Kuchanwa kwa Korani Kwaleta Tafrani Nchini Mauritania

Mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott ulishuhudia mapigano kati ya vikosi vya usalama na umati wa “wananchi wenye hasira”. Habari ni kwamba watu wasiojulikana waliichana chana Quran, kitabu kitakatifu cha Kiislamu, katika moja ya misikiti ya jiji hilo. Matokeo ya mapambano hayo, mtu mmoja aliuawa na watu mbalimbali walijeruhiwa na barabara zilifungwa katika maeneo mengi ya Nouakchott. Mapigano yaliyotokea Machi 3.

Akizungumzia tukio hilo, mwanablogu Abbas Braham alitoa wito kwa marafiki wake kwenye mtandao wa Facebook kuwa waangalifu na si kuanguka katika mtego uliokithiri (bila kujali ni nini) [ar]:

حادثة “تدنيس”* المصاحف اليوم في العاصمة نواكشوط هي حالة تستدعي الانتباه والحذر. فلقد أصبح واضحاً أن التطرف القداسي والتطرف التدنيسي يغذيان بعضهما. وفي كل مرة نتعرض نحن في الوسط من المؤمنين باحترام المقدسات و/أو باحترام الحريات والحقوق لنيرانهما.

Tukio la leo la “kuharibiwa” Koran tukufu katika jiji la Nouakchott, limekuwa ni tukio linaloibua wasiwasi na tahadhari. Kwa sasa ni wazi kwamba watu wenye msimamo mkali wa kidini wanaathiri wengine. Na kila wakati, ni sisi – wale tulioko katikati (linapokuja suala la kuheshimu imani za kidini na/au uhuru na haki) – ambao tunakuwa waathirika wakuu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.