Ulaya Yamuonya Waziri wa Ufaransa Kuhusu Matamshi Yake Dhidi ya Warumi

Manifestation de Roms à Paris en 2007 photo Philippe Leroyer licence creative commons

“Komesheni Mashambulio” Maandamano ya Warumi mjini Paris – picha ilipigwa na Philippe Leroyer – leseni ya 3.0 ya creative commons

 

 

Matamshi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Manuel Valls, yalifufua uhasama uliokuwepo kati ya Ufaransa na Warumi. Bw. Valls alisema katika idhaa ya France Inter radio [fr] tarehe 24, mwezi wa Septemba:

ces populations ont des modes de vie extrêmement différents des nôtres et qui sont évidemment en confrontation [avec les populations locales]”.

Jamii hii ina utamaduni tofauti sana na wetu, na ni wazi kwamba utamaduni wao unahitilafiana na huo wa majirani zao.

Watumiaji wa Twita wazungumzao Kifaransa walimjibu, baadhi yao wakiandika kwa kejeli:

Warumi ndio wanaosababisha matatizo yetu yote, wao ndio wanaosababisha zaidi ya 25 % ya vijana barani Ulaya kukosa ajira.

Familia za Warumi zimejikuta mashakani: Ulaya, inayostahimili kuzorota kwa hali ya maisha, inawakataa, na mifumo ya kimafia inazidi kutajirika

Kwa vile alishughulikia suala nyeti lililogusia haki za binadamu nchini Ufaransa, Waziri alionywa na Baraza la Ulaya:

Ce débat perpétue une tendance inquiétante vers une rhétorique anti-roms discriminatoire et incendiaire, et risque de prendre un virage dangereux avec les prochaines élections municipales et européennes.”

Mjadala huu unaendeleza mwelekeo wa kusikitisha: matamshi ya kibaguzi na ya uchochezi dhidi ya jamii ya Warumi. Huenda ukawa mbaya zaidi wakati wa uchaguzi ujao wa ubunge na wa manispaa barani Ulaya.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.