Global Voices Advocacy ilianzisha mtandao wa Tumblr mapema mwezi Mei kutafuta uungwaji mkono kwa wanablogu tisa na waandishi wa habari – ambao wanne kati yao ni wanachama wa Global Voices – ambao kwa sasa wako kizuizini nchini Ethiopia shauri ya kazi zao. Washirika kutoka duniani kote waliwasilisha picha, ujumbe wa mshikamano, video na michoro kuonyesha kuunga mkono shinikizo hilo la kuachiliwa huru kwa wanablogu hao. Mei 19 #FreeZone9Bloggers Tumblr ilianza kuvuma katika tovuti ya vyombo vya habari vya kijamii. Unaweza kuwasilisha picha kwa Tumblr au jifunze njia nyingine unazoweza kuzitumia kusaidia kampeni hiyo ya utetezi.