Vito na Sarafu za Kale za Syria Zapigwa Mnada Kwenye Mtandao wa Facebook

Looted ancient coins from Syria on sale on Facebook. Photograph shared by @zaidbenjamin on Twitter

Sarafu za kale kutoka Syria zikiwa kwenye mnada kwenye mtandao wa Facebook. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @zaidbenjamin

Vito na sarafu za Syria zimewekwa kwenye mtandao wa Facebook kwa ajili ya mnada.

Habari hizo ziliibuliwa na mwandishi anayeishi Washington DC, Zaid Benjamin, aliyeweka picha kadhaa kwenye mtandao wa Facebook zikionesha sarafu na vito vya zamani vya Syria zikiuzwa nchini Uturuki.

Ukurasa mwingine wa Facebook ukipiga mnada sarafu za Syria. Zinapatikana Uturuki?

Kutoka Misri, Sima Diab anasema:

Uko sokoni kutafuta kununua au kuuza sarafu za Syria? Usitafute kwingine zaidi ya kwenye mtandao wa Facebook

Inaweza kueleweka kwa nini, ukurasa wa mtandao wa Facebook unamwuunganisha Sima haupatikani tena.

A screen shot of a page which used to allegedly sell Syrian antiques on Facebook is no longer available

A screen shot of a page which used to allegedly sell Syrian antiques on Facebook is no longer available

Picha ya ukurasa huo unaodaiwa kuuza sarafu za Kisyria kwenye mtandao wa Facebook ambao kwa sasa haupatikani

SOMA PIA:

Wafanyabiashara wa magendo wanapata dola milioni 1 kwa sarafu hizo za kale zilizoibwa nchini Syria.

Kwa mujibu wa taarifa za habari, wanamgambo wa ISIS wanavuna mamilioni kwa biashara hiyo ya magendo, wakiuza safaru na vito hivyo vilivyoibwa kwenye makumbusho yaliyo Magharibi na karibu na Ghuba kupitia mtandao mpana wa wafanya biashara ya magendo na madalali.

Syrian antiques on sale on Facebook. Photograph shared by @zaidbenjamin on Twitter

Sarafu na vito vya Syria vikiwa sokoni kwenye mtandao wa Facebook.Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @zaidbenjamin

Gazeri la The Daily Mail linadai sarafu hizo zimetengenezwa kwenye miaka isiyopungua 10,000, kutoka Ragga, mji mkuu uliotangazwa na ISIS nchini Syria, kila moja ikiuzwa kwa zaidi ya dola milioni na zimeibwa kutoka Syria na Iraq kupitia Uturuki na Lebanon.

Syrian gold coins on sale on a Facebook page. Photograph shared on Twitter by @zaidbenjamin

Sarafu za Syria zilizotengenezwa kwa dhahabu zikiwa mnadani kwenye mtandao wa Facebook. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @zaidbenjamin

Kundi la ISIS, ambalo ni tawi la Al Qaeda limedhibiti sehemu kubwa ya Syria na Iraq, na kusababisha taharuki kubwa na kusababisha uharibifu mkubwa ndani ya kipindi cha miezi michache. Maeneo yaliyodhibitiwa na kikundi hicho kinachosisitiza kutokomeza maeneo yote ya “tetesi” na “kidini” ni pamoja na lile linaloitwa Cradle of Civilisation, eneo lenye historia kubwa tangu nyakati za zamani.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lina ukurasa maalum kwa ajili ya Kulinda Urithi wa Kiutamaduni wa Syria kwa lengo la kufuatilia uharibifu uliosababishwa na mapigano nchini humo, yanayokaribia miaka minne sasa, na athari zake kwenye historia yanchi hiyo.

Kwa mujibu wa UNESCO:

Uchimbaji na uvunjaji haramu kwa pamoja vimeongezeka tangu kuanza kwa vita nchini Syria. Matukio haya yameharibu maeneo mengi ya kihistoria na makumbusho, na utajiri mkubwa wa kiutamaduni nchini humo umetoweka nchini na kuishia kwenye minada haramu na/au kuhifadhiwa na watu binafsi.

Maeneo mengi ya kihistoria nchini Syria yamekuwa yakilengwa katika mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo ambao mara nyingi huwa na silaha. Mali za kihistoria zinazoibwa zina umuhimu mkubwa wa kihistoria na kuwaletea faida kubwa wafanyabiashara hao wa kimagendo nchini humo na kimataifa. Maeneo hayo yaliyo karibu na mipaka, kwa ujumla, yamekuwa yakilengwa na wahalifu hao wanaotumia fursa ya kuwa karibu na maeneo hayo kuisafirisha utajiri huo nje ya nchi kwa urahisi kwa kutumia njia haramu.

Kuhusu hali ya makumbusho, ukurasa unaozungumzia tathmini ya uharibifu unabainisha:

Uharibufu mkubwa kwenye makubusho hayo nchini Syria umetokea kwenye eneo la kaskazini magharibi mwanchi hiyo, ambapo kumekuwa na matukio ya kuibwa kwa utajiri mkubwa wa kiutamaduni, na kazi nyingi za sanaa hazijulikani ziliko. Idadi kubwa ya majengo ya makumbusho yameharibiwa vibaya ikiwa ni matokeo ya mapigano yanayoendelea kwa kutumia silaha nzito.


UNAWEZA KUSOMA:

ISIS inajaribu kufuta historia nchini Iraq na Syria

Watu wengi wamekasirishwa na namna baadhi ya watu wanavyoguswa na uharibifu wa historia na kuhamisha vito vya thamani badala ya kusikitishwa na kupotea kwa maisha ya sasa kunakotokana na mateso yanayoendelea nchini Syria.

Liam Stack anasema:

Katika majuma ya hivi karibuni maafisa wa Syria wamehamisha vito vya thamani kutoka kwenye makumbusho, lakini hawakuwaonya wakazi kuondoka pia

Na Khaled Diab anaonya:

Hii tabia ya Kimagharibi inayoathiri maisha ya watu ambayo tayari yameshaharibika nchini Syria inaweza kuwafanya ISIS kufanya propaganda zaidi, anasema Khaled Diab

Unaweza kusoma habari zetu nyingine hapa Global Voices:


ISIS Yaharibu sanamu zenye umri wa miaka 3,000 kwenye makumbusho ya Mosul, Iraq


ISIS Yachoma Maktaba ya Mosul nchini Iraq, Yaharibu Maelfu ya Miswada na Vitabu vyenye thamani

Video: ISIS Yaharibu Msikiti wa Nabii Yona huko Mosul, Iraq

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.