Venezuela: Ni Chávez Tena kwa Miaka Sita Zaidi

Posti hii imeandika kwa ushirikiano na Jessica Carrillo [es].

Baada ya chaguzi zilizokuwa na changamoto na ushindani mkubwa katika muongo uliopita, Venezuela itaongeza miaka mingine sita kwa utawala wa Hugo Chávez Frías ulioanza mwaka 1999. Idadi ya watu waliokuwa mtandaoni hasa kwenye mitandao ya kijamii, hasusani twita, ilikuwa kubwa sana hasa kabla matokeo rasmi hayajatangazwa.

Zilikuwepo twiti za upande wa wale wanaomwunga mkono Rais, ambazo zilionyesha furaha na kuridhika, wakati wale waliokuwa wanamwunga mkono Hanrique Capriles walionyesha hisia zao za kusikitishwa na matokeo hayo wakati huo huo wakiwa na matumaini kwamba mambo yanaweza kubadilika kwa siku za mbeleni.

Ukichambua hali ya mambo ilivyo, ni dhahiri kwamba sura ya nchi hiyo kukatwa katika vipande viwili iko dhahiri sana kuliko ilivyowahi kuwa kabla ya uchaguzi huu. Kutenganishwa kwa makundi ya kijamii katika nchi limebaki kuwa sehemu ya mwenendo wa jumla wa mambo.

Wafuasi wa Hugo Chávez wakati wa mkutano wa kampeni tarehe 11 June, 2012 jijini Caracas. Picha ya Sergio Alvarez, haki zimehifadhiwa na Demotix.

Adriana (@SombreroRojo) [es] anasema:

@SombreroRojo: Sigan! sigan el discursito de inclusión tipo: tierruos [apelativo despectivo usado contra la gente que vive en los barrios], brutos, analfabetas. Tendremos Chávez como… 30 años mas? sí, facil!

@SombreroRojo [es]: Endeleeni! Endeleeni na sera ya kuwaunganisha watu: tierruos [jina la dhihaka linalotumiwa kuwatania walalahoi wa uswahilini], wachovu, wajinga. Tunaye Chavez kwa …miaka mingine 30? Ndiyo, rahisi!

Wakati huo huo MariAzul (@Mariazul84) [es] anaandika:

@Mariazul84: Asi con desprecio, con asquito, con arrogancia y todo, se tienen que calar que los tierruos les elija el presidente a la “gente nice”.

@Mariazul84 [es]: Namna hiyo, kwa dharau, kwa kinyaa, kwa majigambo na kadhalika, wakubali kuwa walalahoi huchagua rais wa ‘watu wema’.

Mtumiaji wa mtandao wa twita @Racksonador [es] anatoa wito wa kumaliza mijadala ya kishabiki:

@Racksonador: Y dejen de estar diciendo que van a matar a la gente o que los mataran y que se van a ir del país. LISTO SE ACABO #ElcomandanteSeQueda

@Racksonador [es]: Acheni kusema kuwa watu watauawa au kwamba mtauwa na kwamba mtahama nchi. IMEKWISHA! #ElcomandanteSeQueda (The commander is staying)

Kwa upande wa upinzani kuna pongezi kwa Henrique Capriles na timu yake ya kampeni, kukosolewa kwa tabia ya rais kubahatisha fursa, na madai ya ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi zinazoanzia kipindi cha kampeni.

Vivyo hivyo, wengi wanatoa wito kwa wafuasi wenzao wa Henrique Capriles kutafakari matokeo hayo, kuendeleza mapambano, na kufahamu kuwa hata kama ushindi haukupatikana katika uchaguzi huu, viongozi wa upinzani sasa wameonekana kuwa imara hali inayowezesha kuwa na utendaji wa pamoja na uliobora kwa miaka mingi ijayo.

Fedosy Santaella (@Fedosy) [es] anaandika:

@Fedosy: Capriles seguirá sirviendo, yo seguiré escribiendo. Mi país es mi país. No soy menos venezolano, ni soy menos escritor.

@Fedosy [es]: Capriles ataendelea kutumikia nchi hii, nami nitandelea kuandika. Nchi yangu ni nchi yangu. Mimi si m-Venezuela asiye na haki kama wengine, na si mwandishi asiye kama wengine.

Moraima Guanipa (@haticos) [es] anasema:

@haticos: Reconoceré el triunfo de Hugo Rafael Chávez Frías pero jamás aplaudiré la forma ventajista, abusiva y manipuladora con la que se impuso.

@haticos [es]: Nitautambua ushindi wa Hugo Rafael Chávez Frías lakini kamwe sitampongeza mtu huyu aliyepatikana kwa njia za ubabaishaji, matusi, na ubabe.

Mtumiaji @upallove [es], wakati huo huo, anaonyesha kukatishwa tamaa na matokeo ya uchaguzi huu wa Urais na nyingine zilizopita:

@upallove: En Argentina gano Cristina. En México gano Peña Nieto. En Venezuela gano Chavez. En Latino América gano la ignorancia.

@upallove [es]: Cristina [Fernández de Kirchner] alishinda Argentina. Peña Nieto alishinda Mexico. Chávez ameshinda Venezuela. Ujinga umeshinda kwenye bara lote la Amerika ya Kusini.

Andrea (@DynamiteAndre) anazungumzia, kama wengine wengi, wasiwasi wake kwa matumizi ya bunduki wakati wa maadhimisho:

@DynamiteAndre: “¡VIVA CHÁVEZ!” seguido del sonido de muchos tiros seguidos. No, amigo chavista. No vas a poder convencerme de que esto está bien.

@DynamiteAndre: “UISHI MAISHA MAREFU CHÁVEZ!” maneno yakifuatiwa na milio ya risasi. Hapana, rafiki wa chavista [mfuasi wa Chávez]. Hutaweza kunishawishi kwamba hiyo ni sahihi.

Baada ya kupitia mijadala mbalimbali iliyotokea usiku wa uchaguzi, kuna wazo linaonekana kujitokeza kuwa sehemu ya mjadala: hitaji la kutambua kwa pamoja umuhimu wa kumaliza matabaka katika jamii, na hitaji la wadau wote kujichunguza wenyewe. Luis Carlos Díaz (@LuisCarlos) [es] anabainisha hitaji hili ambalo linabaki kuwa matokeo ya uchaguzi:

@LuisCarlos: Empieza la competencia por el reconocimiento del otro

@LuisCarlos [es]: Mashindano ya kuwatambua wengine ndiyo kwanza yanaanza.

Luis Carlos pia anakazia ukweli unaotakiwa kuwa sehemu ya tafakuri za mienendo yote ya kisiasa:

@LuisCarlos: El presidente Chávez gana por cuarta vez una elección presidencial y tendrá un periodo 1999-2019

@LuisCarlos [es]: Rais Chávez ameshinda uchaguzi wa rais kwa mara ya nne na atakuwa na muhula ulioanza 1999 mpaka 2019.

Kutoka upande unaomwunga mkono Chávez, Gabriel López (@GaboVzla) [es] anasema:

@GaboVzla: El triunfo que ya todos conocemos merece tambien profundas reflexiones,que sin duda vendran.Hoy,a celebrar y a fortalecer nuestra democracia

@GaboVzla: Ushindi ambao wote tayari tunaufahamu unahitaji tafakari ya kina, ambayo ni lazima iwepo. Leo, tusherehekee na kuimarisha demokrasia yetu

Maswali mengi yanabaki bila majibu na maoni mengine mengi yatajaza mjadala huo kwa juma hili katika ulimwengu wa blogu nchini Venezuela.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.