China Yadhibiti Habari za Maandamano Yakupinga Kujenga Kiwanda cha Kemikali

Wakazi wa jiji la kusini magharibi mwa China liitwalo Kunming waliingia mtaani mnamo Mei 4, 2013 kupinga mpango wa kuzalisha kemikali zenye sumu karibu na makazi yao.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, Shirika la Taifa la Mafuta la nchi hiyo lina mpango wa kujenga kiwanda cha tindikali katika mji jirani wa Anning kuzalisha tani 500,000 za sumu ya paraxylene (PX) inayotumika kutengenezea nyuzi. Takribani watu 3,000 walikusanyika katikati ya mji kupinga hatari inayowezekana kutokana na sumu ya PX.

Vyombo vya Habari vya serikali havikutangaza habari za maandamano hayo, na katika hali ya kushangaza wafuatiliaji wa mtandaoni wamefuta habari na picha zinazohusiana na maandamano hayo kwenye mtandao maarufu wa kijamii uitwao Sina Weibo tangu Mei 4, 2013. Watumiaji wengi wa mtandao wa intaneti waliamua kutumia picha ya “Kunming PX” kama utambulisho wao mtandaoni huku ikiwa imewekwa alama ya X kuonyesha kupinga mpango huo.

Kunming inafahamika sana kwa biashara ya maua na mimea kwa sababu ya hali nzuri ya hewa eneo hilo kwa mwaka mzima. Ni moja ya majiji machache ya China ambamo anga angavu lenye rangi ya bluu huonekana mara nyingi.

Maandamano kama hayo yalilipuka kwenye miji mingine katika miaka ya hivi karibuni. Mwaka 2007, maelfu ya watu waishio kwenye jiji Xiamen lililoko mashariki mwa China walipinga kujengwa kwa kiwanda kama hicho. Katika miaka miwili, maandamano makubwa mawili yalilipuka hukoDalian and Ningbo.

Protesters wore symbolic masks and brandished posters warning against the dangers of a paraxylene (PX) spill.(From Sina Weibo)

Waandamanaji walivaa picha kwenye nyuso zao pamoja na mabango yenye ujumbe wa kuonya kuhusu hatari ya paraxylene (PX). (Imetoka kwenye tovuti yaSina Weibo)

Mtumiaji mmoja wa mtandao huo wa Weibo “Boluocun Yihao” anayeishi Kunming alitoa wito wa [zh] uungwaji mkono zaidi mtandaoni:

媒体被控制,手机信号被切断,保卫人民生命安全的警察却没有保卫,"XX石化炼油厂,滚出昆明!"我们不要牛奶河,我们不要PM2.5,我们不要PX。希望大家可以接力转载,转发。保护我们的母亲昆明。

Vyombo vyote vya habari vimedhibitiwa, mtandao kwenye simu za kiganjani umekatwa, polisi waliopaswa kuhakikisha usalama wa raia hawakutimiza wajibu wao wa ulinzi, “Tunapinga kabisa kiwanda cha tindikali hizi, ondoeni viwanda hivi Kunming!” Hatutaki mito itakayoeuka kuwa rangi ya maziwa[mto ulioathirika na uchafuzi wa mazingira umebadilika tangi na kuwa maziwa], hatutaki PM2.5 [kemikali ya uharibifu wa mazingira], hatutaki kemikali ya PX. Tafadhali chapisha tena ujumbe huu. Tuulinde mji wetu wa Kunming.

Mtumiaji mwingine wa Weibo anayeisha Kunming alikosoa vikali [zh] hatua ya kudhibiti vyombo vya habari:

那么大一个中国,只有《北京晚报》一家如实报道了昆明昨天发生的事。而且还不是亲自采访的,是引用网易的。据说中新社的采访了昨天的事,但是最后没能发表。新华社,央视更是能躲则躲…..中国已经没有媒体能为百姓说话了,同意的速转.

