Habari kuhusu Kireno
Serikali ya Angola Yafungia Kituo cha Runinga cha Kibrazili kwa Madai ya ‘Kukiuka Taratibu’
Serikali yatoa ufafanuzi wa kukisimamisha kufanya shughuli zake kituo cha runinga cha Record TV África kwa kile kinachoelezwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wake hakuwa "mzawa" wa Angola. Hata hivyo, kituo hiki kilishafanya mabadiliko ya Mkurugenzi Mtendaji na kumweka raia mzawa.
Netflix kuonyesha filamu ya kwanza ya Angola
Dias Santana ni filamu ya Angola kwa 80% na AfrikaKusini kwa 20%
Waandishi Wa Habari wa Msumbiji Waachiwa Huru Baada ya Kukaa Kizuizini Kwa Miezi Kadhaa Bila Kufunguliwa Mashtaka
Amade Abubacar na Germano Adriano walikuwa kizuizini tangu Januari lakini walishtakiwa tu hapo Aprili 16. Kwa sasa wanasubiri shauri lao lisikilizwe wakiwa chini ya uangalizi.
Mshindani wa Msumbiji Ashinda Mashindano ya Kimataifa ya Kutunisha Misuli nchini Hong Kong
Saraiva ni mtu mashuhuri kwa kutunisha misuli nchini Msumbiji.
Kwa Mara ya Kwanza katika Historia ya Nchi, Mwanamke Aongoza Chuo Kikuu cha Umma Msumbiji
Nafasi yake ya Mkuu wa Chuo kikuu cha umma ni sawa na nafasi ya waziri katika Msumbiji.
Papa Francis Kutembelea Msumbiji Mwezi Septemba, Kipindi cha Kampeni ya Uchaguzi Mkuu
Msumbiji itakuwa na uchaguzi mkuu mwezi Oktoba na bado haijapata nafuu kutokana na kimbunga ambacho kimeharibu kabisa Beira ambao ni mji mkubwa wa pili.
Mtunga Sheria wa Kike wa Brazili Ashambuliwa Mitandaoni Kwa Kuvaa Nguo Zinazoonesha Maumbile
"Ushiriki wa wanawake wenye jamii ni mdogo kiasi kwamba suala la mavazi linaweza kukuzwa kupindukia."
Rais wa Angola Aamsha Hasira Kwenye Mahojiano Yake Akidai Hakuna Njaa Nchini Kwake
"Leo kuna chakula cha kutosha Angola, hakuna mtu anayeweza kusema eti Angola ina njaa. Kilichopo ni utapiamlo," alisema Rais wa Angola kwenye mahojiano.
Kwa nini Cuba Iliamua Kuwaondoa Madaktari Wao 8,000 Kutoka Nchini Brazili
Havana ilitangaza kusitisha makubaliano yake na Brazil kufuatilia kauli ya rais mteule Jair Bolsonaro kuhusu mradi ambao unadaiwa "kuwa hatari na unapungua thamani yake".
Tunaelewa Nini Kuhusu Uchaguzi Mkuu Ujao Nchini Msumbiji?
Mnamo Oktoba, 2019 Msumbiji itachagua magavana wake kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo. Kabla ya uchaguzi huu, magavana hawa waliteuliwa na rais.