kuzuia kufungwa kwa maktaba huko Iquitos, Peru , maktaba ambayo inatilia mkazo vitabu na masuala yanayohusu Amazon. Maktaba hiyo ni ya pili kwa umuhimu katika masuala ya Amazon huko Marekani ya Latini.