PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”

Thousands of anti-greed bill protestors gathered at Tap Seac Square before the rally started. Photo from All About Macau Facebook page. Non-commercial use.

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga muswada uliopachikwa jina la Ulafi wakiwa wamekusanyika kwenye viwanja vya Tap Seac kabla ya mkutano kuanza. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa All About Macau. Kwa matumizi yasiyo ya kibiashara.

Zaidi ya wakazi 20,000 wa eneo la Macau nchini China waliandamana siku ya Jumapili, Mei 25, 2014, kupinga muswada  utakaowalipa fidia maafisa waandamizi baada ya kuondoka madarakani na kumkinga mkuu wa serikali na makosa yoyote ya kijinai  wakati au baada ya muhula wake wa uongozi.

Macau, ambalo ni jimbo maalum la kiutawala la China, lina idadi ya watu wanaofikia 500,000. Waandamanaji walikuwa ni asilimia nne ya idadi yote ya watu, na hivyo kuwa maandamano makubwa zaidi tangu koloni hilo la zamani la Ureno halijakabidhiwa kwenye mamlaka ya China mwaka 1999. Hasira ya watu hao iliwashangaza wengi, hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya upinzani vinaonekana kuwa bado dhaifu kwenye mji huo na pia kwa vile vyombo vingi vya habari vinaonekana kushambikia serikali kwa kuwa vinapokea ruzuku ya serikali.

Muswada huo, unaotarajiwa kupitishwa siku ya Jumanne, Mei 27, 2014, ulitungwa na Waziri wa Macau wa Utawala na Sheria mwezi mmoja uliopita na ulipendekezwa bila ridhaa ya umma. Muswada huo utamhakikishia mkuu wa serikali kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai akiwa madarakani. Vile vile muswada huo utahakikisha kuwa mkuu wa serikali anayeondoka madarakani, sambamba na maafisa wakuu walio chini yake, wataendelea kupata mishahara yao ya kila mwezi yanayofikia asilimia 70 ya mishahara yao ya sasa. Waziri huyo anadai kuwa muswada huo una lengo la kuwavutia wafanya biashara kujiunga na siasa.

Uchaguzi wa mkuu wa serikali utafanyika mwishoni mwa mwaka 2014, na baada ya hapo maafisa wakuu wa serikali nao wataondoka madarakani. Wengi wanaamini kuwa muswada huo umesukwa kwa ajili ya kumnufaisha Mkuu wa Serikali Fernando Chui Sai-on na vigogo wa serikali kwa sababu ndio watakaokuwa wanufaika wa maslahi hayo.

Ingawa muswada huo umejaa utata mwingi, bado serikali imekuwa ikishinikiza baraza la kutunga sheria kuupitisha. Wengi wa watunga sheria ama wamechaguliwa na makundi yao au wameteuliwa na mkuu wa serikali.

Kuishinikiza serikali kuutupilia mbali muswada huo, kikundi cha raia wanaoguswa na hali hiyo wanaoitwa “Macau Conscience” [Dhamira ya Macau] waliandaa maandamano kupinga “Muswada wa Ulafi na Upendeleo.”

Chombo huru cha habari cha All About Macau kilimwomba mmoja wa waandamanaji  kwenye kundi la Facebook kwa nini alijiunga na maandamano hayo:

市民林小姐認為特首在有可能臨離任的時候通過這個法案,是「打劫澳門市民」,根本是與民為敵;

Mama Lam anaamini kuwa mkuu wa Serikali atakayefurahia maslahi hayo manono atakuwa “anawaibia raia wa Macau” na atakuwa anajigeuza kuwa adui wa watu.

Watu wengi walionyesha hasira yao kupitia mabango wakati wakiandamana.

 A protest placard showing the Macau Chief Executive's face on a underworld bank note. The slogan on the placard is:  A monthly salary more than 200 thousand dollars [about 25 thousand US dollars] wanted out-going compensation? Impotent officials are out of their mind! Photo from All About Macau Facebook Page

Mwandamanaji akiwa amebeba bango linaloonyesha kichwa cha mkuu wa serikali kikiwa kwenye noti bandia. Maneno yanasomeka: “Mshahara wa mwezi zaidi ya pataca 200,000 [yapata dola za marekani 25,000] zinahitajika kwa ajili ya kumfidia anapoondoka? Maafisa hawa wasio na nguvu yoyote wamerukwa na akili!” Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa All About Macau

Young people stand out and say no to the Bill of Greeds. Photo from All About Macau Facebook page. Non-commercial use.

Vijana wakipinga “Muswada wa Ulafi.” Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook All Macau. Kwa matumizi yasiyo ya kibiashara.

Protestors stick  the face of Secretary for Administration and Justice, Florinda Chan Lai-man, onto a pig-shape placard to mock at her greed. Chan is the drafter of the bill. Photo from All About Macau's Facebook page. Non-commercial use.

Waandamanaji wakiwa wamebandika uso wa Waziri wa Utawala na SheriaFlorinda Chan Lai-man kwenye sanamu ya nguruwe. Chan ndiye aliyetunga muswada huo. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa All About Macau. Kwa matumizi yasiyo ya kibiashara.

A young man staged the PK body posture against  the Greed Bill in the protest. PK posture is an bodily expression of absurdity among youngster in East Asia.] Photo posted by Facebook user Ar B Cheong. Non-commercial use.

Kijana akiigiza mkao unaojulikana kama PK, kupinga muswada huo wakati wa mkutano. Mkao huo unakusudiwa kumaanisha ujinga na unatumiwa na vijana Asia ya mashariki. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Facebook na mtumiaji aitwaye Ar B Cheong. Kwa matumizi yasiyo ya kibiashara.

Baada ya mkutano, baadhi ya watunga sheria na madiwani wanaounga mkono serikali waliviambia vyombo vya habri kuwa watashauri utawala wa Baraza la Wawakilishi kuunda kamati ya kuupitia upya muswada huo. Kwa wakati huo huo, waandaaji wa maandamano hayo ya “Macau Conscience” walisema wataendelea kuchukua hatua zaidi kama muswada huo utapitishwa na baraza la kutunga sheria siku ya Jumanne.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.