Kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa Kimasedonia Kwachochea Maandamano

"Who's next for Liquidation?" - a poster at today's journalist protest in Skopje, referring to the official code name of the operation ("Liquidation"), in which journalist Tomislav Kezarovski was captured on May 28. Photo by Biserka Velkovska/@bvelkovska, used with permission.

“Nani anayefuata kufilisiwa?” – bango katika maandamano ya leo ya wandishi wa habari mjini Skopje, akimaanisha jina la kificho kwa mpango unaoendelea (“Kufilisi”), ambapo mwandishi wa habari Kezarovski Tomislav alikamatwa pamoja na watu wengine mnamo Mei 28. Picha kwa hisani ya Biserka Velkovska/@bvelkovska, imetumiwa kwa ruhusa.

Waandishi wa habari wa Kimasedonia walikusanyika [tazama video na soma nakala] mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai hivi leo katika mji mkuu Skopje kupinga kukamatwa kwa mwenzao, Tomislav Kezarovski, kwa mujibu wa maandishi haya [en] yaliyoandikwa katika ukurasa wa kundi la Kimasedonia kwenye mtandao wa Facebook yaliyopewa kichwa cha habari cha “Waandishi wa habari na wananchi katika kutetea haki ya uhuru wa habari.” Inaonekana kwamba sababu rasmi ya kutiwa kizuizini kwa Kezarovski kwa siku 30 ni habari aliyoiandika miaka mitano iliyopita kwa ajili ya jarida ambalo  halipo tena. Kwa upande mwingine, amekuwa akichunguza kifo cha Nikola Mladenov, mchapishaji na mhariri wa kampuni huru ya habari, kwa miezi miwili iliyopita.

Ingawa sababu rasmi ya kifo  cha Mladenov ni “ajali ya barabarani,” mengi hayajulikani katika tukio hilo. Kezarovski aliandika makala [mk] kuhusu masaa ya mwisho mwisho ya Mladenov, akitumia ushahidi uliogunduliwa na waandishi wa gazeti la kila siku liitwalo Nova Makedonija, kubainisha kuwa baada ya polisi kuondoka katika eneo hilo la tukio lililokuwa linalindwa isivyo kawaida, ushahidi mwingi uliachwa huko, ikiwa ni pamoja na risiti ya kulipa ushuru wa maegesho na sehemu za gari hilo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.