Simulizi la Video [IsiyoHalisi] ya Kukamatwa kwa Morsi

Video inayoonyesha kile kinachoelezwa kuwa kukamatwa kwa rais wa zamani za Misri Mohamed Morsi inatembea sana mtandaoni hivi sasa. Video hiyo hiyo iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube mnamo Mei 21, 2013 kwa kichwa cha habari “Wakati Rais Mohamed Morsi na mwanae walipokamatwa.”

Morsi ameng'olewa/a> leo [Julai 4] na jeshi la Misri baada ya kutumika kama rais kwa mwaka mmoja. Mamilioni walikusanyika Misri yote tangu Juni 30, siku ambayo ndio kwanza alikuwa ametimiza mwaka mmoja tangu awe madarakani, wakimtaka yeye —na chama chake cha Muslim Brotherhood — waondoke madarakani. Leo, jeshi la Misri lilimtaja rais wa mpito, wakiisimamisha katiba (aliyoipitisha rais Morsi) na kuahidi kuwa uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika mapema.
Video hiyo, yenye jina la “Kwenye Video, Kukamatwa kwa Morsi”, iliwekwa kwenye
mtandao wa YouTube na inaanza na majibizano baina ya watu [ar] wakisema kwamba “ni lazima afungwe pingu na kufanyiwa kama wanavyofanyiwa wahalifu wengine.”
http://www.youtube.com/watch?v=xyt6r0qr7xY

Video hii, na kwa kuzingatia kutolewa kwake kuligongana na taarifa kwamba Morsi alikuwa amezuiwa nyumbani kwake, iliwachanganya wengi.

Iyad El-Baghdadi anabainisha:

@iyad_elbaghdadi: Video inayodaiwa kuwa ya kukamatwa kwa #Morsi. Kuna mtu anarudia rudia kusema “atoke akiwa na pingu”. http://bit.ly/12mCD28 #Egypt

Anaongeza:

@iyad_elbaghdadi: Sielewi mukhtadha wa video hii ya kukamatwa kwa #Morsi. Maafisa kadhaa wa jeshi, lakini hawa raia wanafanya nini pale? http://bit.ly/12mCD28 #Egypt

Mwandishi wa habari Jenan Moussa awali alituma kiungo cha video kwenye mtandao wa twita na baadae kukiondoa. Anaeleza:

@jenanmoussa: Ninaifuta video ya kinachodaiwa kuwa kukamatwa kwa Morsi. Sijathibitisha hata kidogo. Samahani.

Na mtumiaji aitwaye Egyptocracy anatwiti:

@Egyptocracy: Kuna video ya uongo inayosambaa sasa hivi ya kile kinachodaiwa “kukamatwa kwa Morsi”, hajakamatwa, alikuwa chini ya ulinzi wa nchi hiyo.#Misri

Wakati huo huo, Mwandishi wa habari anayeishi Cairo Amira Howeidy anabainisha:

@amirahoweidy: Morsi yuko chini ya ulinzi nyumbani kwake. Hakuna hata kiongozi mmoja wa chama cha Muslim Brotherhood amepatikana. Vituo vyote vya televisheni vimefungwa. Waislamu wenye msimamo mkali wamenyamazishwa. Nini kinafuata?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.