Mkutano: Kutengeneza Dunia Halisi ya Sauti za Dunia kwa Hadhira Halisi

Je, umekuwa ukisoma habari zao na umekuwa ukiwafuatilia kwenye mtandao wa twita kwa miaka kadhaa, lakini hujawahi kukutana na waandishi wa Global Voices na wafasiri wanaoandika kuwakilisha nchi zenu?

Katika majira haya ya mwaka tumeanzisha “mkutano” wetu wa kwanza rasmi wa ana kwa ana kwa kuongozwa na kuendeshwa na wanachama wa Global Voices, wanaoishi na kuzifahamu jamii za mahali katika nchi sita.

Na tayari tupo nusu ya safari kufikia malengo hayo!

Katika toleo la wiki hii la GVFace, nilizungumza na:

Eddie Avila, Mkurugenzi wa Kitengo cha Rising Voices, kinachoshughulika na kuinua sauti za wanablogu wanaochipukia yeye akiwa Cochabamba, Bolivia
Mohamed ElGohary, Mratibu wa Mradi wa Tafsiri (Lingua) akiwa Misri
Faisal Kapadia, Mhariri wa Tafsiri ya Urdu, akiwa Karachi, Pakistan
Sara Moreira, Mhariri wa Kireno akiwa Porto, Portugal

Walitushirikisha uzoefu wao katika juhudi za kuyafikisha maono, ari na upendo wa Global Voices kwa hadhira ya kweli isiyopatikana mtandaoni katika nchi zao.

Huko Karachi, Kampala, Cairo na Skopje washiriki wengi tayari wamekutana na  wanachama wa Global Voices waliowezesha mafunzo ya vikundi na kushirikishana maarifa katika tasnia ya uandishi wa kiraia. Na wawezeshaji wa Mikutano hiyo ya GlobalVoices wanajiandaa kukutana na hadhira ya wakazi wa Porto na baadae Phnom Penh!

Kwa taarifa zaidi kuhusiana na haya tafadhali tembelea Ukurasa wetu wa Matukio.

 

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.