Raia wa Masedonia Watumia Sheria ya Uhuru wa Habari Kupinga Sheria Mpya ya Wafanyakazi

Image of protesters from the first march of part-time and freelance workers in Macedonia, December 2014. Photo courtesy of Akademik.mk, used with permission.

Picha ya maandamano yaliyohusu kazi za mikataba ya muda na wale walio na ajira zaidi ya moja nchini Makedonia, tarehe 24, Desemba. Picha kwa idhini ya Akademik.mk, imetumika kwa ruhusa.

Takribani, watu 1,000 nchini Macedonia wameshatia saini ya kukubali kushiriki kwa mara nyingine kwenye maandamano ya kuwatetea wafanyakazi walio na mikataba ya muda pamoja na wale walioajiriwa na mwajiri zaidi ya mmoja ,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 6 Februari. Katika maandamano ya awali, yaliyofanyika Desemba 2014, maelfu ya watu walijitokeza kwenye mitaa ya Skopje wakipinga ongezeko la kodi pamoja na ada inayotozwa kwa mujibu wa taratibu mpya za serikali zilizoanza kutumika rasmi tarehe 1 Januari, 2015.

Kutokana na sintofahamu iliyopo katika sheria hii mpya na kukosekana kwa mawasiliano mazuri miongoni mwa vyombo husika vya serikali katika kutekeleza sheria hii, malipo ya ada ya kufanya kazi isiyo ya mkataba wa kudumu pamoja na baadhi ya wafanyakazi walio na mwajiri zaidi ya mmoja walizuiwa katika tarehe za mwisho za mwezi Januari. META.mk ambalo ni wakala wa habari, siku za hivi karibuni lilitaarifu kuwa:

Katika mwezi mrefu wa mwaka, wafanyakazi walio na mwajiri zaidi ya mmoja na ambao hutoa ada zaidi ya denari 9,590 (sawa na dola za kimarekani 178) hawatapata hawatalipwa. Wakala wa hati miliki “Berin” walisema kuwa walipokea taarifa kutoka Mfuko wa Pensheni na Bima ya Ulemavu (PIOM) ikiwataka kutokutoa ada zaidi ya denari 9,590 mpaka pale taarifa ya namna ya ukokotoaji unavyofanyika itakapositishwa kuwekwa kwenye tovuti. Kama ilivyoelezwa katika taarifa hiyo, sababu kubwa ya kushindikana kutekelezwa kwa sheria hii mpya ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri kati ya Wizara ya Kazi na Sera ya Kijamii, PIOM na PRO, sheria inayowataka wafanyakazi walioajiriwa na mwajiri zaidi ya mmoja kutoa mchango wa pensheni pamoja na bima ya ulemavu.

Kinachopelekea kuratibiwa kwa maandamano haya mapya ikilinganishwa na maandamano mengine ni matumizi ya mbinu mpya: washiriki wanajiandaa kuiuliza Wizara ya kazi na Sera ya jamii kuhusiana na utata wa kisheria kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya Uhuru wa Kupata Taarifa. Kwa kutumia kigezo kuwa maombi ya kupata taarifa ndio sababu kubwa ya kuchelewesha malipo, waandamanaji wana lengo la kuonesha mapungufu ya utaratibu huu wa wizara ambao wengi wanaamini kuwa urasimu huu ni visingizio na kanuni zisizo na maana yoyote.

Ајде хонорарци да одиме во МТСП и да си ги побараме одговорите што ни ги должат!
Цел јануари многумина од нас не добија хонорар, АЈДЕ ДА ПРАШАМЕ!
На некои им прекина авторскиот договор АЈДЕ ДА ПРАШАМЕ!
Не не прашуваа кога решаваа во лето да сменат 5 закони, ајде сега НИЕ да ги ПРАШАМЕ!
Петок, 6 февруари 11.00часот. Министерство за труд и социјална политика.
Имате формулари.
Имаме ПРАВО на одговори!

ДЕТАЛИ ЗА НАСТАНОТ
Секој хонорарец поднесува барање за информација од јавен карактер до министерството по што им се придружува на останатите кои стојат пред министерството. Поднесувањето барања се планира да трае два часа.
Урнекот на барањето за информации од јавен карактер можете да го преземете од коментарите. Прашања можете сами да поставите или можете да преземете некое прашање од листата што исто така ја имате како коментар.

Jitokezeni wafanyakazi mlio na mwajiri zaidi ya mmoja, twendeni Wizara ya Kazi na Sera za Jamii ili tupate majibu ya maswali yetu.
Wengi wetu hatukulipwa mwezi Januari, watuambie kwa nini hawakutulipa!
Baadhi yetu mikataba yetu ilisitishwa, tuwaulize kwa nini waliisitisha!
Hawakutushirikisha wakati walipoamua kubadilisha sheria zote tano wakati wa kipindi cha majira ya joto, ni muda muafaka wa kuwauliza!
Ijumaa, tarehe 6 Februari majira ya 11:00 p.m. Wizara ya Kazi na Sera ya Jamii.
Tumia fomu zilizoambatanishwa.
Tuna haki ya kupata majibu.

UNDANI WA TUKIO
Kila mfanyakazi aliyeajiriwa na mwajiri zaidi ya mmoja, atawasilisha wizarani maombi ya Uhuru wa Kupata Taarifa (FOI) na kisha kujiunga na wengine watakaokuwa wamekusanyika mbele ya jengo la wizara. Mchakato wa uwasilishaji wa maombi utachukua takribani masaa mawili.
Fomu ya maombi imeambatanishwa kwenye maoni ya tukio hili [katika lugha za kimacedonia na Kialbania]. Unaweza kujichagulia maswali au kunakili baadhi kutoka kwenye orodha iliyoambatanishwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya Macedonia ya Uhuru wa Kupata Taarifa ya Kanuni ya Umma, mamlaka za serikali zinalazimika kutolea majibu ya maombi ya Uhuru wa Kupata Taarifa (FOI) ndani ya siku 30. Kwa wale waliowasilisha maombi kwa kutamka wanapaswa kupokea majibu ndani ya siku tano. Taariza zaidi kuhusu sheria ya Uhuru wa Kupata Taarifa inapatikana katika tovuti ya Tume ya kulinda Haki ya Kupata Taarifa za Umma na Jukwaa la umoja wa upashanaji habari za Kiraia “Haki ya Kujua.”  Mamia kadhaa, pengine na zaidi ya maombi ya Uhuru wa Kupata Taarifa (FOI) yanategemewa kuwasilishwa kwenye serikali ya Macedonia kuptia maandamano haya. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.