Madai ya Ukiukaji wa Haki za Binadamu Wakati wa Mgomo wa Kilimo Nchini Colombia

Tovuti ya ‘kongamano la watu’ imeshutumu hadharani [es] uvunjifu wa haki za binadamu unayoendelea katika mgomo wa kilimo [es] nchini Colombia. Wanaripoti madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika mikoa mbalimbali: Catatumbo na Cucuta, San Pablo-Bolívar, Sogamoso – Boyaca, Kaskazini Santander-Hacarí, Yopal-Casanare, Boyaca, Berlin – Santander, Pinchote – Santander y Arauca. Pia walitoa wito:

Kwa vyombo vya kimataifa vyakutetea haki za binadamu, kuingilia kati na kudai ufumbuzi wa haraka na halisi ya hali inyayoikabili nchi.

Kwa jamii ya kitaifa na jumuiya ya kimataifa na vyombo vya kutetea haki za binadamu, kuongea kuhusu ukweli uliotajwa katika dai hili.

Kwa jamii ya kitaifa na jumuiya ya kimataifa na vyombo vya kutetea haki za binadamu kudai usalama wa watu wanaohusika na kila msemaji wa mgomo wa kitaifa..

Posti iliyochambuliwa hapa ilishiriki katika kampeni ya [es] #LunesDeBlogsGV [Jumatatu ya Blogu] ambayo ni ya kwanza mnamo Mei 5, 2014, ilitumwa na Cati Restrepo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.