Mwanaharakati wa Pakistani Khudi Ali Auawa Katika Mlipuko wa Bomu

Mnamo Januari 10, 2013 katika jiji la Quetta lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Pakistani, watu 82 walipoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu yaliyolenga eneo ambalo kimsingi lina idadi kubwa ya watu wa jamii ya Waislamu wa Shia jamii ya Hazara.

Irfan Khudi Ali, mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu ambaye bila kuchoka aliweka wazi uonevu wa kikabila unaofanywa kwa waShia wa Hazara nchini Pakistan, alifariki katika shambulio lililofuata.

Vigil for @khudiali in Islamabad. Picture by @ali_abbas_zaidi

Kukesha kwa ajili ya @khudiali nchini Islamabad. Picha na @ali_abbas_zaidi

Katika ukurasa wa Twita, Ali alitaarifu kuwa, aliponea chupuchupu kwenye tukio la mlipuko mabomu wa kwanza huko Quetta:

@khudiali : #Quetta, nilikuwa ninaelekea nyumbani na ndipo nikaponea chupuchupu kwenye mlipuko wa bomu lililoua watu 11.

Maria Memon alitwiti:

Ali hakuweza kuepuka kwenye mlipuko wa pili wa mabomu. Pumzika kwa amani. @khudiali RT @khudiali #Quetta, alikuwa akielekea nyumbani na aliponea chupuchupu kwenye mlipuko wa mabomu ulioua watu 11

Kifo chake kimeamsha heshima ya juhudi zake na kupelekea kuamsha tena maandamano kuhusu mauaji ya watu wa Shia nchini Pakistani. Mara ya mwisho Ali alipoTwiti alituma taarifa kutoka katika eneo la machafuko iliyoelezea kuhama kwa watu wa jamii ya Hazara kulikotokana na unyanyasaji wa kiitikadi:

@khudiali #Familia za Hazara za #Machh,Khuzdir hatimaye imejikuta kwenye hali tete ya mauaji ya halaikifinally succumbed to the genocidal pressure&moving out. Siku mbaya itokanayo na utofauti wa asili #Balochistan.

Irfan Ali during a protest against sectarian violence in Islamabad, September 2012. FRom the Facebook page of Pakistan Youth Alliance.

Irfan Ali wakati wa maandamano ya kupinga vurugu za kidini huko Islamabad mnamo Septemba 2012. Kutoka katika ukurasa wa Facebook wa Umoja wa Vijana wa Pakistan.

Tangu mwaka 2001, waislam wa Shia wa Hazara kutoka Quetta – kwa kawaida wamekuwa wakitafutwa na makundi ya kijeshi. wakiwa kama kundi la watu wachache miongoni mwa kundi la watu wa tabaka la chini, mauaji ya Hazara Shia ni miongoni mwa matukio ya kikatili yasiyotolewa taarifa kabisa nchini Pakistan.

Hazara.net inaonesha takwimu za kumbukumbu ya mauaji ya watu wa Hazara ya Shiite nchini Pakistan, ikijumuisha idadi ya mashambulizi na idadi ya watu waliouawa hasi sasa. Kwa mjibu wa takwimu katika katika tovuti hiyo, jumla ya watu 1100 wa jamii ya Hazara Shiite wameshauliwa nchini Pakistan tangu mwaka 1999.

Vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikikabiliana na changamoto pale vinaposhindwa kuweka bayana kiini cha mashambulizi, na wnapofanya hivyo, wanalaumiwa kutumia ‘udhehebu’ pale dhehebu fulani linaposhambuliwa. Katika juhudi za kupigia kelele na kuongeza nguvu kwa mashirika ya kuhakikisha sheria zinasimamiwa pamoja na serikali, kumekuwa na mjadala endelevu katika vyombo vya habari vya kiraia kufuatia mauaji ya kukusudia yanayoelekezwa kwa watu wa Shiite, mjadala unaoendeshwa kupitia viungo ishara #mauaji ya Shia na #mauaji ya kimbari ya shia katika Twita. Kwa kipindi kilichopita, wanaharakati wa Shia, walitumia mitandao ya kijamii ili kupata kuungwa mkono na vyombo ya habari vya kimataifa ili habari zao ziweze kutangazwa.

Mwandishi wa habari anayeheshimika sana, Mohammad Hanif anaandika:

Mwanablogu Omar Biden, aliandika makala fupi ya heshima kuhusu Irfan Khudi Ali katika blogu yake:

Jana ilikuwa ni miongoni mwa siku nyingi za umwagaji damu kwa mji mkuu wa Balochistan ambao ni, Quetta. Mapema asubuhi ya leo, wakazi wa jiji wametoka kusikia sauti ya mlipuko wa mabomu ambayo yalitegwa kwenye gari la mgambo wanaolinda mpakani huko Bacha Khan Chowk. Mlipuko huo ulipelekea watu 12 wasio na hatia kuuawa. Kwa hakika, ilisababishaIndeed, it created helter-skelter kati ya wakazi kuzika miili ya watu waliofariki.

Bado, kanuni ya zaidi-halafu-itoshe haitumiki nchini Pakistani, angalao siyo huko Quetta. Baada ya masaa machache, barabara ya Almadar, makazi muhimu ya watu wa Shia Hazara, ilishuhudiwa mauaji makubwa ya kinyama, na tena kwa kutumia mbinu ileile iliyotumika kwenye mlipuko wa asubuhi. Hata hivyo, hii “Mardanawar”, lililotegwa kwa muda maalum, kwa ujasiri kabisa, mlipuko pacha uliosababisha uharibifu usiosahaulika (…)

Matukio ya kikatili yamegharimu idadi kubwa ya watu kwa hakika. Hali iliyopelekea pia kifo cha rafiki aliyekubalika, mwanaharakati wa haki za binadamu–Irfan Ali Khudi.

Kama inavyodaiwa, Irfan Ali Khudi mwenye umri wa miaka 33, alifika Quetta ili aweze “kutoa mafunzo kwa wanaharakati wanaochipukia”.

Pamoja na kuwa nililenga kuandika mawazo yangu, ninaiacha makala hii bila kuimalizia…

Siku ya damu Quetta, kama Omar anavyoiita, siyo ya kwanza ya aina yake na inaweza isiwe ya mwisho. Hali ya kutokuwa na maelewano imewakasirisha wengi, haswa hswa tokea kikundi cha kijeshi kilipofutwa, Lashkar-e-Jhangvi, waliotangaza kuhusika na mashambulizi, bado hawajakamatwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.