Jaribio la Mapinduzi? Mgogoro wa Kikabila? Tafakuri ya Machafuko ya Sudan Kusini

Salva Kiir, rais wa Sudan Kusininchi mpya zaidi duniani, alisema kuwa Desemba 16, mwaka 2013 jaribio la mapinduzi lililoanzishwa na wanajeshi wafuasi wa makamu wa rais wa zamani, Riek Machar, limekomeshwa. Riek Machar amepinga madai hayo, akisema kwamba mapambano yalikuwa matokeo ya mgogoro kati ya wanakundi wa kikosi cha kumlinda rais.

Machar alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa nchi hii ya Kiafrika kabla hajafutwa kazi na Kiir mwezi wa Julai, mwaka wa 2013.

Inasemekana kwamba raia takribani 500 wameuawa tangu kuanza kwa machafuko hayo.

Je, kulikuwa na mapinduzi Desemba 16? Na machafuko yanayoendelea ni mgogoro wa kikabila ama la?

President of South Sudan Salva Kiir Mayardit outside the Security Council chamber, at UN Headquarters in New York. Photo released under the GNU Free Documentation License  by Jenny Rockett.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, nje ya chumba cha Baraza la Usalama, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York. Picha imetolewa na Jenny Rockett chini ya Leseni ya Matumizi Huru ya Nyaraka ya GNU.

 

Mambo yepi yangemsababisha Rais Kiir kujaribu kumlaumu makamu wake wa awali? Lesley Anne Warner, mchambuzi Mwafrika wa masuala ya usalama, hutueleza:

Uhasama wa kisiasa ulikuwa umezidi tangu baraza zima la mawaziri, hususan Makamu wa Rais Riek Machar, lilipofutwa kazi na Rais Kiir mwezi Julai. Kwa sasa, pahali alipo Riek Machar hapajulikani kwa hakika. (Nimejaribu kuanzisha alama ashiria ya #WhereIsRiek [#RiekYuWapi], lakini kwa bahati mbaya haijapata hadhira.) Salva hakukawia kumlaumu Riek kwa machafuko haya. Lakini, kwa maoni yangu, Riek amekuwa akijaribu kukarabati jina lake kwa muda wa miaka mingi baada ya jaribio la mapinduzi la Nasir la 1991. Yamkini angejaribu juu chini kupata suluhisho ya kisiasa kabla hajafikiria vita. La muhimu hapa ni suala moja: Ni nani atakayefaidika nchi ya Sudan Kusini na jumuiya ya kimataifa zikikumbushwa kuhusu vitendo vya kale vya Riek?  Jawabu ni Rais Kiir. Ndiye mwenye hamu ya kuimarisha taswira yake kama kiongozi wa Sudan Kusini baada ya kulipanga upya baraza la mawaziri na katika maandalizi ya uchaguzi wa 2015. Ona jinsi Rais Kiir alivyovaa sare yake ya kijeshi (ambayo hajaivaa kwa miaka mingi) badala ya kofia yake ya kawaida ya “pama” alipohudhuria mkutano wa wanahabari aliouandaa kuzungumzia matukio ya jana

Je, mgogoro huu ni ugombezi wa madaraka kati ya makabila wawili, Wadinka na Wanuer? Rais Kiir ni Mdinka (kabila kubwa zaidi nchini Sudan Kusini) na Machar ni Mnuer. Mwanablogu Msudan Kusini, PaanLuel Wël ametupilia mbali maelezo hayo:

Inasemekana kuwa mafyatuliano hatari ya risasi miongoni mwa walinzi wa rais ni vita kati ya Wadinka (kabila ya Rais Kiir) na Wanuer (kabila ya Dk. Riek Machar), makamu wa rais wa kale wa Sudan Kusini. Lakini idadi kubwa ya viongozi wakuu wa SPLM wanaotiwa nguvuni ni Wadinka – kutoka Bor na Bahr el Ghazal. Na hata watu kutoka Equatoria na Washilluk. Kwa hivyo suala ni lipi? Wasudan Kusini wanapaswa kutatua matatizo kati ya walinzi wa rais na kutupilia mbali kisa cha kulaumu makabila mawili na kudhabihu wapinzani wa kisiasa wasio na hatia.

Zaidi ya hayo, Wël hufikiria matukio tofauti yanayoweza kukomesha mgogoro huu:

Mbali na msiba huu, yachekesha kuona jinsi serikali inavyokabiliana na matokeo ya uasi – inajifanya kama kwamba ni ushindi mkubwa badala ya mwanzo wa msiba utakaokumba taifa.

