PICHA: Mafuriko Makubwa Katika Mji Mkuu wa Ufilipino

Makala haya yalichelewa kuchapishwa kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Yalipaswa kuchapwa mwezi Agosti 26, 2013.

Dhoruba kubwa ya kitropiki ya Maring ilisababisha mafuriko makubwa kuwahi kutokea katika Metro Manila na mikoa ya jirani nchini Ufilipino ambayo ilisababisha vifo vya watu 8, majeruhi 41, na 4 wakiwa hawajulikani walipo.

Kulingana na ripoti ya serikali, familia 125,348 zenye watu 602,442 ziliathirika na dhoruba hiyo. Kufikia Agosti 20 jioni, watu 40,837 bado walikuwa wamehifadhiwa katika vituo 198 vya uokoaji. Mafuriko yalifanya barabara kuu 65 kutopitika. Jumla ya maeneo 415 katika manispaa/miji 68 zilirekodi visa vya mafuriko. Idadi ya ndege 162 (59 ya kimataifa na 103 za ndani) kubatilishwa kutokana na dhoruba.

Wafilipino walitumia alama habari #maringPH na #floodPH kufuatilia hali ya mafuriko katika Manila na mikoa ya jirani. Zifuatazo ni baadhi ya picha kwenye mtandao wa Twita na Facebook ambazo zaonyesha kiwango cha maafa ya mafuriko.

Image from World Vision

Picha kutoka kwa shirika la World Vision

A flooded village south of Manila. Photo from @erwinlouis

Mafuriko katika kijiji kusini mwa Manila. Picha kwa hisani ya @erwinlouis

Flood in Marikina, east of Manila. Photo from Facebook page of Prospero De Vera

Mafuriko jijini Marikina, mashariki ya Manila. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Prospero De Vera

Photo by YouScooper Jefferson Levie, from Facebook page of GMA News

Picha kwa hisani ya YouScooper Jefferson Levie, kutoka ukurasa wa Facebook wa GMA Habari

A flooded university in Manila. Photo by Salina Teo, from the Facebook page of TomasinoWeb!

Mafuriko katika chuo kikuu jijini Manila. Picha kwa hisani ya Salina Teo, kutoka ukurasa wa Facebook wa TomasinoWeb!

Knee-deep flood in Manila. Photo by Jam Sisante

Mafuriko kufikia urefu wa goti jijini Manila. Picha kwa hisani ya Jam Sisante

Flood near the country's main business district. Photo by @siao88

Mafuriko karibu na wilaya ya nchi ya biashara kuu. Picha kwa hisani ya @siao88

Flood near Manila City Hall. Photo by Manila Bulletin

Mafuriko karibu na Ukumbi wa mji wa Manilla. Picha kwa hisani ya Manila Bulletin

Flood in Guagua, north of Manila. Photo from Facebook page of The College Mirror

Mafuriko katika Guagua, kaskazini ya Manila. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa The College Mirror

Flood in the old downtown of Manila. Photo by Philippine Star

Mafuriko katika jiji la zamani la Manila. Picha kwa hisani ya Philippine Star

Flood in Makati, the country's central business district. Photo by Ryan Chua

Mafuriko jijini Makati, wilaya ya nchi ya kati ya biashara. Picha kwa hisani ya Ryan Chua

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.