Habari za Upotoshaji Kuhusu Afrika Katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa

 Kampeni ya kumkamata #Kony2012 iliyoanzishwa na AZISE ya Watoto Wasioonekana kwa hakika ilibeba mambo yaliyorahisishwa mno kuhusu Afrika. Hii ilisababisha kubuniwa kwa kampeni nyingine #WhatILoveAboutAfrica iliyokusudiwa kurekebisha hitilafu hizo.  

poster for Kony 2012.

Bango la Kampeni ya akamatwe Kony 2012. Kwa matumizi ya umma

Makadirio ya vyombo vya habari yasiyosahihi kuhusu Afrika ni hali iliyozoeleka – hata kama makosa yamekuwa yakipungua kwa miaka michache iliyopita. Tafsiri mbaya ya bara hili inayooneshwa na vyombo vya habari si jambo dogo, kama  Profesa Charles Moumouni anavyoeleza [fr]:

La mauvaise représentation de l’Afrique dans les médias occidentaux n’est ni un
phénomène nouveau, ni un phénomène exceptionnel. Elle fait l’objet de préoccupations depuis les années 1970, notamment dans le cadre des discussions sur le Nouvel ordre mondial de l’information et de la communication (NOMIC). Mais l’image que propagent les médias occidentaux de l'Afrique est d’autant plus préoccupante qu’elle influe négativement sur les efforts de développement de l'Afrique

Picha mbaya ya Afrika inayochorwa katika vyombovya habari vya Magharibi si jambo geni wala la ajabu. Limekuwa suala la mjadala tangu miaka ya 1970, hususani katika mikhtadha ya mijadala kuhusu Utaratibu wa Mawasiliano na Habari katika Dunia Mpya (New World Information and Communication Order, NWICO). Lakini sura ya Afrika ambayo kwa sasa inaendelezwa na vyombo vya habari vya Magharibi ni suala linaleta wasiwasi kwa sababu inaathiri jitihada za maendeleo ya Afrika.

Vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe, hata hivyo, kwa sasa havina kinga dhidi ya ukosoaji wa aina hii. Kuna miradi kadhaa imeibuka, kwa miaka ya hivi karibuni, kusaidia kuboresha umakini wa vyombo vya habari vya Afrika. African Media Initiative (Mradi wa Vyombo vya Habari vya ki-Afrika) na Media Monitoring Africa (Ufuatiaaji wa Vyombo vya Habari Afrika) ni mifano miwili.

Hapa ni muhtasari wa watu maarufu, makosa na kutokuwepo umakini katika habari zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari vya dunia kuhusu Afrika na katika vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe:

Habari za Afrika katika vyombo vya habari vya Afrika

Kanada – RDC:  “Stephen Harper aingia katika moyo wa giza la Afrika”

Kichwa hiki cha habari kilipachikwa kwa makala yaCBC news kuhusu ziara ya waziri mkuu wa Kanada nchini Kongo DRC wakati wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi Zingumzazo Kifaransa  Ingawa kicha kicho cha habari kinarejea kitabu cha Joseph Conrad, Moyo wa Giza, lakini pia kinaamsha picha iliyopitwa na wakati, iliyoanza kwisha ya kuiona Afrika kama bara la lisistarabika na hatari. Makala inaongeza:

Ni nchi ya hovyo katika uso wa dunia.

 

Makala hiyo inaifanya ionekane kuwa waziri mkuu Harper alisitahili kutunukiwa medali kwa uajsiri wake wa kuitembelea Kongo DRC.

Israel – “Waafrika wa Kusini mwa Jangwa la Sahara si wabakaji”

Slate Afrique inaeleza mukhtadha wa asili ya kichwa hiki cha habari [fr]:

Les noirs ne sont pas des violeurs. Tel est le message que veulent faire passer des demandeurs d'asile Africains subsahariens en Israël. Ces derniers sont pointés du doigt par l'opinion publique israélienne à la suite d'un cas de viol très médiatisé, ayant impliqué quatre demandeurs d'asile érythréens en Israël. Pour contrer une stigmatisation des noirs, un centre d'aide aux travailleurs étrangers a aidé des Africains à rédiger des «lettres ouvertes au peuple israélien», rapporte le quotidien israélien Haaretz le 20 mai.

