Bangladeshi: Msichana Mwingine Mzawa Abakwa na Kisha Kuuliwa.

Kwa mara nyingine tena msichana mzawa ameuliwa mara baada ya kufanyiwa ukatili kwa kubakwa katika kijiji cha Borodalupara, Kawkhali Upazila ya wilaya ya Rangamati. Khomaching Marma (14) ambaye ni mhanga wa kitendo hiki, alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la nane. Mwili wake ulikutwa katika miteremko ya milima takribani yadi 200 hadi 300 kutoka nyumbani kwake. Mara ya mwisho alionekana akielekea kwenye msitu wa karibu na nyumbani kwake kuchukua mifugo ya familia yake kutoka malishoni.

Rina Dewan aliandika katika ukurasa wake wa Facebook [bn] akieleza sababu za kufanyika kwa kitendo hiki cha kikatili:

Kuna mlowezi mmoja katika kijiji ajulikanaye kwa jina la Nallyachari Uttor Matha aishie takribani umbali wa nusu ya kilometa kutoka sehemu ilipokutwa maiti ya Thomaching. Kwenye miaka ya 1980 hivi, serikali iliwaondoa wakazi wazawa wajulikanao kama Marmas kutoka kwenye ardhi yao na kisha kuwakaribisha watu wa Kutoka Bengali. Kwa sasa wahamiaji hao wanataka kujimilikisha sehemu kubwa ya Borodalupara. Siku chache zilizopita, baadhi ya wanavijiji wa Marma walipanda tangawizi kwenye mashamba yao lakini wahamiaji hao waliharibu mazao yao na kusababisha hali ya amani kupotea. Imekwishafahamika kuwa kuna mgogoro wa ardhi uliopo kati ya mjomba wa Thomaching Marma na wahamiaji wa Bengali. Kwa hiyo, inadhaniwa kuwa alibakwa na kisha kuuliwa kama namna ya kulipiza kisasi.

Violence against indigenous women has increased in recent times. Image by A M Ahad. Haki miliki Demotrix.

Uonevu dhidi ya wanawake wazawa umeongezeka siku za hivi karibuni. Picha na A M Ahad. Haki miliki Demotrix.

Ukatili dhidi ya wanawake wazawa umeongezeka siku za hivi karibuni. Miezi michache iliyopita, msichana mwingine alibakwa na kisha kuuliwa.Alikuwa ni mwanafunzi wa darasa la tano. Mwandishi wa habari Hari kishore Chakma, anatoa baadhi ya takwimu zinazoonesha matukio ya kubakwa kwa wanawake wazawa katika makala ya gazeti la kila siku la Prothom Alo [bn]:

Mpaka mwezi wa Novemba mwaka jana, wasichana na wanawake 20 wazawa walibakwa katika wilaya tatu za mlimani. Na kwa sasa, jina la Thomaching Marma linajumuishwa kwenye orodha hii inayoendelea kukua. Mwaka 2011, wanawake 10 wazawa walibakwa. Kapaeng ambalo ni shirika la kutetea haki za binadamu lilitoa takwimu hizi. Kwa mujibu wa shirika hili, wanawake wazawa 51 walikuwa wahanga wa matukio haya kwa mwaka huu. Mwaka 2011 matukio kama haya yalikuwa 31 na manne tu mwaka 2008.

Ukatili huu wa ubakaji na mauaji kwa mara nyingine tena umeshaeneza hasira na vurugu nchini kote. Mazungumzo yalikwisha kupangwa katika miji ya Dhaka, Chittagong na Sylhet. Raia wa mtandaoni nao wameshaonesha hasira yao na pia kuandamana.

Maandamano huko Dhaka ya kupinga ubakaji na mauaji ya msichana mzawa. Picha na Firoz Ahmed. Haki miliki Demotix

Mithun Chakma Jummo aliandika katika ukurasa wake wa Facebook:

Kama tu jinsi ilivyo kwa mwili baridi wa dada yetu usioweza kufanya lolote, je, nasi pia tumekuwa hivyo? India waliandamana vikali kabisa kupinga ubakaji wa magenge. Mjini Imphal , watu walipaza sauti zao ili kutafuta haki dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia wa msichana. Maandamano yetu yawe kwa lengo gani? Kwa jambo moja tu? Halafu tuwe kimya na tuliopooza tena!

Adivasi Aodhikar Andolon (CHT) aliandika:

Kwenye habari, niliona India wakinguruma katika maandamano wakipinga ubakaji katika magenge katika gari la abiria la Delhi. Ilifurahisha kuona umoja wao. Vyombo vya habari pia vipo upande wao. Serikali ya India ililazimishwa kuwatia nguvuni wahusika wa vitendo hivi vya kikatili.

Siku za hivi karibuni, msichana mzawa alibakwa na kisha kuuliwa katika kijiji cha Borodalupara huko Kawkhali upazila katika wilaya ya Rangamati.

Hata hivyo, Polisi wameshindwa hata kumtia nguvuni angalau mhusika mmoja.

Kama ilivyo kwa tukio hili, mamia ya akina dada zetu na mama zetu wazawa wamebaki kuwa wahanga wa kubakwa na mauaji kwa muda mrefu.

Blogger Anik aliandika:

Ukatili huu unanijengea taswira ya Bangladeshi katika akili yangu.Taswira ya wabakaji na wauaji. Ni jambo la kikatili kwa wabakaji na wauaji kufanya ukatili huu katika makazi yetu muda wote. Hakuna uhakika kuwa, miongoni mwao ghafla hawatajisahau na kasha kutoa misimamo yao.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.