Baada ya Miaka 33, Cuba Haipo Kwenye Orodha ya Marekani ya Nchi Zinazofadhili Ugaidi

Plaza de la Revolución. Photo taken from Mark Scott Johnson licensed by CC BY 2.0

jengo la Plaza de la Revolución. Picha imechukuliwa kutoka kwa Mark Scott Johnson ina leseni ya CC 2.0

Marekani imeiondoa Cuba kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi siku ya Ijumaa, hadhi zinazopewa nchi, kwa mujibu wa Marekani, ambazo zina kawaida ya kuwezesha vitendo vya ngazi ya kimataifa vilivyopangwa, na vyenye lengo la kupambana kisiasa na raia wasio na silaha.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nchi ya Marekani:

Mnamo Desemba 2014, Rais alimwagiza Waziri wa Nchi kupitia upya haraka hadhi ya Cuba kama Nchi Inayofadhili Ugaidi, na kutoa taarifa kwake ndani ya miezi sita kuhusu ufadhili wa Cuba kwa vitendo vya kimataifa vya ugaidi. Mnamo Aprili 8, 2015, Waziri wa Nchi alikamisha kazi hiyo na kumshauri Rais kwamba Cuba haina sifa tena ya kuwa Nchi Zinazofadhili Ugaidi.

Hivyo, mnamo Aprili 14, Rais alitoa hoja kwenye Bunge kuomba taarifa inayoonesha nia ya Utawala wake kuiondoa Cuba kwenye orodha ya Nchi Zinazofadhili Ugaidi, ikiwa ni pamoja na uthibitisho kwamba Cuba haijatoa ushirikiano wowote kuwezesha Ugaidi wa kimataifa katika kipindi cha miezi sita; na kwamba Cuba imetoa uhakikisho kwamba haitawezesha vitendo vya ugaidi wa kimataifa katika siku zijazo. Kipindi cha siku 45 ilizopewa Bunge kutafakari taarifa hiyo kimekwisha, na Waziri wa Nchi ametoa uamuzi wa mwisho wa kuiondoa Cuba kwenye orodha ya Nchi Zinazofadhili Ugaidi kuanzia leo, Mei 29, 2015.

Kuondolewa kwa Cuba kwenye orodha ya Nchi Zinazofadhili Ugaidi kunaonesha tathimini yetu kwamba Cuba ina sifa za kuondolewa kwenye orodha hiyo. Wakati Marekani ina wasiwasi na haikubaliani na sera na mienendo mingi ya Cuba, bado inaamini kwamba hazina uhusiano na kufadhili vitendo vya ugaidi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.