“Nchi” Nzuri ya Afrika

Katika toleo la wikii hii la Brainstorm, jarida la mtandaoni la Kikenya, Brenda Wambui hulaani masimulizi ya sasa kuhusu Afrika: “Afrika ni nchi”, “Afrika inapaa”, ‘”Mitindo ya Kiafrika.” Huchunguza jinsi Wakenya wanavyoweza kukomboa simulizi lao na kujiainisha kwa kuweka masharti yao wenyewe:

Kama wenyeji wa Kenya ama nchi nyingine ile, tunafaa kujiainisha, kueleza msimamo wetu, kueleza tunayotarajia kutoka kwa nchi zingine tunazoshirikiana nazo, na kutaja yale tutakayokubali na yale ambayo hatutayakubali. Tunafaa kuunda utambulisho usiotegemea matarajio na dhana za wengine, kisha kuuegemeza. Kujitambulisha kwa maneno pekee yao hakutoshi, lazima ujitambulishe kwa vitendo vyako pia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.