Baada ya Miaka 29 Madarakani, Rais wa Uganda Museveni Hana Mpango wa Kung'atuka

Uganda's president Yoweri Museveni. Photo released under Creative Commons by Russell Watkins/Department for International Development UK).

Rais wa Uganda Yoweri Museveni. Picha imetolewa chini ya leseni ya Creative Commons na Russell Watkins/Idara ya Maendeleo ya Kimataifa Uingereza).

Asilimia sabini ya wa-Ganda wana umri chini ya miaka 29. Ndio kusema tangu wazaliwe wamemwona rais mmoja tu. Januari 26, 2015, Rais wa Uganda Yoweri Museveni na chama chake cha National Resistance Movement (NRM) walisherehekea miaka 29 madarakani. Siku hiyo imetengwa kuwa siku ya ukombozi kuadhimisha siku ambayo chama cha NRM kilitwaa madaraka baada ya mapambano ya miaka mitano msituni kuiondoa serikali kandamizi madarakani.

Rais Museveni tayari anatafuta kuchaguliwa kwa kipindi cha sita cha Urais. Mabango yaliyotengenezwa na chama chake kuunga mkono nia yake ya kuendelea kuitawala nchi hiyo yameenea kwenye jiji la Kampala, makao makuu ya nchi hiyo. Ili adhima yake hiyo iungwe mkono na wananchi, Museveni amekuwa akionekana hadharani akikabidhi bahasha za kaki zenye pesa kwa raia maskini awapo kwenye mikusanyiko ya watu. Amekuwa na mazoea hayo hata siku za nyuma. Hata hivyp, amekosolewa na wananchi kwa kuifanya hazina ya nchi hiyo kama Mashine binafsi ya Kutoa Fedha (ATM).

Kwa wa-Ganda wengi, sherehe za siku ya ukombozi ulikuwa ni wakati wa kutathimini utawala wa NRM na ahadi zake ambazo chama hicho kilizitoa kilipokuwa kinaingia madarakani.

George Ayittey, prefesa wa uchumi wa Ghana na rais wa Mfuko wa Uhuru wa Afrika (FAF) jijini Washington, DC, aliukumbusha ulimwengu kile ambacho Museveni alikisema mwaka 1986 alipokuwa rais wa Uganda:

Mwaka 1986, Rais Museveni alituambia, “Hakuna Rais wa Afrika anapaswa kubaki madarakani kwa zaidi ya miaka kumi.” Yeye mwenyewe bado yuko madarakani kwa miaka 29 baadae

Mwandishi wa Uganda, Benjamin Rukwenge amechoshwa na watumiaji wa mtandao wa Twita wanaolalamika badala ya kuchukua hatua kukabili hali hiyo:

Haijalishi hisia zako zikoje, huwezi kupambana na historia. NRM ina mema yake kwa miaka 29. Msilalamike, rekebisheni yale mnayoona ni makosa

Wakati Edgar Mwine, mhitimu wa uchumi asiye na ajira, alimnukuu mwanasheria, mchambuzi wa sera na mjasiria mali wa kijamii Godber Tumushabe:

“Ni kutukana akili za wa-Ganda kusema kwamba miaka 29 ya utawala wa Museveni ni mafanikio

Museveni alisema kwenye hotuba yake kwamba kamwe hataachia madaraka kwa upinzani, anaouita mbwa mwitu, kwa sababu anaungwa mkono na jeshi. Akitoa maoni kuhusu hotuba hiyo kwenye tovuti ya Daily Monitor website, “Kabindist” aliandika:

Kwa hiyo ni rasmi. Hakuna demokrasia nchini Uganda. Museveni na Jeshi lake ndio kila kitu. Kw ahiyo, miaka yote hii aliposema alihitaji muda zaidi kulifanya jeshi liwe la kisasa, alimaanisha kulipumbaza akili lifanye anachotaka yeye. Ukomo wa madaraka, ukomo wa umri na yote hayo yapo lakini ni kama mchezo tu kwa Kaguta. Anaamini siku yake haitafika. Akiwa na mbwa mwitu wkae wa NRM nchi tayari imechanwa vipande vipande na kama mbwa mwitu walafi hatakata tamaa. Anamdanganya nani?

Akitoa maoni kwenye makala hiyo hiyo, Bishanga Paul alimuonya Museveni:

Gadafi alikuwa na Jeshi imara na aliungwa mkono na watu ambao baadae walichoshwa na kumfukuza jijini kuhakikisha hatawali nchi hiyo milele.

Na ili kuihusisha hoja hiyo na hali ya mambo nchini, Daily Monitor lilionesha kwa mchoro:

KATUNI: Leo tunatimiza miaka 29 tangu NRM itwae madaraka

Akimkosoa Museveni, Charles Onyango Obbo, mhariri wa Mail & Guardian Africa, alimfananisha Museveni na kiongozi wa waasi wa Lords Resistance Army Joseph Kony:

Kwa kuanzia, Kony na Museveni ni viongozi waliotawala kwa muda mrefu baada ya mwaka 1986 taasisi zao. Kwa kuhesabu kuanzia alipochukua madaraka, Museveni amekuwa kiongozi wa NRM, rais na amiri jeshi mkuu kwa miaka 29. Kony alikuwa kiongozi rasmi wa waasi wa LRA mwaka 1988, baada ya kuwaunganisha masalia ya chama kilichokufa cha Alice Lakwena kiitwacho Holy Spirit Movement.
Kony, kwa hiyo, ameiongoza LRA kwa miaka 26, kiongozi pekee wa waasi katika kipindi cha Museveni anayemkaribia Chifu mwenyewe (Museveni). Linapokuja suala la kudumu jeshini na kisiasa, kwa hiyo, Museveni na Kony wako kwenye kundi la aina yake. Ninadhani Museveni atadumu zaidi ya Kony, lakini wakati mwingine mambo yasiyo ya kawaida hutokea kwenye maisha haya yasiyotabirika kwa hiyo sitajiapiza kwa hilo.

Mwezi Desemba mwaka jana, jarida laDaily Monitor lilimnukuu Museveni akisema kwamba wa-Ganda hawataki aondoke madarakani. Aliwabebesha lawama wa-Ganda kwa kuendelea kumchagua na hivyo kumfanya abaki madarakani.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.