Habari kuhusu Kikorea
Picha Mpya ya Korea Kaskazini ya Shirika la Anga la Marekani
Wasomaji wa kimataifa wanaofuatilia masuala ya Korea Kaskazini labda wangekutana angalau mara moja na picha hii maarufu ya rasi ya Korea kutoka Shirika la Anga la Marekani (NASA) kuonesha tofauti kubwa ya taa zinazoangaza usiku kwenye nchi hizo mbili za Korea. NASA hatimaye walihuisha picha zao za Satelaiti na ‘ina mwonekano mzuri kuliko picha ya...
PICHA: Vyama vya Wafanyakazi na Asasi za Kiraia Vyaandaa Mgomo
Huku ukiwa umepangiliwa ufanyike mwanzo wa kipindi cha pili cha Rais Park Geun-hye madarakani, takribani wa-Korea elfu 40 (polisi wanadai ni elfu 15) walifanya mgomo nchini kote. Mgomo huo, ulipangwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Korea, ukiwa na wito wa kusitishwa kwa kudhibitiwa kwa vyama vya wafanyakazi, hatua...
Rais wa Korea Kusini Aapa Kupambana Uzushi Unaoenezwa katika Mitandao ya Kijamii
Je, serikali ya Korea Kusini imejiandaa kwa kufuatilia mitandao ya kijamii? Matamshi ya hivi karibuni ya Rais Park (full transcript [ko]) yamewashitua wa-Korea wanaotumia mtandao. Park, akiwalenga “uvumi ule unaosambaa kupitia mitandao ya kijamii”, alisema “kama serikali ikiachia mambo haya yakaendelea, itakuwa ghasia nchi nzima” na kuongeza “kumbukeni mamlaka za nchi zinahitaji...
South Korea: Ahadi ya Rais ya Ustawi Iliyoshindwa Yakosolewa
Rais Park yuko kwenye wakati mgumu kwa r ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni kuwa angepandisha ruzuku ya pensheni gharama za mafunzo. Wakosoaji wanasema kampeni yake iliahidi kinyume na sera yake kama mgombea mhafidhina, ilimsaidia kuzoa kura katika uchaguzi uliopita. Akaunti ya mtandao wa twita wa @metempirics ilikusanya viunganishi vinavyohusika na...
Korea Kusini: Mpango wa Kuwakutanisha Wenzi Wakwama
Mpango mpya kabisa wa kuwakutanisha wenzi kwa njia rahisi katika mkesha wa Krismas nchini Korea Kusini hatimaye ulijikuta ukishindwa kabisa baada ya waliojitokeza asilimia 90 kuwa ni wanaume. Inasemekana zaidi ya watu 20,000 walijiandikisha na hata polisi walikuwepo kufuatia uwezekano wa vitendo vya ngono za kulazimisha. Mtumiaji mmoja wa mtandaoalibainisha [ko]...
Korea Kusini: Dikteta Kim Jong Il wa Korea ya Kaskazini afariki dunia
Kim Jong Il, dikteta wa Korea Kaskazini amefariki. Japokuwa kifo cha dikteta huyo mwenye sifa mbaya duniani ni jambo ambalo watu wanapaswa kulipokea vyema, watu wengi wa Korea Kusini wameonyesha wasiwasi juu ya hali tete katika bahari ya Korea itakayotokana na kifo chake cha ghafla.
Korea: Ziara ya Clinton Korea Kaskazini
Habari ya kushangaza. Kwa ghafla, Clinton alizuru Korea ya Kaskazini na kama vile 007 aliwarudisha nyumbani wanahabari wawili wa kike ambao walikuwa wameshikiliwa nchini Korea Kaskazini. Kuhusiana na habari hii ya ghafla, hakuna habari zilizowekwa kwenye vyombo vya habari vya umma vya Korea na hata kwenye maoni ya wanablogu. Zifuatazo...
Korea: Wajibu wa Kitaifa Wachuana na Dhamiri
Kijana mmoja anayetumikia jeshi kama askari polisi aliamua kutorudi kwenye kikosi alichokuwa akifanya kazi baada ya likizo na alipeleka taarifa kuwa dhamiri yake ilikuwa ikimshtaki. Sababu ilikuwa kwamba dhamiri yake ilimshtaki baada ya kuwa amewanyanyasa raia walioshiriki katika mkesha wa tukio la kuwasha mishumaa. Uamuzi wa kijana huyu umevuta hisia...