Ujasiriamali,Utamaduni na Mshikamano katika Afrika

Makala haya yamechapishwa kwa kuchelewa kwa sababu za kiufundi.

Tangu mapema miaka ya 2000, ujasiriamali katika bara la Afrika [fr]umeonekana kuwa na taarifa za kukua [fr] kwa kasi kwa shughuli za kulinda uasili. Hata hivyo maendeleo hayo bado hayajaenea katika sekta zote za soko na pia mara nyingi inaonekana kujikita tu katika eneo dogo la viwanda huduma na biashara. Afrika ina viwanda vidogo na vya kati vipatavyo milioni 65 [fr], hata hivyo bado inajikongoja kuendeleza kundi la wajasiriamali wa ndani wa kusimamia viwanda vya kimkakati, hususani mauzo ya mazao ya nje ya mazao ya kilimo, madini, usafiri na sekta ya viwanda vya umma ambapo soko mara nyingi mno hugeuka kuwa ya mameneja wa kigeni.

Hata hivyo shauku ya wawekezaji kwa ajili ya Afrika, ambayo wengi wanaona kama hatua ya kufa na kupona kwa wale wanaotafuta njia mbadala ya masoko yaliyozoeleka ya barani Asia, inaathiri sera za serikali za Afrika ambazo zimejikita katika kuendeleza sekta zao za binafsi. Ripoti ya mwisho [fr] ya Benki ya Dunia inaonyesha kwamba mageuzi yaliyofanywa na serikali nyingi za Kiafrika yameboresha mazingira ya kibiashara katika utawala, fedha na udhibiti.

Kiwanda cha kampuni ya sukari ya Senegal Picha ya Manu25 kutoka Wikipedia chini ya leseni Creative Commons

Wengi wa wasomi na watafiti wamechunguza athari za shughuli za kiutamaduni ili kuelewa masuala ya kiujasiriamali katika Afrika. Utafiti wao uliwasababisha kuzingatia uzito wa maadili ya kitamaduni na kanuni ambazo zilizojikita katika mawazo ya kawaida ya wafanyabiashara wa Afrika ili kutathmini sababu za mafanikio ya wajasiriamali wa Afrika.

Hatua za uchaguzi wa kiuchumi zisizoleta mantiki miongoni mwa wakurugenzi wa mashirika ya biashara ya Afrika yanayokabiliwa na mashinikizo ya ubaguzi wa rangi, au familia zao zilikuwa sehemu muhimu ya utafiti huo.

Masimulizi ya mafanikio ndani ya bara la Afrika- viongozi wajasiriamali wenye mafanikio makubwa kutoka kwenye kipindi cha news21TV na M. Dogui rais wa klabu ya Africagora 


Tunu za Jadi za ki-Afrika zinazokabili uchumi huria  

Kabeya Tshikuku, Profesa katika Taasisi ya Utafiti ya Kiuchumi na Kijamii (IRES) katika Chuo Kikuu cha Kinshasa, anaamini kuwa mantiki ya kibiashara ni kulazimisha watunga sera wa Afrika kufanya maamuzi magumu kati ya tunu za msingi wa ustaarabu wao (mshikamano wa kifamilia, ustawi wa marafiki zao nk) na utawala wa biashara, unaohusishwa na kutafuta faida tu bila ya kujali ubinadamu. Mizizi ya ubepari, utumiaji na ubinafsi,
imekutana na upinzani zaidi katika hisia za Afrika.

Afrika na Waafrika hawana hatia na kosa lolote lenye mwonekano usiowa kimantiki. «Suala la utamaduni” lipo mahali pengine, kwa kadri suala la maendeleo lilivyo. Jambo hili lipo limejikita katika tofauti iliyofanywa na kila utamaduni kati ya «tunu za kuu za ustaarabu” na “tunu wezeshi”. Kwa kulitazama suala hili kwa jicho la kiutamaduni, mifumo hii miwili inashindania utii wa watu na ugawaji wa rasilimali. […] Kuliweka suala hili bayana zaidi, Afrika inaogelea kati ya mifumo miwili ya kiutamaduni inayoshindana, mfumo wa kurudi nyuma kwa kusimamia watu na (mapinduzi?) ya utawala wa mambo. Sababu za kuwepo na hatua husika bado hazijapoteza kabisa mizizi yake katika mfumo uliokuwepo kabla ya kibepari; na bado haijaota mizizi katika mfumo wa kibepari. Mfumo wa zamani wa mshikamano wa maisha bado hujaporomoka; mfumo mpya wa ubinafsi wa kibepari hujamaliza kujongea ndani katika jamii zetu.

