Habari kuhusu Macau (China)
Macau: Watu 3,000 Wazunguka Baraza la Wawakilishi Kukwamisha “Muswada wa Walafi”
Taarifa zaidi zinapatikana kwenyetaarifa yetu ya awali ya GV.
PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”
Muswada utampa mkuu wa serikali jimboni Macau, nchini China, kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai wakati akiwa madarakani na ataaendelea kupata mshahara wake hata baada ya kuondoka madarakani.
Maandamano Yasitisha Ujenzi wa Mtambo wa Nyuklia Kusini mwa China
Kufuatia siku tatu mfululizo za maandamano, inaonekana kuwa serikali ya Manispaa ya Heshan katika jiji la Jiangmen imesitisha mpango wake wa ujenzi wa mtambo mkubwa wa nishati ya Nyuklia. Baadhi ya watu wanaamini kuwa ushindi huu ni wa muda mfupi tu. Wana wasiwasi kuwa, mradi huu unaweza kuibukia sehemu nyingine karibu na Delta ya mto Pearl, Kusini mwa China mahali palipo na idadi kubwa sana ya watu.