Global Voices Yasaidia Wahanga wa Haiyan Nchini Ufilipino

Typhoon Haiyan,moja ya kimbunga chenye nguvu sana kuwa kutokea katika historia, kimeshaua maelfu ya watu nchini Ufilipino.

Kwa mujibu wa waandishi wetu nchini humo watu wengi zaidi wamejikuta katika makazi yasiyokuwa na chochote, huku wakipata shida kubwa, hawana chakula, maji wala msaada. Kwa ujumla, misaada haiwafikii kwa muda muafaka watu hawa waliosalimika katika kimbunga Haiyan, kinachojulika kwa jina maarufu, Yolanda.

Wiki moja mara baada ya kutokea kwa kimbunga kikubwa katika majimbo ya Leyte na Samar, katika visiwa vya Visayas, tutakuwa tunawasiliana na waandishi wetu wa habari walioko Ufilipino pamoja na mfanyakazi anayehusika na usambazaji wa misaada kuhusiana na namna Ufilipino inavyokabiliana na janga hili, maendeleo ya harakati za uokoaji na jinsi jamii ya kimataifa inavyoweza kutoa msaada.

Mhariri wetu wa Kaskazini Mashariki mwa bara la Asia, Mong Palatino (@mongster) aungana nasi kutokea Manila, pamoja na mwanaharakati na mwandishi wa picha za video, Chantal Eco @chantaleco, ambaye anaratibu juhudi za utoaji misaada huko Manila katika jimbo la Leyte alipokulia.

Pia, tembelea ukurasa wetu maalum kuhusiana na Kimbunga Haiyan, Haiyan yaharibu Ufilipino.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.