Weusi si wabakaji. Huu ni ujumbe ambao watafuta hifadhi kutoka eneo la Kusini mwa jangwa la Sahara wanataka usikike nchini Israeli. Maoni ya wengi nchini Israeli yanawanyooshea kidole watafuta hifadhi wa Kusini mwa Jangwa la Sahara baada ya kesi iliyotangazwa sana iliyowahusisha wa-Iritrea. Jarida la kila siku la Israeli Haaretz liliripoti mnamo Mei 20 kuwa kupambana na unyanyapaa wa watu weusi, kituo cha kuwasaidia wafanyakazi wa kigeni kimewasaidia Waafrika kuandaa “barua ya wazi kwa watu wa Israeli”.

Ufaransa- Mkanganyiko kati ya Guadeloupe na Madagascar kwa ajili ya I-télé 

Mapambano katika Guadeloupe kati ya Liyannaj Kont Pwofitasyon [zingatia: hiki ni chombo cha wafanyakazi na harakati za kijamii] na majeshi ya ulinzi yalipambana na mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini Madagaska. Matukio mawili yalikuwa karibu sana kwa wakati, kwa ukweli, kuwa I-télé (kituo cha televisheni nchini ufaransa) kilikusanya picha ambazo maelezo yake yanakinzana na matukio ya Guadeloupe na yale ya Madagaska [fr]:

Marekani – Kingo DRC: “Wameachwa yatima, wamebakwa na wamepuuzwa”

Hiki nikichwa cha makala kilichoandikwa na mwandishi Nicholas Kristof kuhusu mtoto wa miaka 9 ambaye alikuwa mhanga wa kubakwa na kundi la watu nchini Kongo DRC. Kama Laura Seay anavyoeleza katika tafsiri ya tovuti ya Slate Afrique, makala hii inaibua masuala kadhaa ya kimaadili [fr]:

Après de violentes polémiques, Kristof posta une réponse sur son blog dans laquelle il promettait de ne pas le refaire, tout en réfutant les critiques affirmant qu’il mettait l’enfant en danger en l’identifiant. Il reconnut cependant qu’imprimer son nom violait la politique du Times, même s’il avait reçu l’autorisation d’une femme qui jouait le rôle de tutrice de l’enfant. Difficile d’imaginer un rédacteur en chef, quel qu’il soit, laisser une telle «bavure» se produire dans un article concernant une victime occidentale de pédophilie.

Baada yamijadala kadhaa ya kulazimisha, Kristof alituma maoni katika blogu yake ambapo aliahidi kutokufanya hivyo tena -baada ya muda mfupi alipinga madai kwamba alimhatarisha mtoto kwa kumtambulisha. Alitambua, hata hivyo, kuwa kuchapisha jina la mtoto kulikiuka sera ya jarida laThe Times, hata kama alipata ruhusa kutoka kwa mwanamke anayebeba jukumu la kumlea mtoto. Ni vigumu kufikiri mhariri mtendaji angeruhusu “blanda” hiyo kuonekana kwenye makala inayohusu mtoto wa kimagharibi aliyeathirika na udhalilishaji.

Vyombo vya Habari vya Afrika

Afrika Kusini – Mhanga wa ubakaji atambulishwa kwa kificho katika  ripoti  ya mwezi Oktoba 

Musa Rikhotso anaripoti kuwa :

habari iliyotokea Sapa ikiwa na kichwa cha habari, “Hukumu yapunguzwa kufuatia kubakwa kwa binti wa kambo” (The Star, la tarehe 10/10/2012, uk.7). Makala inamtaja mwanaume wa Limpopo, ambaye hukumu yake ilipunguzwa kutoka kifungo cha maisha kuwa mwaka mmoja kwa kumbaa bintiye wa kambo mwenye umri wa miaka 15; kwa kufanya hivyo, jarida hilo likishindwa kulinda utambulisho wa wa mhanga wa ubakaji.

 

Senegali – “Wasenegaliwatimuliwa kutoka Ivory Coast”

Wakati mgogoro wa Ivory Coast ukiwa uko katika joto lake, jarida la Walfadjiri-l'Aurore lilikuwa na kichwa cha habari “wa-Senegali wametimuliwa kutoka Ivory Coast wamalaumu [Rais]Wade“:

wade sénégal côte d'ivoire

Ukurasa wa 2 wa gazeti la kila siku la Senegali likiwa na makala kuhusu mgogoro wa Ivory Coast- wazi kwa matumizi ya umma

 

Jarida la Le Post linaeleza kuwa hayo yalikuwa ni makosa [fr] kwa sababu:

justement ces hommes et femmes reprochent au gouvernement de n'avoir pas été “rapatriés” mais bel et bien d'avoir du rentrer par leurs propres moyens.

watu hawa na wanawake waliikosoa serikali kwa sababu hawakufukuzwa bali walitakiwa kurudi nchini mwao kwa njia zao wenyewe.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.