Jambo moja li wazi: Mgogoro huu hautatatuliwa ila kwa upatanishi wa kupangwa kati ya Rais Kiir na Riek Machar. Riek Machar atarudi mjini Juba kama Makamu wa Rais wa kwanza nchini Sudan Kusini; yawezekana kwamba kutakuwa na kishazi kitakachozuia kufutwa kwake kazi na Kiir. Kama hayo ndiyo yatakayotokea, si itakuwa bora zaidi kuanzisha mazungumzo na suluhisho lenye amani MARA MOJA badala ya kungojea vifo vya watu wengine kutoka pande zote mbili kabla hawajatekeleza mapatanisho?

Martin Garang anadhani kwamba mgogoro ulisababishwa na mapinduzi ama kushindwa kwa vikosi vya usalama kuushughulikia mchakato wa uteuzi vyema:

Mpaka sasa, maraia wamekuwa nyasi zinazoumia fahali wawili wapiganapo; wamevamiwa bila sababu au kufungiwa kwenye nyumba zao mjini Juba bila chakula au maji. Taarifa zinadokeza kwamba Bor, mji mkuu wa Jonglei, umestahimili upigaji risasi mwingi, na vifo vingi vimetangazwa.

 

Aidha mchafuko ulikuwa mapinduzi ama vikosi vya usalama vilishindwa kuushughulikia machakato wa uteuzi vyema kwenye makao yao. SPLM imechafua sifa yake kwa kitendo cha kutia hatarini maisha ya watu wasio na hatia. Licha ya ukweli kuhusu madai ya serikali, maneno matupu na malalamiko ya viongozi kuhusu uwezo wa nchi ndiyo yaliyosababisha hali ya mambo iliyomo mjini Juba.

 

Sudan Kusini ina historia ya mapinduzi kadhaa ambayo yalihusisha ukabila kwa kadiri kubwa wakati wa miongo ya vita vya uhuru. Ni ukweli unaoonekana wazi kwenye vipengele vyote vya maisha nchini humo. Kwa hivyo, ni jukumu la uongozi wa SPLM kukabiliana na ukweli huu kwa kuwahimiza waongozi kutotumia hila za ukabila katika michezo yao ya kisiasa.

Akiandika kwenye tovuti ya African Arguments, Jairo Munive (anayeshughulikia utafiti ufuatao mapokezi ya shahada ya uzamivu katika Kitengo cha Amani, Hatari na Vurugu kwenye Taasisi ya Masomo ya Kimataifa) huashiria kwamba huenda yaliyotokea nchini Sudan Kusini siyo mapinduzi:

Lakini je, tunayoshuhudia nchini Sudan Kusini ni mapinduzi? Pengine siyo mapinduzi. Kwanza, ni lazima watu wayasahau au kuyatahadhari maneno yanayotumiwa na wahusika wa mgogoro. Rais Kiir ameongea juu ya “jaribio la mapinduzi” na “vitendo vya jinai,” huku Machar anazungumza juu ya “utungaji wa njama ya mapinduzi, lengo lake likiwa kuangamiza upinzani… nchi iwe na umoja; haiwezi kuhimili utawala wa mwanamume mmoja au udikteta”.

 

Ni bora zaidi kufikiria utengano ambao unaonekana kuwa umekumba SPLA. Kwa sasa, kwa maoni ya mkuu wa Ujumbe wa Muungano Nchini Sudan Kusini, Hilda Johnson, ya muhimu haswa ni nidhamu, ukamanda na udhibiti kwenye vikosi vya usalama. Kuyatambua matukio ya hivi karibuni, tunafaa kuelewa SPLA- siasa zake, mivutano iliyomo, na visa vyake

 

Siasa za Kisudan Kusini zimehusishwa na vita vya ukali wa kiwango cha chini, vurugu baina ya makabila na desturi za mamlaka zilizojengwa juu ya msingi wa vurugu. Vurugu hizi zinakusudiwa kuzalisha uaminifu, hofu na uhalali wa wenye uwezo kwenye mioyo ya wakaazi wa eneo fulani ama ya watu wa kabila fulani. Jeshi nchini Sudan Kusini ni muhimu kwa njia mbili: inawapa watu nafasi penye wanaweza kushughulikia siasa, na inawahudumia kwa ‘kutimiza masilahi yao’ kwenye nchi hii changa. Zaidi ya hayo, katika jeshi mna utengano mwingi wa kisiasa kama ilivyo nchini Sudan Kusini.