 Kuchanganya mshikamano na ukuaji

Ukuaji ulio ongezea Pato la Kuu la mwaka la bara la Afrika kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita unaonyesha kwamba ubepari huu wa kimantiki na kibinafsi umejijenga sawia ingawa si kwa usawa barani humu. Ukuaji huu unajiingiza katika fikra za umma katika ufanisi au mageuzi makubwa yaliyochukuliwa na serikali kukuza sekta binafsi. Utawala wa mashirika na makampuni ndilo limekuwa kiini kikuu kwa jamii ya kibiashara hususani baada ya wimbi la kushtua ya kashfa ya Enron nchini Marekani. Je wajasiriamali wa Afrika wanaweza kujua jinsi ya kuunganisha kanuni falsafa ubuntu za utawala bora na ambao kikundi huja kabla ya mtu binafsi?

Waziri wa zamani wa Viwanda Uwekezaji, na Biashara wa Mali, Amadou Diallo Abdoulaye, alisema kuwa Afrika ni mfano mzuri wa fumbo. Anaeleza kwa Celia D'Almeida katika Jarida la Mali:

Il y a une décennie, l’environnement socio-économique en Afrique était jugé défavorable à la création et au développement de l’entreprise. Dans certains pays, le cadre juridique des affaires n’est pas très incitatif à cause de la faiblesse, voir l’absence, d’accès au crédit, l’accès difficile à l’information sur les opportunités d’affaires, du manque de soutien au jeune entrepreneur (absence d’incubateurs d’entreprises) et de l’insuffisance de main d’œuvre qualifiée pour la gestion de l’entreprise. À tout cela, s’ajoutait le manque de stratégie politique. Mais, depuis quelques années, des pays africains comme le nôtre, ont amorcé d’importantes réformes pour faciliter la création d’entreprise et offrir un climat favorable au développement des entreprises.

Muongo mmoja uliopita, Mazingira ya kijamii na kiuchumi ya ki-Afrika yalionekana kuwa mabaya kwa utengenezeaji na ukuuzaji wa miradi ya biashara. Katika baadhi ya nchi, mfumo wa kisheria kwa ajili ya biashara umetoa motisha kidogo kutokana na udhaifu kama vile ukosefu wa upatikanaji wa mikopo, uhaba wa habari juu ya fursa za biashara, kutokuwepo kwa msaada kwa ajili ya wajasiriamali wadogo (hakuna vituo vya kuuzia biashara) na nguvukazi isiyotosha kwa usimamizi wa kampuni. Kwa haya yote kuna suala la uhaba wa mkakati wa kisiasa. Hata hivyo, hivi karibuni zaidi, nchi za Afrika kama zetu, zimefanya mageuzi makubwa ili kuwezesha kubuni biashara na kutoa mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya biashara.

Nchini Cameroon, posti ya Richard Ewelle katika Blogu ya Kamer inahitimisha [fr] kuhusu utamaduni na ujasiriamali barani Afrika:

Le développement de l’entreprenariat en Afrique passera par la création d’un concept d’entrepreneuriat africain et pas forcément par la copie conforme de ce qui existe à l’étranger. Nous devons associer les bonnes pratiques occidentales en matière de création d’entreprise, au contexte et aux concepts africains. Le concept de l’entrepreneuriat africain sera basé sur la valorisation de la culture africaine mais aussi sur le développement solidaire en mettant en avant l’environnement socio-économique.

Kukua kwa ujasiriamali barani Afrika kutahitaji kubuniwa kwa dhana ya ujasiriamali wa ki-Afrika na si lazima iwe kama ilivyo nje ya nchi. Tunahitaji kuchanganya njia bora katika kubuni makampuni ya muktadha wa ki-Magharibi kwa kutumia mawazo ya ki-Afrika. Dhana ya ujasiriamali Afrika itakuwa na msingi wake katika tunu za utamaduni wa ki-Afrika lakini pia katika kujenga mshikamano unaodumisha mazingira ya kiuchumi na kijamii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.