Wanablogu wa Brazili Wadai Mgombea Urais Anawadhibiti Wakosoaji wake Kwenye Mtandao wa YouTube

Aécio Neves has filed suit against Twitter demanding it discloses information on 66 users; now bloggers claim he's using fake accounst to deal with negative Youtube videos. Image by flickr official Aécio Neves account. CC BY 2.0

Aécio Neves amefungua mashtaka dhidi ya mtandao wa Twita kudai taarifa za watumiaji 66 ziwekwe wazi; hivi sasa wanablogu wanadai anatumia anuani bandia kujaribu kupambana na wapinzani wake kwenye mtandao wa YouTube. Picha na anuani rasmi ya Flickr ya Aécio Neves . CC BY 2.0

Siku kumi zilizopita, filamu ya maisha halisi mtandaoni [dokumentari] inayoitwa “Helicoca – The 60 Million Reais Helicopter” iliondolewa kwenye mtandao wa YouTube  kufutia hatua ya mtu anayeitwa “Jorge Scalvini” aliyedai kuibiwa haki miliki. Watumiaji wa mitandao walishuku kuwa kuondolewa kwa video hiyo kulipangwa na kutekelezwa na mgombea urais Aécio Neves.

Filamu hiyo inachunguza tukio la kukamatwa kwa madawa ya kulevya na Polisi, ambalo ni tukio kubwa kuwahi kutokea katika historia ya Brazili, ambapo  kiasi cha nusu tani za dawa za kulevya kiligundulika kwenye helkopta inayomilikiwa na familia tajiri na yenye nguvu ya Perrella. Wanafamilia wa Perella ndio washirika wakuu wa kisiasa wa Aécio Neves, ambaye ndiye mgombea wa urais kupitia chama cha Demokrasia ya Kijamii Brazili (PSDB) na gavana wa zamani wa jimbo la Minas Gerais, linalopakana na São Paulo na Rio de Janeiro. Rubani na wafanyakazi waliohusika na mpango huo walishtakiwa kwa makosa ya jinai, na polisi [inasemekana] kufanya jitihada za kuiepusha familia ya Perrella na sakata hilo. Kukosekana kwa taarifa za kuhusika kwa familia ya Perella kwenye tukio hilo kulishangaza wengi na kuwafanya waandishi wa habari kuamua kulifuatilia suala hilo kwa kina.

Diário do Centro do Mundo ni filamu iliyoandaliwa na kufadhiliwa kwa michango ya watu wengi imeratibiwa na tovuti huru ya habari yenye mrengo wa kushoto na kuongozwa na mwongozaji wa filamu  Joaquim de Carvalho, mwandishi wa habari aliyewahi kufanya kazi na mashirika makubwa ya habari nchini Brazil kama vile O Estado de S. Paulo na TV Globo. 

Wanaohusika na filamu ya Diário do Centro do Mundo wanasema kwamba  anuani ya Scalvini, ambayo iliyoomba uongozi wa YouTUbe kuifuta Helicoca, ilikuwa bandia:

Nós procuramos saber quem é Scalvini. Seu email é zerobeta000@gmail.com. Enviamos uma mensagem nesse endereço. Não obtivemos resposta. Tudo indica que se trata de um perfil fake. Scalvini possui uma conta no Twitter, aberta em 2012, sem nenhuma postagem. Seu perfil no Facebook é vazio, com curtidas em páginas como as da “TV Revolta”, “Mensaleiros na Cadeia” e “Chega de Corrupção”. Há também uma conta no YouTube com seu nome. A última movimentação foi há três meses.

Tulijaribu kuchunguza kujua Scalvini ni nani. Barua pepe yake ni zerobeta000@gmail.com. Tulituma ujumbe kwa anuani yake hiyo na hatukupata majibu. Inaonekana ni anuani bandia. Scalvini ana anuani ya Twita , aliyoifungua mwaka 2012, na haina twiti yoyote. Wasifu wake kwenye Facebook hauna kitu, ukiwa na mashabiki wachache kwenye kurasa kama “TV Revolta”, “Mensaleiros na TV” e “Chega de Corrupção”. Na pia ana anuani kwenye mtandao wa YouTube kwa jina lake. Aliingia mara ya mwisho miezi mitatu iliyopita.

Ili kuepuka mashitaka ya kuingilia haki miliko, ni kawaida kwa Google (mmiliki wa YouTube) kuondoa video zinazodaiwa kuingilia haki miliki. Ni lazima mtengenezaji wa video, na sio mlalamikaji, kuthibitisha kwamba ana haki ya kuweka video hiyo. Diário do Centro do Mundo imekata rufaa kwa Google na imejulishwa kwamba itegemee kupata majibu rasmi ndani ya kipindi cha siku 10.

Wakati huo huo, mwandishi wa habari Ana Paula Freitas alichapisha kwenye mtandao wa Facebook  kwamba alikutana na tukio jingine la video kuondolewa kwenye YouTube , pia kwa madai ya haki miliki yaliyofanywa na mtu anayeitwa “George Scalvini”. Video hiyo ni maarufu, yenye vichekesho vyenye jina “Nataka kuwaambia rafiki zangu watakaompigia kura Aécio Neves” na inamwonesha mwanamke akiwa kwenye sherehe akipiga kelele kwa rafiki yake, anayeonekana kalewa, “Siwezi kukusaidia, samahani!”

Freitas aliandika:

O vídeo, como vocês podem ver, foi tirado do ar. Um tal de GEORGE SCALVINI requisitou direitos autorais. Desnecessário apontar a semelhança entre os nomes. Aparentemente, o jurídico do Aécio tem uma equipe especializada em tirar do ar não só os vídeos que contém acusações que possam prejudicá-lo politicamente, mas também brincadeiras como essa, que dentre o hall enorme de exemplos de humor ativista, é uma das mais bem-humoradas e inofensivas.

