Habari kuhusu Majadiliano kwa Dunia Bora

Bolivia: Uhaba wa Maji Kwa Sababu ya Theluji Inayoyeyuka

  7 Novemba 2009

Safu ya milima ya Chacaltaya ina baadhi ya vilele ambavyo ni alama zenye maana katika safu ya milima Andes iliyopo Bolivia. Kwa kuwa ilikuwa ni sehemu moja pekee ambapo mchezo wa kuteleza barafuni uliweza kufanyika katika nchi hii ya milimamilima, milima hii ni maarufu sana kwa wale walio kwenye Idara...

Amerika ya Kati: Kasi Kubwa ya Ueneaji wa Jangwa

  6 Novemba 2009

Ueneaji wa jangwa unasambaa kimyakimya lakini kwa kasi kubwa mahali pengi duniani na Amerika ya Kati haijaweza kukwepa hali hii iliyo na athari mbaya za kutisha. Wakati ambapo majangwa ni maumbo ya asili, ueneaji wa jangwa ni mchakato wa kuharibika kwa nyanda za ardhi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu unaofanywa na binadamu.

Ujauzito na Magereza: Afya na Haki za Wanawake Magerezani

  5 Novemba 2009

Mapambano bado yanaendelea kuhakikisha haki za binadamu kwa wanawake wajawazito duniani pote, ni inaelekea kwamba katika mchakato huo, wanawake waliopo magerezani wanasahauliwa. Je ni hatua zipi zilizochukuliwa kuhakikisha kuwa nao wanaangaliwa kwa utu, kwa kuzingatia uhai wanaoubeba.

Uanaharakati na Umama Barani Asia

  24 Oktoba 2009

Je, mwanamke anatoa sadaka zipi ili kupigania jambo analiamini? Je, watoto wake wanaathiriwa vipi na mateso yanayoelekezwa kwake? Makala hii inachambua kwa kifupi maisha ya wanawake wanaharakati katika Asia ambao pia ni ma-mama.