Maandishi ya Facebook Kukosoa Kuivamia Crimea Yamgharimu Mwandishi Ajira

An "unidentified" soldier is defending this Russian-speaking cat. "Thanks for the fact that I'm no longer a "kit"" (Ukrainian for "cat" (kit) is a homonym of Russian for whale (kit)). Anonymous image found online.

Mwanajeshi “ambaye hakutambuliwa jina” akiwa anamlinda paka azungumzaye Kirusi. “Nashukuru kwa ukweli kuwa mimi si paka. Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani

Wakati watu wakikijadili kitendo cha serikali ya Urusi kudhibiti vyombo vya habari pamoja na mtandao wa intaneti nchini Urusi, sasa imekuwa ni kawaida kabisa vitendo wa udhibiti wa jinsi hiyo kufanyika kwa ngazi za chini, kama vile mashirika ya habari. Kuna tukio la hivi karibuni zaidi ambapo mwandishi wa habari wa Pem alitimuliwa kazi kwa kunukuu maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwenye blogu moja na kuyaweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Facebook kwa namna ya kawaida sana.

Bandiko la awali liliandikwa na Roman Romanenko wa Vologodsk, mnamo Machi 4, 2014. Kwenye bandiko hilo, Romanenko, ambaye naye anafanya kazi ya uandishi wa habari, aliandika maandishi makali akitoa mwito kwa Putin ‘kulikalia’ Jimbo la Vologodsk, ili kulinda haki za watu ‘wanaozungumza Kirusi’ wanaoishi eneo hilo. Romanenko alikuwa, kwa hakika, akirejea madai ya Urusi kuvamia eneo la Crimea (ingawa maafisa wa serikali ya Urusi bado wnakanusha uwepo wa vikosi vya kijeshi kule). Kwa uwazi kabisa aliandika [ru]:

Мы тут все сплошь русскоязычные и наши права очень ущемляются. Наши больные не могут получить нужных им лекарств и лечения, уровень нашего образования падает с каждым годом […] А еще мы узнали, что вы собираетесь потратить много денег, чтобы нормализовать жизнь в Крыму. Стесняемся спросить: можно ли потратить эти деньги на нормализацию жизни в Вологодской области. А то наша область в такой долговой яме, что ни на что денег не хватает. А нам очень нужны мосты, дороги, спортивные сооружения, промышленные объекты, новые рабочие места…

Sisi sote ni watu tunaoongea Kirusi hapa, na haki zetu zinapuuzwa. Wagonjwa wetu hawawezi kupata madawa wala huduma za kitabibu wanazozihitaji, elimu yetu inaendelea kuporomoka kila mwaka […] Pia, tumesikia kuwa unapanga kutumia ‘mapesa’ mengi kuboresha maisha ya wa-Crimea. Hatusiti kuuliza: je si vizuri fedha hizi zikatumika kuboresha maisha ya watu wa Jimbo la Vologodsk? Kwa sababu jimbo hilo liko kwenye madeni mengi, hatuna fedha kwa ajili ya chochote. Na tunahitaji madaraja, barabara, michezo, maendeleo ya viwanja, maeneo mapya ya kazi…

Alexander Erenko, mwandishi kutoka Perm, alinukuu  [ru] maandishi hayo na kuyaweka kwenye ukurasa wake wa Facebook, na akabadilisha maelezo yake ya alikozaliwa kuwa Vologodsk. Ingawa alichokiandika kilinukuliwa mara 44 pekee, ukilinganisha na mara 3,323 ambapo bandiko la awali la Romanenko lilinukuliwa, maneno hayo yalimwingiza matatani na mmoja wapo wa wakuu wake wa kazi. Erenko akatimuliwa kazi ndani ya saa moja, akama inavyoandikwa na Echo of Perm [ru] (ofisi ya mikoani ya Echo Moskvy).

Wakati huo huo, Romenenko hakuwa mtu peke aliyeleta mtazamo wa tofauti wa namna gani Moscow inaonekana kuwatendea raia wa Crimea, na namna gani inashughulika na wananchi wake nyumbani. Twiti hii kutoka kwa mwanablogu Irina Petrova ilisambaa kwa kadri ya mara 1000, na kiongozi wa upinzani Alexey Navalny akiwa ni mmoja wapo wa walioisambaza (hata kama bado anatumikia kifungo cha nyumbani na kimsingi haruhusiwi kuonana na watu):

Gavana wa Jimbo la Moscow atatenga Ruble za Urusi milioni 40 kutoka kwenye bajeti ya jimbo hilo kukarabati hospitali huko Crimea. Ukichaa huu!!! Hivi amewahi kwenda kwenye hospitali za Jimbo la Moscow???  

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.