China Yawaamrisha Vijana Kuwatembelea Wazazi Wao

Wiki hii China imeanza kutumia sheria mpya inayowataka watoto waliokwishafikia umri wa kujitegemea kuwatembelea wazazi wao “mara kwa mara”.

Ni utaratibu wa lazima kabisa kwa nchi ya China kuheshimiwa watu wazima na kuwatunza wazazi kwa kadiri ya umri wao unavyosogea, lakini aina mpya ya maisha imewalazimu vijana wadogo huondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha yao. Sheria mpya inawataka vijana kujali “mahitaji ya kiroho” na “kutowapuuza wazee” lakini sheria hii haijaweka bayana ni mara ngapi vijana wanapaswa kuwatembelea wazazi wao au ni adhabu gani watakabiliana nayo endapo watashindwa kuitii sheria hii.

Sheria hii imeanzishwa kufuatia idadi kubwa ya watu wa China kuonekana kuwa na umri mkubwa na hii inatokana na sera ya kuzaa mtoto mmoja tu. The journal liliripoti kuwa, zaidi ya asilimia 14 ya watu wa China ambao ni watu milioni 194 wana umri wa zaidi ya miaka 60, hii ni kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni za Shirika la Taifa la Takwimu. Hadi mwaka 2030, ididi hii itakuwa mara dufu.

Kwa nyongeza, tangu mwaka 2012, mfumo wa malipo ya uzeeni wa China umekuwa katika mgogoro kwani umekabiliwa na upungufu wa kiasi cha fedha cha Dola za Marekani trilioni 2.9. Vijana wadogo wa China wana mashaka kuwa, wanalazimishwa kuisaidia katika kuwatunza wastaafu wa serikali.

Katika tovuti ya jukwaa maarufu la kublogu la nchini China, Sina Weibo, sheria hii mpya imeonekana kudhihakiwa ambapo wengi wanakejeli kwa kusema kuwa utekelezaji wa sheria hii una walakini kwani kuwatembelea wazazi lilipaswa kuwa jambo la kijamii lililohitaji uhamasishaji wa kawaida badala ya kushurutishwa kwa sheria. Baadhi ya watu walilalama kuwa, hawawezi kupata muda wa kutosha kutoka kazini na kwenda kuwatembelea wazazi wao hata kama wangekuwa tayari kufanya hivyo, wakati wengine wanafikiri kuwa, sheria hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuimarisha hali mbaya iliyopo ya mfumo wa posho ya uzeeni nchini China.

Mtumiaji wa mtandao wa intaneti “Zhuomo Xiansheng” aliandika [zh] kwa kejeli:

Photo from Sina Weibo

picha kutoka Sina Weibo

亲情本是人性,列入法律着实让人觉得可笑,就跟要求婚后夫妻要性生活和谐一样。

Ukaribu wa Kifamilia unapaswa kuwa ni wa hisia za hiari. Ni jambo la ajabu kulifanya kuwa sehemu ya sheria, yaani ni kama kuwaomba wapenzi waishi maisha ya kimahusiano ya usawa mara baada ya kuoana.

Mwanaasheria Yang Lei alisisitiza [zh] mtazamo uliotangulia kusemwa:

重点在于这法律怎么落实,比如说给老人家里弄个指纹考勤机让孩子打卡?

Swali ni kuwa, sheria hii itasimamiwa vipi? Kwa mfano, wazazi watapewa kifaa cha kutambua alama za vidole? blockquote>
“Yu linfeng” alihisi[zh] kuwa China kukosa usimamizi mzuri wa mambo ya kijamii ni moja ya sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa sheria hii:

社保基本只能保障公务员,大部分普通老百姓都将老无所依

Hifadhi ya jamii ipo zaidi kwa wafanyakazi wa umma, watu wengi wa kawaida hawana kiinua mgongo wanachoweza kukitegemea.

Mtangazaji wa Runinga, Cao Baoying anafikiri [zh] kuwa sheria hii imeanzishwa kama namna ya serikali ya kukwepa wajibu wake:

法律不能片面强调公民义务,而弱化政府职责。

Kwa kuanzisha sheria hii, serikali inasisitiza uwajibikaji wa upande mmoja, yaani jukumu la wananchi, lakini kwa upande mwingine inadumaza majukumu ya serikali.

Sehemu ya maoni ya ifeng newskilihitimisha [zh]:

立法推行孝道,固然有强制子女的效用存在,但若强大的外在压力无法减轻,这种无奈的“孝道”究竟有多少真情实意?而法律的尊严又能剩下多少?

Kuanzishwa kwa sheria hii inayolenga kuhamasisha watoto kuwatii wazazi wao inaweza kuwa muafaka katika kuwalazimisha watoto kuwatembelea wazazi wao, lakini kama hawatasaidiwa katikakukabiliana na changamoto nyingine wanazokabiliana nazo, sheria hii ya “watoto kuwatii wazazi wao” itakuwa na msaada gani? Ni kwa jinsi gani tunapaswa kuona umuhimu wa sheria hii?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.