 

Matukio ya wiki hii yanashuhudia kwamba mazingira ya kisiasa nchini Sudan Kusini bado yana uwezekano wa kusababisha kushirikishwa kwa wanajeshi. Usaliti na mizozo ya ndani imeathiri SPLA kwa muda wa miaka kadhaa. Makamanda, hususan wale wa makundi mengine yenye silaha yaliyojiunga na SPLA (haswa wale kutoka SSDF), wameitikia ukosefu dhahiri wa ushirikiano na mamlaka, uwezo na ukamanda wa jeshi.

Kwenye mtandao wa Twitta, watu waliotumia alama ashiria ya #SouthSudan (#SudanKusini) walisema haya:

Kusisitiza kwa #SalvaKiir kwamba yaliyotokea yalikuwa mapinduzi,kunamfanya apoteze uaminifu na kunasababisha nchi ya #SudanKusini kupoteza huruma + uungaji mkono wa nje.

Tuyaonayo yanalingana na vyenye wachambuzi wamekuwa wakisema kwa muda wa miaka mingi, #SPLA hamna ushikamano. Bali kuna makada wanaotii waongozi tofauti. #SudanKusini

Methali mpya ya Kiafrika?? “Mwenye #bunduki husababisha ghasia nyingi mno” #SudanK #Juba #SudanKusini #SalvaKiir #RiekMachar #Kenya

Wafaransa hawakutia #SudanKusini ukoloni. Kwa hivyo hawawezi kuingilia kati. Na kama kawaida, #UmojaWaAfrika, unalala chini ya blanketi nzito!

Ulafi wa #Uongozi: #SudanKusini ilipokuwa sehemu ya #Sudan, watu walidhani kwamba mji wa Khartoum ulikuwa Ibilisi WA PEKEE. Basi mbona kisa hiki kimetokea? #Afrika

Unapoombea #SudanKusini, je ombi lako hushughulikia kumrejesha fahamu Kiir na kuacha kwake udikteta?

Ninaisema tena: Waheshimu wanahabari #Waafrika washupavu wanaoripoti juu ya #SudanKusini! Visa vingi bado havijasimuliwa… http://t.co/S8XWHvUHdl

1 maoni

  • […] Jaribio la Mapinduzi? Mgogoro wa Kikabila? Tafakuri ya Machafuko ya Sudan Kusini Salva Kiir, rais wa Sudan Kusini, nchi mpya zaidi duniani, alisema kuwa Desemba 16, mwaka 2013 jaribio la mapinduzi lililoanzishwa na wanajeshi wafuasi wa makamu wa rais wa zamani, Riek Machar, limekomeshwa. Riek Machar amepinga madai hayo, akisema kwamba mapambano yalikuwa matokeo ya mgogoro kati ya wanakundi wa kikosi cha kumlinda rais. Machar alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa nchi hii ya Kiafrika kabla hajafutwa kazi na Kiir mwezi wa Julai, mwaka wa 2013. Inasemekana kwamba raia takribani 500 wameuawa tangu kuanza kwa machafuko hayo. Je, kulikuwa na mapinduzi Desemba 16? Na machafuko yanayoendelea ni mgogoro wa kikabila ama la? Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, nje ya chumba cha Baraza la Usalama, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York. Picha imetolewa na Jenny Rockett chini ya Leseni ya Matumizi Huru ya Nyaraka ya GNU.   Mambo yepi yangemsababisha Rais Kiir kujaribu kumlaumu makamu wake wa awali? Lesley Anne Warner, mchambuzi Mwafrika wa masuala ya usalama, hutueleza: Uhasama wa kisiasa ulikuwa umezidi tangu baraza zima la mawaziri, hususan Makamu wa Rais Riek Machar, lilipofutwa kazi na Rais Kiir mwezi Julai. Kwa sasa, pahali alipo Riek Machar hapajulikani kwa hakika. (Nimejaribu kuanzisha alama ashiria ya #WhereIsRiek [#RiekYuWapi], lakini kwa bahati mbaya haij… Kusoma makala kamili  »  https://sw.globalvoicesonline.org/2014/01/jaribio-la-mapinduzi-mgogoro-wa-kikabila-tafakuri-ya-machafuko-ya-sudan-kusini/ […]

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.