Tamko la Uhuru wa Mtandao wa Intaneti

Kama ambavyo wengi wamebaini, ulimwengu uko katika wakati tete linapokuja suala la uhuru wa mtandaoni. Katika nchi nyingi duniani kote, sheria mpya zimeendelea kuundwa kwa malengo ya kudhibiti mtandao, wakati huo huo wanablogu wakizidi kuwa katika hatari kwa kupaza sauti zao.

Katika mwaka uliopita, mashirika duniani kote yameshikamana pamoja kuliko ilivyowahi kutokea kabla  kupigania uhuru mtandaoni. Kuanzia vita dhidi ya SOPA na PIPA  huko Marekani hadi juhudi za kimataifa zilizomaliza Mkataba wa Kupinga Biashara ya Fedha Bandia (ACTA), tumefikia nyakati za uwazi wa uhuru wa mtandaoni.

Tukiyatambua hayo, vikundi kadhaa hivi karibuni viliungana kuunda Tamko la Uhuru wa Mtandao wa Intaneti, ambalo Mradi wa Kutetea Sauti za Dunia ulikuwa moja ya watiaji sahihi wa awali. Mpaka sasa, Tamko hilo imetiwa sahihi na zaidi ya mashirika na kampuni 1300 na bado zoezi linaendelea kukua. Hapa chini utapata andiko la awali la Tamko hilo. Unaweza kutia saini kuunga mkono tamko hilo hapa; waweza pia kuiona kupitia mashirika mengineyo, ikiwa ni pamoja na EFF, Free Press, Shirika la Access na pia Cheezburger.

 DIBAJI 

Tunaamini kwamba  mtandao ulio huru na wazi  waweza kufanya dunia iwe bora zaidi. Kwa kuufanya mtandao kuwa huru na wazi, tunatoa wito kwa jumuiya, viwanda na nchi kutambua na kuheshimu kanuni hizi. Tunaamini kwamba zitasaidia kuleta ubunifu zaidi, ugunduzi zaidi na kufanya jamii ziwe wazi zaidi.

Tunajiunga na harakati ya kimataifa kutetea uhuru wetu kwa sababu tunaamini kwamba uhuru ni suala muhimu kupiganiwa.

Hebu tujadili kanuni hizi – kubali ama pingana nazo, zijadili, zitafsiri, zifanye kuwa zako na panua mijadala katika jamii yako – kwani mtandao ndio utawezesha hayo.

Ungana nasi kuufanya Mtandao wa intaneti kuwa huru na wazi.

 ILANI

Tunasimama imara kudai mtandao huru na wazi.

Tunaunga mkono michakato wazi na shirikishi ya kutengeneza sera ya mtandao na uanzishaji wa kanuni tano za msingi:

Kauli: Kuto dhibiti mtandao.

Upatikanaji: Kuza upatikanaji wa mitandao ya kasi na nafuu duniani kote.

Uwazi: Kuufanya mtandao wa intaneti kuwa wazi ambapo kila mtu ana uhuru wa kuunganishwa, kuwasiliana, kuandika, kusoma, kutazama, kuzungumza, kusikiliza, kujifunza, kuunda na kubuni.

Ugunduzi: Kulinda uhuru wa kugundua na kuunda bila kulazimika kuomba idhini. Msizuie teknolijia mpya, na msiwaadhibu wagunduzi kwa vitendo vinavyofanywa na watumiaji wa teknolojia zao.

Faragha: Kulinda faragha na kupigania uwezo wa kila mtu kudhibiti namna data na vifaa vyao vinavyotumika.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.