Wanajumuia wa Global Voices Washinda Tuzo za Knight News Challenge za Kuboresha Huduma ya Intaneti

Global Voices co-founder, Rebecca MacKinnon, was awarded a Knight News Challenge award to develop a global ranking of Internet companies. Photo by Brooke Bready.

Mwanzilishi wa Global Voices, Rebecca MacKinnon, alitunukiwa tuzo ya Knight News Challenge kwa ajili ya kutayarisha safu ya kiulimwengu ya makampuni yanayotoa huduma ya intaneti. Picha na Brooke Bready.

Jumuia ya Global Voices inawapongeza wanajumuia wetu wawili ambao ni miongoni wa washindi wa tuzo ya mwaka 2014 ya Knight News Challenge. Matokeo ya shindano hili yametangazwa leo katika Ukumbi wa MIT-Knight Civic Media  Cambridge, Massachusetts. Mwaka huu, taasisi ya Knight yenye maskani yake huko Miami ilitoa fedha kiasi cha dola za Marekani 3,466,000 katika miradi iliyolenga kujibu swali lililouliza: “Ni kwa jinsi gani tunaweza kuimarisha mtandao wa intaneti kwa ajili ya uhuru wa kujieleza na ubunifu?”

Mwanzilishi mshiriki wa Globalvoices, Rebecca MacKinnon,alipokea kiasi cha dola za Marekani 300,000 ili kumwezesha yeye pamoja na wenzake wa taasisi ya New America katika kuandaa Safu ya Haki za Digitali. Ufadhili huu utamuwezesha Rebecca na wenzake katika kuandaa safu itakayoonesha ni kwa kiasi gani makampuni yanayotoa huduma ya intaneti yanavyoweza kutunza haki za wateja wao, ikiwa ni pamoja na kuiweka hadharani rafu hiyo ya kidunia kwa lengo la kuyahamasisha makampuni hayo kuboresha huduma zake.

Rebecca alifafanua, “watu wanatumia majukwaa ya mitandao ya kijamii, huduma za mawasiliano pamoja na simu za gharama kutoka katika makampuni haya”. “Sera na utendaji kazi wao ni upi?” Rebecca aliongeza kuwa, mradi ya kuandaa Safu ya Haki za Digitali uliungwa mkono katika majadiliano yaliyofanyika katika Kongamano la mwaka 2012 la Global Voices lililofanyika Nairobi, Kenya. “Nilikuwa nikijadiliana na watu mbalimbali kuhusu namna ambavyo tunavyoweza kuyawajibisha makampuni yanayotoa huduma ya intaneti, hapo ndipo[mwanajumuia wa Jumuia ya Watu wa Misri] Mohamed ElGohary aliposema, “ningependa kuona orodha.” Na pia, watu wengine waliendelea kuliunga mkono jambo hili.”

Jillian C. York's Knight News Challenge-winning project will tackle

Jillian C. York aliye miongoni mwa washindi wa tuzo ya Knight News Challenge ambaye mradi wake utahusika na kukusanya taarifa za udhibiti wa taarifa katika majukwaa ya mtandaoni kama vile Facebook na Twitter. 

Mradi wa mwanajumuia mwingine wa Global Voices aliyejipatia tuzo kwa kazi yake nzuri, Jillian C. York, utajikita zaidi kwenye makampuni binafsi, pamoja na kuwa, malengo yake yatakuwa kwa mtazamo tofauti.

Jillian, aliyejiunga na Global Voices mwaka 2007 na kufanya kazi kwenye jukwaa hili kama mwakilishi wa kujitolea, alitunukiwa kiasi cha dola za Marekani 250,000 kwa ajili ya OnlineCensorship.org, jukwaa atakalolianzisha yeye pamoja na wenzake katika taasisi ya  Electronic Frontier, ambapo, yeye ni mkurugenzi wa taasisi ya Uhuru wa Kimataifa wa Kujieleza. Katika vipau mbele ilivyojiwekea, jukwaa hili litakusanya taarifa kuhusiana na matukio ya udhibiti wa taarifa katika majukwaa ya mtandaoni kama vile Facebook na Twitter, ikiwa na lengo la kuisaidia jamii kuwa na uelewa mpana na namna ya kukabiliana na mambo yanayohusiana na udhibiti wa taarifa na uhuru wa kujieleza.

“Wengi wetu tumeshashuhudia matukio ya makampuni ya uanahabari wa kijamii yakiondoa baadhi ya yale tuyawekayo katika mitandao na pia kufunga akaunti zetu,”Jillian alidokeza. “Kwa kweli, hali hii ipo kila mahali”. Ni matumaini yangu kuwa jumuia ya Global Voices itachangia katika kutoa taarifa ambazo zitatuwezesha kuyaonesha makampuni pamoja na ulimwengu kuhusiana na madhara halisi yatokanayo na vitendo vya makampuni binafsi kudhibiti uhuru wa kujieleza wa mtandaoni”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.