Video, kama unavyoona, iliondolewa. Jamaa anayejiita George Scalvini alidai kuwa na haki miliki ya video hiyo. Haina haja ya kutoa maoni juu ya kufanana kwa majina hayo mawili. Ni wazi, kampeni ya Aécio ina timu ambayo si tu imebobea kwenye kuondoa video zenye tuhuma zinazoweza kuathiri harakati zake, lakini pia kudhibiti vichekesho vidogo kama hivi, ambavyo katika harakati huwa havina athari kubwa.

Ingawa filamu hiyo ina vipande vya habari za Neves zilizochukuliwa kutoka kwenye vituo vya runinga vya habari, vinavyoweza kuyapa nguvu madai ya kukiukwa kwa haki miliki, filamu hizo hazina maudhui ya namna hiyo. Kinachowapa wasiwasi watumiaji wa mtandao wanaofuatilia habari hiyo ni kwamba video hizo zililalamikiwa haki miliki na mtu mmoja— ambaye anaweza kuwa si mtu halisi hata hivyo. Kilichowazi kinachoweza kuunganisha video hizo mbili ni kutajwa kwa jina la Aécio Neves.

Hofu hiyo imekuwa kubwa kufuatia majaribio ya zamani aliyoyafanya Neves kuwanyamazisha wapinzani wa utawala wake kwenye mitandao ya kijamii.

Mwishoni mwa Agosti, Neves alifungua mashitaka dhidi ya Twita baada ya kampuni hiyo kukataa kutoa taarifa za anuani za utambulisho (IP) za watumiaji wapatao 66. Gavana huyo wa zamani alidai anuani hizo za twita ni bandia zinazoendeshwa na kundi la watu wenye lengo la kusambaza uongo na upinzani dhidi yake na kampeni zake. Tamko rasmi la shitaka hilo linaweza kuonekana hapa.

Jarida la Magazine Revista Fórum liliwahoji wamiliki wa anuani kadhaa kati ya zile 66 zilizotajwa kwenye shitaka hilo. Mmoja wao ni mchambuzi maarufu wa filamu Pablo Villaça, mwanzilishi wa Cinema em Cena, tovuti ya filamu ya muda mrefu nchini Brazil. Villaça ametangaza hadharani kumwuunga mkono mpinzani wa Neves, ambaye ni rais wa sasa Dilma Rousseff. Akihojiwa na jarida la Revista Fórum kuhusu madai hayo alisema: 

Acho ótimo, cabe a ele provar que isso existe. Eu milito politicamente desde os 18 anos. Minha mãe combateu a ditadura, minha tia foi presa e torturada. E ainda insinua que sou pago para militar.

Nadhani ni suala zuri, sasa athibitishe kwamba upo [mtandao wa unaolipwa kumtengenezea shutma]. Nimekuwa mwanaharakati wa siasa tangu nikiwa na umri wa miaka 18. Mama yangu alipambana na udikteta, shangazi yangu alikwenda jela na kuteswa. Sasa huyu bwana anajaribu kufanya nionekane nalipwa ili kuwa mwanaharakati.

Tukio jingine la ajabu ni lile la filamu ya 2008 “Kuzuiliwa Brazil,” iliyotayarishwa na mtengeneza filamu Daniel Florêncio kwa ajili ya kituo cha runinga cha Current TV. Florêncio, anayetoka jimbo la Minas Gerais, anachunguza uhusiano wa serikali ya jimbo lake na vyombo vya habari. Miezi michache baada ya kutoka kwa filamu hiyo nchini Uingereza na Marekani, filamu hiyo ilifungiwa na kituo hicho cha Current TV. Katika amakala iliyoandikwa kwa ajili ya jarida la Observatório da Imprensa, Florêncio alieleza kile kilichotokea :

Na semana anterior, os executivos seniors do canal [Current TV] nos EUA receberam cartas com severas considerações e críticas sérias em relação ao filme. As cartas foram enviadas pelo PSDB de Minas Gerais. O PSDB afirmava que meu filme tinha caráter político-partidário, que não representava a realidade no estado e questionava minha conduta ética na produção do filme.

Katika majuma yaliyopita, mkuu [wa kituo cha Current TV] nchini Marekani alipata barua zenye maneno makali ya kukosoa filamu hiyo. Barua hizo zilitumwa na chama cha PSDB jimboni Minas Gerais wakisema kwamba filamu hiyo ilikuwa na chembechembe za “ushabiki wa kisiasa” na haikuwa ikieleza uhalisi wa mambo, pamoja na kuhoji maadili ya kazi yangu wakati wa kutayarisha filamu hiyo.

Kwa mujibu wa Florêncio, wakati wa uchuguzi wa ndani kwenye kituo hicho cha runinga cha Current TV ilimbidi kuthibitisha kwa mkurugenzi wa uandishi wa habari Andrew Fitzgerald kila kauli iliyotumika kwenye filamu hiyo na kwamba madai yaliyofanywa na chama hicho jimboni Minas Gerais hayakuwa kweli. Mwezi mmoja baadae, Fitzgerald alikubali kuirudisha filamu hiyo hewani.. 

Wakati huo huo, Vijana wa chama cha PSDB wametengeneza filamu nyingine , ambayo pia ina maelezo ya Kiingereza, kujaribu kujibu madai yaliyotolewa na filamu ya”Kufungiwa Brazil”.

Kwa ujumla, matukio haya yamewaacha wanablogu katika hali ya wasiwasi kwamba kuondolewa kwa video hizi si tukio la bahati mbaya. Na tabia ya zamani ya Neves inaonesha yapo mengi yanayoweza kutarajiwa katika siku za usoni.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.