Nchi kubwa kama hii, eti chaneli moja tu ya “Beijing Evening News” ndiyo iliripoti kwa ukweli kile kilichotokea Kunming jana. Haikuwa taarifa yao wenyewe bali walinukuu kutoka mtandao wa NetEase. Inasemekana Shirika la Habari la China lilifanya mahojiano jana, lakini mwishoni lilizuiwa kutangaza habari hizo. Shirika la Habari la Xinhua na lile la CCTV yamejaribu kujificha mbali kabisa na habari hizi kadri wanavyoweza. China kwa sasa haina chombo cha habari cha kuwasemea watu. Tafadhali chapisha tena ujumbe huu kama unakubaliana na hili.

Mwanamuziki kutoka Kunming “Yinyue Xiaosun” alionyesha tena [zh] hisia zilezile:

Sign reads: "Beatiful Kunming! We need to survive! We want to be healthy! PX—out of Kuming !"

Bango linasomeka: “Kunming Nzuri! Tunahitaji kuendelea kuishi! Tunahitaji kubaki na afya zetu! PX-iondoke nje ya Kunming !” (Imetoka kwenye mtandao wa Sina Weibo)

各位昆明的媒体朋友,我理解你们的工作,就像我们理解今天的警察哥哥,警察叔叔,警察姐姐一样。但是,你们都生活在昆明,都爱自己家乡,都希望自己的孩子呼吸新鲜的空气,不是吗??不是吗?不是吗?

Marafiki wa Vyombo vya Habari jijini Kunming, ninaelewa vyema kazi mnayoifanya, kama tunavyowaelewa polisi wetu wa leo. Lakini ninyi mnaishi Kunming. Sote tunaupenda mji tulimozaliwa na tunataka watoto wetu wavute hewa safi, au sivyo?

Mtumiaji mwingine wa (mtandao wa)Weibo “Kong Batian” alikumbuka [zh] Tamko la Dunia la Biashara ya Maua jijini Kunming mwaka 1999:

14年前的今天,在“人与自然,和谐发展——共同迈向21世纪”的口号下,昆明人满怀激动与自豪迎来了中国第一个世博会!而14年后的今天,云南人竟然要为了自己的生存环境走上街头进行抗争!这真是对昆明人民莫大的讽刺!

Miaka 14 iliyopita, kwa kutumia kauli mbiu ya “mtu na mazingira, kuelekea karne ya 21″, watu wa Kunming walijivunia na kuhamasika katika Tamko la kwanza la Dunia nchini China! Miaka 14 baadae, watu wa Yunnan imebidi waingie mitaani kupambana kulinda mazingira yao! Huu ni ushupavu mkubwa kwa watu wa Kunming!

Watumiaji wengine wa Weibo walinukuu [zh] utenzi uliandikwa na mwandishi mashuhuri aitwaye Bai Yansong:

Sign reads " Uncle and aunt, we need clean air!"

Bango linasomeka “Mjomba na Shangazi, tunahitaji hewa salama!” (Kutoka kwenye mtandao wa Sina Weibo)

用不了多久,这座城市将慢慢退出人们的视线,沦为历史的鸡肋,美丽的传说将永远成为传说,没有人会对此负责,应该对此负责的人早已离开了这个城市,甚至这个国家,他们的子女早已远居海外,留下的只是一个破烂污染的废城,一方癌症的区域,一群朴实、愚昧的人民, 这个城市叫作昆明。

Si muda mrefu jiji hili taratibu litafutika kwenye historia ya dunia. Alama nzuri ya historia huendelea kuwa kuwa alama nzuri. Hakuna atakayewajibishwa kwa sababu wale ambao wangefanya hivyo tayari wameshalihama jiji hili, na watoto wao wamehama, na hata watoto wao pia wameshaondoka, wakiliacha jiji lilijaa watu walioathirika vibaya na uchafuzi wa mazingira, eneo lenye magonjwa ya kansa…jiji hili linaitwa Kunming.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.