Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Liberia Wawekwa Shakani Kufuatia Vita Dhidi ya Ebola

The body of a victim of Ebola virus is seen covered with a sheet at the back of a truck inMonrovia, Liberia -Public Domain

Mwili wa mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa ebola ukiwa umefunikwa kwa shuka ukiwa umepakizwa katika gari huko Monrovia, Liberia -Public Domain

Umoja wa wanahabari wa Liberia wasikitishwa na hali ya kukosekana kwa uhuru wa upashanaji habari kufuatia hatua ya serikali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya ebola. Umoja huu ulimwandikia barua Waziri wa sheria kumtaka kutafakari upya madhila wanayokabiliana nayo waandishi wa vyombo vya habari. Ufuatao ni muhtasari wa barua yenyewe:

Lengo la Umoja wa Vyombo vya habari wa Liberia umejikita haswa katika mambo ambayo siyo tu yanawakwamisha waandishi wa habari katika jukumu lao la kutafuta na kusambaza habari na taarifa muhimu kwa jamii, lakini pia, bila shaka yoyote, jambo jingine ni hili la kuhatarisha ushiriki wa vyombo vya habari katika vita ya kidunia ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola. Ni dhahiri kuwa, tasnia ya habari nchini Liberia imekuwa moja ya mshiriki mkuu katika harakati za kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na madhara na changamoto zitokanazo na ugonjwa huu wa kuambukiza. Licha ya kupoteza mapato kufuatia mlipuko wa kushtukiza wa ugonjwa huu pamoja na athari zinazokabili maisha ya kila siku, vyombo vya habari vimeendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
Kwa bahati mbaya, vikwazo kadhaa kutoka kwa watendaji wa serikali dhidi ya vyombo vya habari, hususani katika kipindi hiki, umetoa mwanya wa kuongezeka kwa hali ya sintofahamu kuhusiana na ugonjwa huu, na pia kuendelea kuongeza hali ya jamii kutokuamini uwepo wa ugojwa huu. Tunaamini kuwa hali hii haileti usawa na wala siyo sahihi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.