Waandamanaji Wavamia Ukumbi wa Sinema na Kusema ‘Hunger Games’ Inaendelea Nchini Thailand

The #DistrictThai demonstration in London, via the District Thai Facebook page

Maandamano ya #DistrictThai jijini London, Picha kupitia ukurasa wa Facebook wa District Thai.

Kikundi cha raia wa Thailand kilikusanyika nje ya Ukumbi wa Sinema wa Odeon uliopo kwenye viwanja vya Leicester jijini London siku ya Jumatatu, Novemba 10, wakati wa kuonesha kwa mara ya kwanza kwa filamu maarufu ya “The Hunger Games: Mockingjay Sehemu ya 1,” kama jitihada za kufanya dunia iangazie uwepo wa hali inayotishia demokrasia, uhuru wa kujieleza, na utawala wa sheria nchini Thailand. 

Filamu hiyo ina umuhimu mkubwa kwa wa-Thai wengi. Kwa hakika, wapinzani wa mapinduzi ya kijeshi hivi majuzi nchini Thailand, yaliyoiong'oa madarakani serikali iliyokuwa imechaguliwa kidemokrasia iliyokuwa ikiongozwa na  Yingluck Shinawatra, na waliweza kuiga  alama ya vidole maarufu ya vitatu inayoonekana kwenye filamu hiyo. Alama hiyo imekuwa maarufu sana kiasi kwamba jeshi la nchi hiyo limeipiga marufuku, ikiwa ni pamoja na upinzani mwingineo wa kisiasa. Mamia ya wa-Thai hivi karibuni yalitumia salamu hiyo kwenye mazishi ya Naibu spika wa zamani Apiwan Wiriyachai, kwa kumsalimia Yingluck Shinawatra kwa ishara hiyo, alipowasili kutoa heshima zake za mwisho. 

Katika kusanyiko hilo juma hili jijini London, wengi wa wanaharakati hao walilazimika kuvaa magamba ya kuficha nyuso zao, kwa hofu ya kuwasababishia matatizo ndugu na jamaa zao walioko nchini Thailand. 

Wanaharakati hao walifungua  ukurasa wa Facebook na akaunti ya Twita katika kuratibu jitihada zao, kwa kutumia alama ishara #DistrictThai. “District” inaaminisha mkakati ulioitwa “The Hunger Games,” ambapo udikteta wa kiimla unaoanzia mahali fulani hutawala  maeneo mengine ya kijiografia yanayoitwa wilaya (“districts”). Maeneo haya yamefukarishwa na kutumikishwa na “Makao Makuu.”

Anuani hizo za mitandao ya kijamii zinaendeshwa kwa lugha za ki-Thai na Kiingereza, kwa ajili ya hadhira ya nyumbani huko Thailand na duniani kote. Ukurasa wa Facebook wa kundi hilo ulikuwa maarufu, ukivutia watu 1,000 kuupenda ndani ya mwisho wa juma moja pekee. Ujumbe wa kwanza ulionekana Ijumaa, Novemba 7:

districtthai messageWafanyakazi wa Ukumbi wa Sinema wa Odeon jijini London, walipogundua maandamano ya #DistrictThai, waka twiti:

Maandamano ya #DistrictThai yako jijini na yanaonekana poa. Nawapa alama A kwa jitihada zao!

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.