Televisheni ya Taifa Urusi Yahariri Wikipedia Kuibebesha Ukraine Lawama kwa Kuanguka MH17

The war in Ukraine moves to Wikipedia. Images mixed by author.

Vita nchini Ukraine imeahamia kwenye kamusi elezo ya Wikipedia. Picha zimechanganywa na Mwandishi wa makala.

Siku moja baada ya tukio baya la kutunguliwa kwa ndege mashariki mwa Ukraine iliyopoteza maisha ya watu wapatao 300, maneno ya kutafuta kujua nani wa kumlaumu kwa kuitungua ndege hiyo zimepamba moto. Viongozi wa Ukraine, Urusi, na hata waasi wanaotaka kujitenga wa Donetsk wote wamekuwa wakibebeshana lawama. Jijini Kyiv, Rais Poroshenko aliwalaumu waasi mashariki mwa nchi hiyo na kuishambulia Urusi kwa kufanya hali ya mpaka iwe tete. Jijini Moscow, Vladimir Putin aliibebesha lawama Kyiv kwa chochote kinachotokea Ukraine. Kiongozi wa waasi wa Donetsk alikana kuhusika na shambulio la ndege hiyo ya Malaysia MH17, akidai limefanywa na jeshi la anga la Ukraine.

Katika hali isiyoshangaza, mchezo huo wa kulaumiana sasa umehamia kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo vita ya wahariri kuweka kumbukumbu vinazoelekeana na upande wao. Mapema asubuhi hii, ukurasa wa Kirusi wa Wikipedia ulikuwa na andiko lililohusu kuanguka kwa ndege hiyo, ambapo mtumiaji mmoja mwenye alama ya utambulisho wa kompyuta iliyoko Kyiv alihariri habari za MH17 kusema kwamba ndege hiyo ilitunguliwa ‘na magaidi waliojitangazia nchi inayoitwa Jamhuri ya Watu wa Donetsk kwa kutumia makombora ya kisasa, yaliyotoka kwenye shirikisho la Urusi.” Ndani ya muda mfupi usiozidi saa moja, mtu mwingine mwenye alama ya utambulisho wa kompyuta ya Moscow alibadili maelezo hayo na kuandika, “ndege hiyo ilitunguliwa na wanajeshi wa Ukraine.”

Shukrani kwa mtandao wa Twita unaonukuu uhariri wowote unaofanywa kwenye kamusi elezo ya Wikipedia unaofanywa na alama za utambulisho wa kompyuta zinazotumiwa na serikali ya Urusi, kwani sasa tunafahamu kuwa uhariri huo wa pili kwa makala hiyo ya MH17 ulitoka kwenye kompyuta iliyoko kwenyeKituo cha Televisheni la Taifa la Urusi.

Makala ya Wikipedia kuhusu kuanguka kwa ndege ya MH17 ilihaririwa na VGTRK.

VGTRK ambayo ni makzi ya Dmitri Kiselyov, anayefahamanika kwa jina la utani mkuu wa propaganda wa Kremlin. Kiselyov anajulikana zaidi kwa kukosoa vikali serikali za Kyiv na Washington. Wakati wa mgogoro wa Crimea, Kiselyov aliwahi kujitapa kwenye televisheni kwamba “Urusi ndiyo nchi pekee duniani iliyobaki inayoweza kuigeuza Marekani kuwa vumbi kwa mabomu ya nyuklia.” Mwezi Juni, waandishi wawili wa VGTRK waliuawa karibu na Luhansk baada ya kuunguzwa kwa moto wakiwa na waasi wa maeneo hayo. Nadiya Savchenko, rubani wa helkopta ambaye waasi walimkamata nchini Ukraine na kumsafirisha kwenye Voronezh mapema mwezi huu, sasa anashikiliwa kwenye mahabusu ya Urusi, akituhumiwa kushiriki mashambulizi yalisababisha kuuawa kwa waandishi wa VGTRK.

Akaunti ya Twita iliyogundua matumizi ya mtandao wa intaneti yaliyofanywa na VGTRK, @RuGovEdits, imetengenezwa na zana (bot) nyingine, @CongressEdits, ambayo hufuatilia uhariri unaofanywa na Wikipedia kutoka kwenye kompyuta za Bunge la Marekani. Alama maalum ya CongressEdits, ilitengenezwa na mtaalam wa program za kompyuta Ed Summers, na ni zana huria inayoweza kurekebishwa kirahisi ili kuwezesha kufuatilia utambulisho wowote wa kompyuta.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.