I am a Tanzanian, professionally a science Teacher specifically for chemistry and Mathematics. I fluently speak Kiswahili. As a Swahili speaker, its my duty to inform swahili speakers around the Globe with news which are hardly found in other news media but only in Global Voices, “Sauti za Dunia, Ulimwengu unaongea, wasikiliza”.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima
Rajisi ya Usajili wa Watumiaji wa Simu za Mkononi Nchini Mexico Yazua Hofu Kuhusu Haki ya Faragha
"Uanzishwaji wa rajisi kam hii ulifanyika mwaka 2009, hata hivyo, kanzidata hii iliishia kuvujisha taarifa za watu na baadae kufikia uamuzi wa kuuzwa."
Serikali ya Angola Yafungia Kituo cha Runinga cha Kibrazili kwa Madai ya ‘Kukiuka Taratibu’
Serikali yatoa ufafanuzi wa kukisimamisha kufanya shughuli zake kituo cha runinga cha Record TV África kwa kile kinachoelezwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wake hakuwa "mzawa" wa Angola. Hata hivyo, kituo hiki kilishafanya mabadiliko ya Mkurugenzi Mtendaji na kumweka raia mzawa.
Watumiaji wa simu za mkononi wanajilinda vya kutosha dhidi ya ukiukwaji wa haki ya faragha?
Kwa makampuni ya teknolojia, taarifa binafsi za watu ni chanzo kikuu cha mapato yao. Hata hivyo, watumiaji wa makampuni haya wanakabiliwa na hatari kubwa ya usalama wa taarifa zao. Je, kuna njia muafaka ya kulinda haki yao ya faragha?
Jean-Jacques Muyembe-Tamfum: Mwanasayansi wa Congo Aliyegundua Tiba ya Ebola
Mwanasayansi huyu amegundua dawa ya kutibu ugonjwa wa Ebola. Je, jina lake litashika vichwa vya habari kwa mapana katika vyombo vya habari kama ilivyo kwa habari kuhusu ugonjwa wenyewe?
Wanaharakati wa Mazingira wa Bulgaria Wapata Ushindi Muhimu wa Mahakama Kufuatia Kampeni yao ya #SaidiaHifadhiyataifayaPirin
"Habari njema kwa @zazemiata + maelfu ya watu wanaandamana dhidi ya mpango wa uharibifu wa #Hifadhi ya Taifa ya Pirin nchini Bulgaria! #SaidiaPirin"
“Nilitamani Wajukuu wangu Wakulie kwenye Nyumba Ile”:Ushuhuda wa Mwanamke wa Syria mwenye Miaka 61 kutoka Zamalka
Nilitamani wajukuu wangu wakulie kwenye nyumba ile, na hivyo kuweza kuongozea uhai mpya nyumbani pale, kama walivyofanya mabubu zetu wa kila kizazi kilichopita.
Maandamano ya Nicaragua Yachochea Kufungwa kwa Vyombo vya Habari, Shambulizi la DDos na Mauaji ya Mwandishi wa Habari Angel Gahona
Ripoti ya Utetezi wa Raia wa mtandaoni inakuletea mkusanyiko wa changamoto, mafanikio na mwenendo wa matukio yanayojitokeza kuhusiana na haki za matumizi ya mtandao wa intaneti ulimwenguni kote.
Serikali ya Ufilipino Yapanga Kukifunga Kisiwa cha Kitalii cha Boracay na Kutishia Kuhamisha Maelfu ya Wakazi
"Malefu kwa maelfu ya watu wataathirika ikiwa kisiwa hiki kitafungwa moja kwa moja. Watu halisi, wanaopumua, siyo takwimu."
Msanii Duo wa Nepal Aweka Tumaini la Michoro ya Utupu Kuhamasisha Wanaume Kujipambanua Zaidi
“INi jambo jema ukijikubali, ni vizuri, wanaume wanaweza pia kulia, wanaweza pia kujijali"
Kipi Kinajiri Maekelawi? Simulizi ya Ukatili wa Kituo cha Kushikilia Watuhumiwa cha Ethiopia Kinachotarajiwa Kufungwa
"Imefahamika kwamba hofu ya wafungwa nchini Ethiopia, kitu ambacho kilishakaribia kufutika kwenye kumbukumbu za watu, kumbe ni nkumbukumbu iliyokaribu kabisa"