Baada ya Kuchoshwa na Kudorora kwa Uchumi, Wa-Ghana Waanzisha Harakati

Photo by Victoria Okeye.

Wanachi wa Ghana wakishiriki katika harakati za #OccupyFlagStaffHouse. Picha na Victoria Okeye. Imetumiwa kwa ruhusa.

Kundi la raia wa Ghana walikusanyika karibu na Ikulu ya Rais kama sehemu ya kampeni yao #OccupyFlagStaffHouse yenye lengo la kupinga rushwa pamoja na hali tete ya uchumi ikiwa ni sehemu ya harakati zao za kuishinikiza serikali katika kukabiliana na matatizo haya.

Matembezi haya ya amani yaliyoratibiwa katika muda wa siku zisizozidi tano, yalitokea mnamo tarehe 1 Julai, 2014, siku ya mapumziko inayoadhimishwa tangu Ghana ilipokuwa jamhuri kufuatia utawala wa Kijerumani. Harakati hizi zilianzishwa katika mtandao wa Facebook kwa jina la OccupyGhana siku ya tarehe 28 Juni, na hadi kufikia Julai 1, ilikuwa na wafuatiliaji zaidi ya 3,000 waliokuwa wakiunga mkono maandamano haya. Kwa sasa ina zaidi ya waungaji mkono 6,000. 

Harakati hizi zinakuja kufuatia mfululizo wa maandamano dhidi ya serikali kutokana na kupungua kwa haraka kwa thamani ya fedha ya Ghana kwani serikali iliongeza vikwazo katika taratibu za fedha za kigeni na mwezi uliopita ikavilegeza tena,  hali iliyopelekea kupungua kwa nishati na hivyo kusababisha misururu mirefu ya watu katika vituo vya mafuta, hali iliyodumu kwa takribani wiki moja.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale serikali iliposemekana kupeleka kiasi cha dola milioni 3 za Marekani kwa ajili ya kikosi cha taifa cha mpira wa miguu Ghana Black Stars kabla ya mechi yao ya kombe la dunia dhidi ya Ureno, ambapo Ghana ilipoteza mchezo huo. Wachezaji walitishia kususia mchezo huo kama wasingepewa kiasi hicho cha fedha kabla ya mchezo huo. Mtazamo wa jumla wa tukio hili ni kuwa, serikali haikuwajali watu wake, udhalilishaji uliokithiri katika kupitia redio, televisheni na majukwaa ya mitandando ya kijamii.

Katika siku za kukaribia maandamano, kundi la OccupyGhana liliweka jumbe zilizokuwa zikielezea kutokuridhishwa na serikali pamoja na namna hali ya mambo ilivyo nchini mwao. Tarehe 29 Juni, kundi hili liliandika  katika ukurasa wa Facebook:

Jioni hii niliona magari ya polisi yakijazwa mafuta na hata kuchukua na ya ziada.

Niliziona nyuso za waendesha magari ya kukodisha wakiwa wanaapaswa kufanya kazi na kupeleka fedha kwa waajiri wao, na pia wanaotakiwa kurudisha mikopo, wanahaha ili kupata mafuta na pia kutoa mikopo kwa ajili ya kununulia nishati

Niliwaona wafanyakazi waiojawa hofu walioondoka makazini kwao saa 11 asubuhi na kisha kurejea saa 2 usiku, na kupewa ujira mdogo, wakiwa na hofu, wanaonekana wakiwa na galoni zao kwenye misururu

Na ndipo nilipowaona wapenzi walio na watoto wao ughaibuni waliokuwa wanahitaji mafuta kwa ajili ya kumpeleka baba yao kwenye matibabu, wakiwa na butwaa kuwa tatizo la kukosekana kwa mafuta lilitoka na nini.

Wauza mikate, wauza maharage, wachuuzi wa kahawa ambao hawakuweza kupata magari ya kukodisha kwa ajili ya kubeba mizigo yao.

Ndipo nilipowaona watu kama wewe na mimi, watumiaji wa Facebook, tabaka la vijana wa umri wa kati, wanaowasalimu majirani zetu walio masikini kwa kuwapungia mikono huku wakitoa salamu ya majivuno, “hamjambo”? Unajawa hofu ya namna utakavyonunua nishati, au namna ya kurudisha deni, au namna ya kufanyia matengenezo lile gari la mkopo…

Mwanamuziki wa mahadhi ya kufoka aliye na makazi yake huko Marekani @BlitzAmbassador aliye na wafuatiliaji zaidi ya 19000, alitwiti:

Watu wamechoshwa na uongozi ulioonekana kushindwa.

Mshindi wa uanahabari wa radio katika tuzo za CNN Africa @AnnyOsabutey  aliweka picha ya waandamanaji:

Picha zilizoandaliwa vizuri kutoka #OccupyFlagStaffHouse

Kufuatia maandamano haya, Rais wa Ghana John Dramani Mahama aliandika katika mtandao wa twita na kuwahakikishia wananchi kuwa madai yao yamesikiliwa na yatafanyiwa kazi:

Bado sijasahau kuwa, miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika uongozi ni kuwa na uwezo wa kusikiliza watu

Ninataka kuwahakikishia kuwa tutafanya mabadiliko. Tutaijenga nchi ambayo tutajivunia kuviachia vizazi vijavyo.

Hii ni nchi yetu, Hii ni nchi yetu, nyumbani kwetu, na pia watu wote wa Ghana wana stahili haki ya kuishi, kufanya kazi na kulea familia zetu kwa utu na kwa kujivunia.

Ni maoni mazuri, lakini yapaswa kuwa mabadiliko ya kweli– na sio kuwa maneno matupu– hii itamaanisha kuwa tunajali.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.