Hispania: Maandamano ya Wachimbaji Madini Yaungwa Mkono na Wananchi

Makala haya ni sehemu ya habari zetu maalumu zaUlaya katika Migogoro.

Maelfu ya watu waliingia mitaani kwa lengo la kuwaunga mkono wachimbaji wa madini wa nchini Hispania, na walijumuika nao walipowasili katika jiji la Madridi baada ya wachimba madini hao kutembea kilomita 400 wakitokea kaskazini mwa Hispania. Maandamano yalianza saa 4 usiku, Jumanne ya tarehe 10 mwezi Juni katika mji wa La Moncloa, palipo na kitovu cha serikali, na yalimalizikia puerta del Sol plaza ya Madridi takribani saa 8 usiku. Wachimbaji hao wa makaa ya mawe wanaandamana kupinga mpango wa serikali ya Mariano Rajoy wa kubana matumizi pamoja na hatua ya serikali hiyo kusitisha ruzuku inayotakiwa kulipwa kwa makampuni ya uchimbaji wa makaa ya mawe ili kupunguza gharama za bidhaa hiyo kwa walaji.

Kusanyiko la kukaribisha kinachojulikana kama “matembezi meusi” (“Black March”) yalifanyika kwa ari iliyochochewa na mshikamano. Raia waliokusanyika hapo waliwapokea wachimbaji madini hao kwa kuwashangilia kwa kuwapigia makofi, maneno ya kuwakubali, misemo iliyoonesha kutambua hisia za wachimbaji hao wa madini pamoja na wimbo wao wa kuonesha namna wanavyo wathamini ambao uliimbwa wakati wa matembezi ya pamoja katikati ya mji mkuu. Wachimbaji hao walipatwa na mshangao kwa jinsi watu walivyojikusanya, jambo ambalo liliongeza chachu ya kile kinachojulikana katika mitandao ya kijamii kama #nocheminera [es] (Usiku wa uchimbaji madini).


Matembezi ya giza yakipita katikati ya jiji la Madrid. Picha na Ismael Naranjo.

Miongoni mwa misemo maarufu ilikuwa, “Ndio tunaweza!”, “Ndio, ndio, (wachimbaji hawa) wanatuwakilisha!” na “Huu ndio mfumo wetu” wakirejelea ushindi wa hivi karibuni wa nchi ya Hispania katika kinyang’anyiro cha michuano ya mpira wa miguu barani Ulaya ambapo nchi hii ilikuwa bingwa. Jambo moja lilikuwa wazi: wale wanaowaunga mkono wafanyakazi hawa wanajisikia fahari na wanajichanganua zaidi na daraja la wafanyakazi kuliko ilivyo kwa wanasiasa au wacheza soka.

Wachimbaji wa makaa ya mawe sio tu kuwa waliangaza mitaa kwa taa walizokuwa wameziweka vichwani mwao, pia walitumia mwanga kwa waandamanaji kama ishara yenye kubeba maana pana zaidi. Sekta nyingine nyingi ziliunga mkono maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na wale wanaoipinga serikali kutoka katika maeneo mbalimbali ya Hispania. Kwa kuwa yalikuwa ni maandamano yenye nia ya kuiasi serikali, zaidi kuliko maandamano mengine yaliyokwisha itishwa nchini Hispania, juhudi za wachimbaji wa madini hawa zimekuwa ni kiini cha harakati za maandamano ya wafanyakazi na yamekuwa ni hatua kali zaidi za kuipinga serikali kwa hatua zake za kutokutoa ruzuku kwa makampuni ya wachimba madini.

Video hapa chini inawaonesha waandamnaji wakionesha mshikamno wao pamoja na wachimba madini waliojitokeza [es]
(Video na Juan Luis Sánchez):

http://youtu.be/6FeZXoupDIo

Kupitia mitandao ya kijamii, watu wengi waliwahamasisha wachimbaji madini kuendelea kupinga hatua ya serikali kusitisha utoaji wa ruzuku kwa makampuni ya kuchimba madini, hatua mbayo ingeweza kusababisha kufa kwa sekta ya madini nchini humo. Idadi kubwa ya watumiaji wa Twita walieleza kupitia twiti zao katika alama ishara #yosoyminero (Mimi ni mchambaji wa madini). Kama ilivyokuwa kwa maandamano yaliyotangulia, mitandao ya kijamii ndiyo iliyotumika kusambaza taarifa kwa kiasi kikubwa, hatua iliyosababishwa na kile watumiaji wake walichokiita #silenciomediático (kimya cha vyombo vikuu vya habari).

Maandamano haya ya kihistoria ya wachimbaji wa madini yalianza tena asubuhi ya Jumatano ya tarehe 11, Julai. Hata hivyo, siku hii ilibadilika na kuwa ya misukosuko zaidi kuliko ile ya maandamano ya awali kutokana na waandamanaji hao kukabiliana vikali na polisi. Zaidi ya watu 76 walijeruhiwa katika migogoro hiyo [es] na takribani watu 10 waliwekwa kizuizini.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.