“Hatuwezi Kukandamiza Utu wa Wengine bila Kuukana utu Wetu Kwanza

Atnaf Berahane, Mahlet Fantahun, Zelalem Kiberet, Befeqadu Hailu, Natnael Feleke, Abel Wabela.

Wanablogu sita waliofungwa gerezani: Atnaf Berahane, Mahlet Fantahun, Zelalem Kiberet, Befeqadu Hailu, Natnael Feleke, Abel Wabela.

Mnamo mwezi wa Aprili, wanablogu tisa pamoja na waandishi wa habari walikamatwa nchini Ethiopia. Baadhi ya wanaume na wanawake hawa walikuwa wakifanya kazi na Zone9, blogu ya ushirika  liyokuwa inazungumzia masuala ya kijamii na ya kisiasa nchini Ethiopia ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uzingatiaji wa haki za binadamu na uwajibikaji wa serikali. Miongoni mwao, wanablogu wanne walikuwa ni waandishi wa Global Voices. Mwezi Julai, walihukumiwa chini ya sheria ya nchi ya kupambana na ugaidi. Tangu wakati huo, wameendelea kuwepo gerezani, huku shitaka lao likiwa linaahirishwa mara kwa mara.

Jumuia ya Global Voices, na hususani timu ya Ukanda wa chini wa Jangwa la Sahara, umekuwa ukifanya juhudi za hali na mali kwa muda wa kipindi cha miezi 12 iliyopita ili ulimwengu ufahamu kesi yao pamoja na kusherehekea machango wao katika jukwaa la mtandaoni. Katika wiki zinazofuata, tunategemea kumzungumzia kila mwanablogu kwa kutumia kipande mahususi cha makala, sanaa, ushairi au video. Katika makala hii ya awali, Mwandishi wa Nigeria na mshairi, Nwachukwu Egbunike azungumza kwa niaba yetu kwa kutumia mchanganyiko wa nathari na ushairi.

Hatuwezi Kukandamiza Utu wa Wengine bila Kuukana utu Wetu Kwanza. Igbo, mara zote wakiwa wahalisia, wazungumzia hili kwa ufasaha kabisa kwenye msemo wao- “Onye ji onye n'ani, ji onwe ya” – “Yeyote atakaye kumzamisha mwingine kwenye tope lazima na yeye awe kwenye tope hilo ili aweze kumzamisha mwingine”

Chinua Achebe

Wanablogu hawa tisa wa Ethiopia bila sababu inayoeleweka waliwekwa kizuizini gerezani na wale wanaomanika kupewa jukumu na wengi la kuliongoza taifa la Ethiopia. Matazamia yetu katika wiki zinazofuata ni kutoa simulizi zinazowahusu mmoja baada ya mwingine.

Katika jina kuna nini? Ni kitu cha muhimu sana kwa utu wa mtu. Mtazamo wa jumla wa Mwafrika ni kuwa, majina kamwe hayawezi kufutwa. Lakini taifa la kiharamia linataka kufanya hivyo kirahisi tu.

Kosa la Wanablogu wa Zone9′ ati lilikuwa ni kuthubutu kuonesha dhamira yao ya kuupigania “Ubuntu”. Waliihamasisha jamii yao kuachana na dhana ya ubinafsi. Jukumu lao kubwa lilikuwa ni kuondoa na kuangamiaza kabisa vikwazo vikubwa vya kauli mbiu yao ya gereza la “Zone Nine” la Ethiopia. Uhuru upo katika hali tete, uhuru wa kujieleza haupo. Ukimya wa hofu unamea.

Wakitumia mtandao wa intaneti, wanaume na wanawake hawa walipanua wigo wa uhuru. Lakini, kwa bahati mbaya, kama zawadi yao, walijikuta kwenye uonevu usiomithilika kwa kushitakiwa kwa makosa ya ugaidi ya kusingiziwa. Hadi wakati huu, wanablogu hawa bado wapo gerezani.

Mradi wa utetezi wa Global Voices unalenga kuendelea kuyaweka majina haya hai ikiwa ni pamoja na kutoa simulizi zinazowahusu ili kila mmoja awafahamu. Tunalenga kuzuia mfumo wa kurahisisha utu wao kwa kuwahesabu kama namba tu au kama watu waliokosa tumaini la kuishi. Wanayo majina, simulizi, haiba, tabia zao za kipekee, mapungufu.

Majina, simulizi
Zoned into Gaul
Tisa siyo kutokuwepo
Kulindwa siyo kunyamazishwa
Kukandamizwa siyo kutokomezwa.

Majina yao na hahari zao zitasimuliwa hapa. Kwa namna hii, tunataka kamwe tusiwasahau na kuelendelea kupaza sauti zao kwa uiamara, hadi pale watakapoachiwa huru.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.