Mauritania: Wafanyakazi wa Migodini Wapinga ‘Aina Mpya ya Utumwa’

 

Katika miji ya kaskazini mwa Mauritania ya Zouerat na Nouadhibou kumeshuhudiwa maandamano ya wafanyakazi wasio na ajira za kudumu. Zaidi ya wafanyakazi 2,3oo waliandamana katika mji wa migodi wa Zouret, na kuzorotesha shughuli za uchimbaji madini katika migodi kumi ya Kampuni la Taifa la Madini na Viwanda (SNIM [fr] pamoja na kuvuruga kazi katika maeneo mengine.

Wafanyakazi hawa wanadai nyongeza ya mishahara kwa mujibu wa mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni na SNIM kwa wafanyakazi wake; pia wanadai mafao ya hifadhi ya jamii, pamoja na raia wa Mauritania kupewa kipaumbele katika kazi ikilinganishwa na wafanyakazi wageni wanaotoka mataifa jirani.

Aina mpya ya utumwa

Wafanyakazi hao, wanaojulikana kama ”journalia” kwa lugha ya mitaani, vile vile wamedai kutaka kuingia mkataba wa moja kwa moja na SNIM badala ya makampuni madogomadogo ambayo hulipa asilimia 40 tu ya mshahara wa mfanyakazi wa SNIM,  kitu wanacho wanaona ni sawa na biashara ya binadamu na aina mpya ya utumwa.

Waandamanaji hao pia walitishia kufanya maandamano kutoka Zouerat hadi Nouakchott, sawa na yale yaliyoandaliwa na wanaharakati wa Nouadhibou hivi karibuni. Huko Nouadhibou nako ”journalia” pia wamenaandaa maandamano dhidi ya kile wao wanachokiita biashara ya binadamu. Wafanyakazi wapatao 1,000 wanatishia kusitisha kazi na kushiriki katika mgomo.

Photo of the Journalia Protest in Nouadhibou by Mauritannet blog

                                                                                  Picha ya Maandamano ya Journalia huko Nouadhibou kutoka kwenye blogu ya Mauritannet

The demonstration in Zouerat

Maandamano huko Zouerat

Mauritannet blog [ar] aliandika kuhusu maandamano hayo na unaweza kusoma kuhusu matukio Zouerat katika ukurasa wa Facebook wa Harakati ya Februari, 25:

تعيش مدينة” الزويرات “على وقع اعتصام “الجرنالية” الذي يدخل في أسبوعه الثاني.
هذا الاعتصام وجد تعاطفا كبيرا من سكان الزويرات حيث لم تتوقف المساعدات عن المعتصمين من أجل أن يستمر إعتصامهم.
وكذالك يقوم فنانو المدينة ومداحيها وشعرائها كل ليلة باحياء سهرات من اجل الترفيه عن المعتصمين وحثهم على مواصلة نضالهم من اجل إنتزاع حقوقهم.
وتجد رالاشارة الى أنه في الزويرات يعتصم الان حوالي أكثر من 2300عامل من عمال “الجرنالية” إحتجاجا على مايصفونه بمقاولة البشر ومن.أجل فسخ العقودالموقعة مع الشركات الوسيطة
Maisha katika mji wa Zouerat yamekuwa yakifuata mdundo wa maandamano ya wafanyakazi ambao umeingia katika wiki ya pili sasa. Wakaazi wa Zouerat wameonyesha huruma zao kwa waandamanaji na kufikia hata kuwapa misaada ili kuhakikisha maandamano yanaendelea. Wasanii na washairi wa mji huo wanatumbuiza kila usiku kwa ajili ya kuwachochea waendelee na mapambano yao kwa ya kudai haki zao. Huko Zouerat sasa, zaidi ya wafanyikazi 2,300 wanapinga kile wao wanaita biashara ya binadamu na wanatoa wito wa kusitisha mkataba wao na makampuni madogomadogo

Mwanablogu wa Mauritania Alddedd Wald Al Sheik [ar] pia aliandika juu ya suala hili:

المشكلة تعود إلي دفع الشركة لرواتب مضاعفة أربع مرات إضافة إلي زيادة نسبية لرواتب العمال الرسميين بينما تجاهلت عمال” الجرنالية “وهي حسب النقابيين سابقة خطيرة وقد تؤدي إلي انفجار الوضع داخل الشركة.

Tatizo liko katika ukweli kwamba makampuni haya hulipa wafanyakazi wake walio rasmi kwa mujibu wa sheria mara nne ya mishahara wanaoyowalipa “journalia,” na pia imeongeza mishahara yao wakati ilipuuza madai ya wafanyakazi wa journalia, ambayo kwa mujibu wa vyama vya wafanyakazi, jambo hilo ni hatari na ambalo inaweza kusababisha kutokea kwa milipuko kazini dhidi ya uchumi wa makampuni hayo.

Ahmed Haymoudane [ar]  alikemea kukosekana kwa nia yoyote ya kutatua mgogoro na kampuni inayohusika:

بوادر حل الأزمة لم تبد بعد في الأفق نتيجة ل:
– إصرار شركة “اسنيم” على المواصلة في استغلال العمال الموريتانيين في مشهد يعيد إلى الأذهان قصص استغلال العمال الأفارقة في مزارع قصب السكر في القارة الأمريكية في القرون البائدة؛
– إصرار العمال على المضي قدما في إضرابهم السلمي وعدم الخضوع للضغوط التي تمارسها الشركة ضدهم من خلال تهديدها لهم بتعويضهم بالعمال الأجانب.
– إصرار السلطات على إسكات كل من يصدح مطالبا بحقه في هذا الوطن حتى لا تنتشر عدوى الثورة وتخرج الأوضاع عن سيطرتها.

Hakuna dalili ya ufumbuzi hadi sasa na hii ni kutokana na:

-Msisitizo wa SNIM kuendelea kuwatumia wafanyakazi raia wa Mauritania kwa njia ambayo inaleta kumbukumbu za unyonyaji uliokuwa ukifanywa dhidi ya wafanyakazi Waafika katika mashamba ya miwa katika miongo iliyopita.

-Msisitizo wa wafanyakazi kuendelea na mgomo wao na kutokubali shinikizo linalotumiwa na kampuni dhidi yao na kutishia kuchukukuliwa kwa nafasi zao na wafanyakazi wa kigeni.

-Msisitizo wa mamlaka wa kumnyamazisha mtu yeyote mwenye kuibua sauti yake na kudai haki zake katika nchi ili kuzuia migogoro hiyo isisambae mahali pengine kiasi cha kufikia hatua ya kutodhibitika.

Alddedd Wald Al Sheikh alitwiti pia:

@dedda04: ثورة الحقوق وبوادر التمرد التي تعم ‎‫#موريتانيا‏ تصل إلى عمال الجرنالية.
@dedda04: Haki za mapinduzi na ishara ya uasi uliopo katika Mauritania zimeanza kufikia wafanyakazi wa journalia

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.