Misri Yapandisha Bei ya Mafuta Hadi Asilimia 78

A copy of the order to more than double the cost of fuel in Egypt. Photo source: Ahmed Kheir on Twitter

Nakala ya agiz la kupandisha bei ya mafuta kwa zaidi ya mara mbili nchini Misri. Chanzo cha Picha: @AhmedKheir kwenye mtandao wa Twita

Watumiaji wa mtandao nchini Misri wamepandwa na hasira kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta, hatua ambayo wanaamini itasababisha kupanda kwa gharama za usafiri, chakula na hata huduma nyinginezo.

Kwa mujibu wa Ahmed Kheir, mtumiaji wa mtandao wa Twita kutoka Cairo, mwenye wafuatiliaji 2,200:

Mafuta ya Oktane 92 yamepanda kwa asilimia
Mafuta ya Oktane 80 yamepanda kwa asilimia 78
Dizeli, inayotumiwa na mabasi madogo madogo na usafiri mwingineo, imepanda kwa asilimia 63
Oktane 95, inatumiwa na kada ya matajiri wa nchi hiyo, imepanda kwa asilimia 7 #haki_jamii

Takwimu hizo zimerudiwa tena kwenye taarifa ya shirika la habari la Reuters, inayosema kwamba bei zimeongezwa kwa kile kinachosemekana kuwa serikali ya Misri inajaribu kufuta ruzuku kwa nishati ili kupunguza mzigo kwenye bajeti yake yenye nakisi kubwa.”

Katika twiti nyingine, Kheir anabainisha:

Wameongoza bei ya mafuta kwa zaidi ya nusu ya bei ya awali, bila Bunge. Walichukua maamuzi kwa siri tena kwenye siku ya mapumziko. Vitendo hivi vyote hufanywa na wezi tu.

Peter Ramez, mwenye wafuatiliaji 500 kwenye mtandao wa twita, anamlaumu rais mpya wa Misri Abdelfattah El Sisi, kwa ongezeko hilo, akisema:

Ongezeko la asilimia 40 kwa bei ya mafuta nyie wadhalimu?
Haki ya Mungu ikutane nanyi. Mnastahili kila aina ya laana mtakazozipata

Na Ahmed Fathi El Badry anaongeza:

Hivi kweli mnadhani upendo wa watu kwenu utamaanisha chochote baada ya uamuzi huu? Hatua hii ni kifo chenu wenyewe cha kisiasa na kijamii

Wengine walichagua kutumia utani kueleza kuchanganyikiwa kwao. Shay Sokar Bara, mwenye wafuasi 83,000 kwenye mtandao wa twita, anasema:

Sikuasi dhidi ya [rais wa zamani Mohamed] Morsi kwa kuengeza ruzuku au kupunguza bei ya umeme au kutoa kwa hisani [fedha zangu kwa serikali]. Sina chochote na wala sitaki kwenda jela kwa kugoma

Katika twiti nyingine, anabainisha:

Wamisri wamejipanga kwenye vituo vya kuuzia mafuta na kila mmoja anasema wanajaza matanki yao ya akiba kabla bei hiyo haijaanza kupanda. Sisi ni taifa la werevu. Ni kama vile mafuta kwenye matanki ya akiba hayatakaa yaishe

Na Hesham Mansour anatania:

Kuongezeka kwa bei ya mafuta ni ongezeko la kimkakati. Baada ya kuongeza bei ya mafuta na umeme, serikali inataka raia wake wakose kabisa fedha za kujilipua kwa moto

Twiti hii inatukumbusha tukio lililosababisha mapinduzi ya Kiarabu, mwezi Desemba 2010, wakati mchuuzi wa matunda wa Kitunisia Mohammed Bouazizi kujilipua kwa moto.

Wakati huo huo, video hii kutoka kwa Mansoura inanyesha foleni ndefu za magari kwenye kituo cha kuuzia mafuta, ambavyo vimeanza kukosa mafuta hayo:

Nini mustakabali wa Wamisri?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.