Habari kuhusu Kibangla
Bangladesh: Jengo Laporomoka, Mamia Wauawa kwenye Vifusi
Janga jingine tena la kiwanda nchini Bangladesh, safari hii jengo la ghorofa tisa lilianguka na kuua zaidi ya watu 142 na watu wengine karibu elfu moja kujeruhiwa. Watu wengine wengi bado wamenaswa kwenye kifusi na harakati za kuwaokoa bado zinaendelea. tukio hili linatokana na uzembe wa baadhi ya watu kwani utawala wa kiwanda hiki uliwashinikiza watu kuendelea kufanya kazi katika jengo ambalo halikuwa salama.
Serikali ya Bangladeshi Yawafuatilia Wanablogu, Yawatuhumu Kuukashfu Uislam.
Kadri mapambano makali kati ya wanaharakati wa Kiislamu na serikali yanavyoendelea kusababisha migongano ya kidini nchini Bangladesh, Mamlaka ya Mawasiliano ya nchi hiyo imechukua hatua ya kuwanyamazisha wanablogu wanaoonekana wapinzani wa Uislamu na serikali. Asif mshindi wa tuzo ya mwanablogu bora amekuwa akilengwa na hatua hizo kwa siku za hivi karibuni.
Bangladeshi: Raia Wakutana Kudai Haki Itendeke
Kidogo kidogo, makutano ya Shahbag katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka yamefurika watu wenye lengo la kutaka haki kufuatia ukatili uliofanywa mnamo mwaka 1971 wakati wa harakati za vita vya kutafuta uhuru pamoja na kudai hukumu ya kifo kwa wahalifu wa vita.Drop by drop, the Shahbag intersection in Bangladesh's capital city Dhaka has become an ocean of people, demanding justice for the atrocities committed during the country's 1971 liberation war and death penalty for war criminals.
Bangladeshi: Msichana Mwingine Mzawa Abakwa na Kisha Kuuliwa.
Kwa mara nyingine msichana mzawa ameuawa nchini Bangladesh baada ya kubakwa kikatili. Mhanga huyo, Khomaching Marma (14) alikuwa mwanafunzi wa darasa la nane. Ubakaji huu wa kikatili uliosababisha mauaji kwa mara nyingine tena umeamsha hasira na ghadhabu nchini kote. Watumiaji wa mtandao pia wanapinga vikali vitendo hivyo.
Watoto wa Mitaani Bangladesh Wakabiliwa na Unyanyasaji
Jumla ya watoto wa mitaani nchini Bangladeshi wanakadiriwa kufikia 400,000. Karibu nusu ya idadi hiyo wanaishi katika Jiji la Dhaka. Asilimia kubwa ya watoto hao ni wasichana. Wasichana hao wa mitaani huishi katika mazingira yenye hatari nyingi hasa unyanyasaji na dhuluma nyingine.
Italia Yalaumiwa kwa Ukiukaji wa Haki za Wakimbizi wa Kiafrika
Februari 23, Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya huko Strasbourg ilikuja na hukumu ya kihistoria kwamba Italia imevujna Tamko la Ulaya la Haki za Binadamu kwa kuwazuia na kuwarudisha wakimbizi wa ki-Eritrea na Somalia kwenda Libya. Abdoulaye Bah anaripoti.
Video: Vijana duniani kote wajieleza kwa sekunde 60
mradi wa OneMinuteJr unawapa vijana......
Bangladeshi: Ku-twita na kublogu tetemeko la ardhi
Tetemeko la ardhi la wastani lilitikisa jiji la Dhaka siku ya tarehe 27 Julai mnamo muda wa saa 00:51 kwa saa za Bangladeshi (+6 GMT). Russell John anaripoti katika blogu yake: Nilikuwa nimelala kwenye kitanda changu huku nikongea kwa simu na rafiki yangu, na ghafla nikahisi kitanda kikitetemeka. Ndani ya...